DOKEZO Sehemu ya kusubiria abiria Kivukoni joto ni kali na feni hazifanyi kazi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna tatizo tunaomba Serikali, Jamii na hasa mamlaka husika zifahamu ili hatua zichukuliwe, ni kuhusu kero ya joto kutokana na msongamano wa watu Kivukoni Jijini Dar es Salaam.

Abiria tunaotumia vivuko tunapata shida sana wakati wa kusubiri Kivuko kwenye lounge kutokana na joto kali linalotokana na msongamano wa watu.

Nashauri waweke hata feni maana watu wanajazana sana na joto kali, feni zilizopo hazifanyi kazi, sijui hata pesa zinazopatikana zinafanyiwa nini!


Pia soma:
 
Lounge ya Kigamboni feni zipo ila zote mbovu na ile lounge ingine feni zimewekwa pembeni tu na hazizidi 7
 
Tafuta pesa kijana ukate VIP, sehemu ya kusubiria ina full A.C mpaka unaganda kama barafu
We jamaa unatuchukuliaje sisi?

Haya onyesha hiyo VIP iko wapi tukakae tunavosubiri kivuko
 
Lounge ya Kigamboni feni zipo ila zote mbovu na ile lounge ingine feni zimewekwa pembeni tu na hazizidi 7
Kwa hiyo umeamua kuja kulalama humu, ofisi zipo hapo hapo Ferry, why hukuenda kutoa malalamiko yako hapo?,nilitegemea ungekuja na mrejesho kutoka kwao na sio kulalama humu n you do nothing, push back inaanzia na wewe sio mwingine
 
Alafu mbona kivukoni joto sio kali sana au wewe ni mgeni kutokea mbeya? usijali utazoea tu
 
Mpaka muive ile ni natural oven sasa uo upepo wa bahari hausaidii, alafu feni haitosaidia maana itapuliza ilo ilo joto,
 
Hapo ni bichi wewe unahitaji zifungwe feni bichi! Huenda umekosea ulipokuwa.
 
We jamaa unatuchukuliaje sisi?

Haya onyesha hiyo VIP iko wapi tukakae tunavosubiri kivuko
Nunua ticket ya vip, watakuonyesha sehemu ya kusubiria, wanakupa hadi juisi na soda. Sitanii hapa
 
Maji si yapo karibu sheikh? Ingieni mpige mbizi, natania mkuu, mimi ilinikuta juzi kati ilikuwa saa nne usiku pantoni lilikuwa moja mbona nilihisi kufa, navuja jasho balaa na sikuwa na leso
 
Ukishaingia kwenye kivuko
Je hizo seat zenu nyie VIP ziko sehemu GANI?
Zipo juu kabisa katikati. Usawa wa anapokaa nahodha. Econom class kuna mateso maana watu ni wengi sana, siku moja ukijaribu vip au vvip hautarudi tena economy.
 
Zipo juu kabisa katikati. Usawa wa anapokaa nahodha. Econom class kuna mateso maana watu ni wengi sana, siku moja ukijaribu vip au vvip hautarudi tena economy.
Mzee tunazungumzia panton SIO meli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…