KWELI Seif Maalim Seif ndiye mwanzilishi wa Umoja Party (UP)

KWELI Seif Maalim Seif ndiye mwanzilishi wa Umoja Party (UP)

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Chama cha siasa kilijulikano kama Umoja Party (UP) kimeomba usajili wa muda. Chama hicho tayari kimewasilisha maombi ya usajili wa muda ili kuanza kutafuta wadhamini kwa lengo la kupata usajili wa kudumu. Maswali yalikuwa mengi kuhusu nani hasa mwanzilishi wa chama hicho.

UMOJA2.png
 
Tunachokijua
Mwasisi wa Umma Party ni Seif Maalim Seif, ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama hicho kinachojinasibisha na sera za John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwaka 2020 Seif Maalim Seif aligombea urais kupitia Alliance for Africa Farmers Party (AAFP). Kabla ya kugombea urais Seif aliwahi kugombea ubunge jimbo la Welezo visiwani Zanzibar mwaka 2016, lakini hakufanikiwa.

Seif ambaye alikuwa mwanachama wa kawaida wa AAFP amesema ameachana na chama hiko na kuanzisha cha kwake kwasababu aliyoitaja kuwa "Msingi uliochimbwa na mtu mwingine mwenye maono yake, kwa hiyo nilijaribu kuepuka sintofahamu na kukorofishana. Watu walikuwa na maono yao, sikutaka ya kwangu yaonekane bora zaidi kuliko ya kwao. Kama yangu ni bora basi nitayaweka katika muktadha wa Umoja Party. Kwa hiyo Umoja Party ni matokeo ya mkusanyiko wa uzoefu, upeo na uzalendo uliotimia wa miaka kadhaa hadi kuasisiwa kwake.”

Chama cha Umoja kinajipambanua kiitikadi kuwa kinaazimia kutumia utajiri wa rasilimali uliopo Tanzania kunufaisha wananchi kwanza na kutatua tatizo kubwa la ajili linalowakabili watanzania.

Seif ni muumuni wa siasa za utulivu na kuleta mabadiliko kwa njia za majadiliano. Kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 aliwahi kunukuliwa akipinga vikali siasa za kusambaza maneno ya uchochezi ambayo yangehatarisha amani nchini. Seif alisema kuwa vyama vyote vina lengo moja la kuongoza dola, hivyo basi lazima vifanye siasa za kiungwana, pasi kuchochea vurugu kwani Tanzania ni moja na hakuna nyingine.
Back
Top Bottom