Sekela chicken

Sekela chicken

sekela ni kuku wa kuchoma. anapakwa viungo halafu anachomwa kwa moto mchache. mimi huwa natengeneza sekela siku nikifurahi. simply nawasha jiko la mkaa naweka nyavu za kuchomea kisha juu namuweka kuku aliye tiwa viungo. akishaiva nauliza wapi kilimanjaro baridi. mia

anapakwa viungo vipi sasa?
waweza elezea?
 
anapakwa viungo vipi sasa?
waweza elezea?

pilipili,chicken masala,vinegar,wengine huweka mdalasini uliosagwa,soy sauce muhimu!chumvi,mimi huweka hata na mtindi pia kuweka taste zaidi!chumvi thn naoka kwenye moto wa wastani!
ukiweka kwenye mkaa ndo poa,ile oven la mkaa lile!
aive tratiiibu!
BTW ule mgahawa wa vyakula vya wenye sukari uliishia wapi?
bonge la hela ile unajua!?
 
anapakwa viungo vipi sasa?waweza elezea?
mkuu siku hizi wamelahisisha. ukienda duka la vyakula ukaagiza viungo vya sekela wanakupatia. yaani vinakuwa kwenye pakiti vishachanganywa tayari. wewe unafika na kupaka tu. nenda k/koo. mia
 
The Boss, King'asti, et al....kuna hii "mbu recipe" hebu jaribu [marination] kila mtu na ingredients Qty anavyojiskia;

Changanya;
1. Maziwa mgando
2. Kotmiri aka Dhania aka Coriander
3. Pilipili mbuzi kidogo
4. Limao (juuce)
5. Tomato paste aka puree
6. Vitunguu swaumu na tangawizi
7. Vitunguu maji kidogo
8. Olive Oil kidogo
9. Curry powder (simba mbili?)
10. Chumvi na pilipili manga (unga)

Blend mchanganyiko huu,
Changanya kwenye kuku wako (mbichi)...

uhifadhi kwenye fridge au funikia kwa angalau saa moja kabla hujachoma kwenye Oven au Open pit BBQ.

Enjoy!
 
Last edited by a moderator:
chicken "SEKELA", sina uhakika hili jina sekela lina asili ya wapi katika ulimwengu wa mapishi kama ilivyo chicken tikka n.k..kwa ufupi ni kuku wa kuchoma (grill, bbq sijui vinafanana!).

Mahitaji
Kuku alietolewa ngozi,(vipande, au mzima) kulingana na upendavyo .
Kitungu thoumu na tangawizi3 vijiko ,
Limau au ndimu,
Chumvi kiasi
Binzari 2 vijiko ,
Masala ya Tanduri au Garam 2 vijiko
Pilipili mbichi iliyosagwa au black pepper 1kijiko
Ukwaju au vinegar 1/2 kikombe,
Soy sauc 3 vijiko.
Asali au sukari vijiko 3 au kadri unavyopenda radha ya utamu.
Rangi ya chakula(food color) kias (red yavutia zaidi, japo me hupendelea kipapripapri ama kijani) , Ongeza maji kidogo kama mchanganyiko utakuwa mzito sana, baada ya hapo una mloweka kuku wako(vipande, ama aliepasuliwa tu kati) kwenye mchanganyiko kisha una mwacha kwenye friji kwa muda wa masaa mawili. Hapo sekela anakuwa tayari kwa kuchomwa.

mbona nafanya hvyo lakin anababuka ngoz na kuwa mweus na bado hana radha wa sekela au nakosea wapi
 
Back
Top Bottom