Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mwili unaogombaniwa na familia mbili ambao ulizikwa katika kitongoji cha Dungi, Kijiji cha Kibosho Kindi, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, umefukuliwa leo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya vina saba (DNA).
Mwili huo unaodaiwa kuwa wa Richard Shoo, (31)aliyefariki Juni 16,2024 na kuzikwa Juni 25, mwaka huu, nyumbani kwao Dungi, umefukuliwa kwa ajili ya uchunguzi na vipimo vya vinasaba (DNA) baada ya familia ya Jackson Joseph (29) kuibuka na kudai kuwa mwili huo uliozikwa sio wa marehemu Shoo na kwamba ni wa kijana wao Jackson.
Polisi walilazimika kuomba kutumiwa kibali hicho kwa simu ambacho walidai walikiacha ofisini, ambapo hata hivyo familia ilikataa na kudai wanahitaji kukiona hali ambayo ilifanya kuahirishwa kwa zoezi hilo.
Leo Septemba 4,2024, familia zote mbili, zilifika mahakamani na amri kutolewa kaburi likafukuliwe ili mwili huo utolewe na kupimwa DNA, kujiridhisha ni mwili wa nani.
Baada ya amri hiyo, saa 9:20, Askari polisi sita wakiongozwa na mkuu wa upelekezi Wilaya ya Moshi, wakiambatana na Madaktari wawili na familia ya Jackson Joseph akiwemo mama yake mzazi, walifika nyumbani kwa Shoo kwa ajili ya kufukua kaburi hilo, ambapo pia kuliibuka vurugu za baadhi ya wananchi na familia kuonyesha hawajaridhishwa na kinachotaka kuendelea.
PIA SOMA
- Polisi wafeli kufukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi baada ya Familia kudai kutoshirikishwa