GE2025 Sekeseke la Mpina ni Maigizo ama ni muendelezo wa kuibagaza Demokrasia?

GE2025 Sekeseke la Mpina ni Maigizo ama ni muendelezo wa kuibagaza Demokrasia?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

JF Analyst

Member
Joined
Jan 30, 2025
Posts
11
Reaction score
14
Simulizi ya Luhaga Mpina imebaki kama moja ya hadithi za kisiasa yenye kusisimua zaidi katika historia ya uchaguzi wa Tanzania. Fikiria Kutoka kwenye kura 92.3% za uteuzi ndani ya chama chake, kisha kuwekewa pingamizi mara ya kwanza na kulishinda kwa kesi mahakamani, kisha kuangukia pua kwa mara ya pili mbele ya Tume dhidi ya safari ya kuelekea Ikulu.

Soma pia
Kitendo cha Mpina kutimkia ACT kiliibua hisia tofauti na maoni kinzani miongoni mwa watu, wengine wakiamini kuwa haukuwa uamuzi mzuri kwani walitegemea angejiunga na chama ambacho wao wanakitizama kama chama chenye upinzani thabiti. Lakini wengine wakawa na mtizamo kwamba Mpina anaenda kuongeza nguvu ya ACT hususani kukifanya chama hicho kitambulike zaidi kanda ya Ziwa ambapo ndipo anapotokea.

Tukio lililovuta hisia za watu wengi zaidi ni pale ambapo Chama cha ACT kilipompitisha Luhaga Mpina kwa zaidi ya asilimia 92.3 kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye mbio za Urais, ikiwa ni siku chache tu toka alipojiunga.

Soma pia GE2025 - Luhaga Mpina apitishwa kuwania urais kwa tiketi ya ACT kwa 92.3%

Hii ilichukuliwa kama Move itakayowanufaisha zaidi ACT huku wengine wakiamini kuwa Mpina ametumwa na CCM kwenda kudhoofisha upinzani na pengine baada ya uchaguzi atapata uteuzi kutoka serikalini kama ilivyofanyika kwa Anna Mghwira aliyepata ukuu wa mkoa baada ya kugombea 2015. Wengine walienda mbali zaidi na kutamani angegombea ubunge kuliko Urais ambao ulionekana kuwa kama maigizo tu. Na wengine wakiamini ya kuwa anaenda kuleta upinzani kwa namna moja ama nyingine.

Baadhi ya matukio aliyoyafanya Mpina yalikoleza moto zaidi wa mjadala kuhusu kama ni kweli ameamua kuwa mpinzani ama la!. Mathalani wakati akiwa kwenye ziara ya kutafuta wadhamini Mpina alionekana akiwa na Tisheti lenye picha ya aliyekuwa Rais wa Tanzania kupitia CCM, chama ambacho Mpina alikuwepo siku kadhaa nyuma.

Mapingamizi aliyowekewa Mpina kwa nyakati tofauti yameendelea kuchagiza mijadala tofauti, ikionekana kuwa Msajili anakosa uthabiti wa kuchukua maamuzi yanapokuja masuala ya chama tawala ilhali ya upinzani yanachukuliwa kwa uzito na hatua huchukuliwa kwa uharaka zaidi. Hili linavunja imani ya wananchi dhidi ya mfumo mzima wa uchaguzi.

Mwenendo wote huu haiwi mwisho na haitakuwa mwisho katika taifa lililochagua kwenda kwa njia ya kidemokrasia, bali inakuwa ni hatua nyingine muhimu ya kuitengeneza kesho iliyo bora zaidi.

Kwa ujumla matukio ya Kuenguliwa, kurudishwa na kisha kuenguliwa tena kwa mgombea wa ACT, Luhaga Mpina, ni matukio yanayobeba ishara kadhaa muhimu kisiasa nchini Tanzania ikiwemo:

  • Mwenendo wa Tume ya Uchaguzi na Mamlaka za Uchaguzi
    Inazua maswali juu ya ufanisi, uwazi na uthabiti wa maamuzi ya taasisi zinazohusika na uchaguzi. Mabadiliko ya mara kwa mara yanaweza kuashiria ukosefu wa msimamo thabiti au changamoto katika taratibu za kisheria na kiutendaji.

  • Taswira ya Demokrasia ya Vyama Vingi
    Kuenguliwa na kurudishwa mara kadhaa kwa mgombea, si tu kwa nagzi ya Urais lakini pia hata kwa ngazi ya ubunge na udiwani ama serikali za mitaa kama ilivyofanyika katika awamu ziizopita kunatengeneza picha kwamba nafasi ya vyama vya upinzani kushiriki kikamilifu bado inakabiliwa na changamoto. Hii inaweza kudhihirisha mvutano kati ya dhamira ya kuendesha uchaguzi wa kidemokrasia na utekelezaji wake kivitendo.

  • Ishara kwa Wananchi
    Kwa wapiga kura, hali hii inaweza kupunguza imani kwa mfumo wa uchaguzi. Wengine wanaweza kuamini kuwa upinzani unakandamizwa, huku wengine wakihisi kwamba mgombea hana uthabiti au uhalali wa kisheria. Huku upinzani ukionekana kutokuwa na uimara unaotakiwa ili kukiondoa chama cha CCM madarakani, mathalani kauli za aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba Humphrey Polepole kudokeza kuwa baadhi ya vyama vya upinzani ni ‘Projects’ za CCM. Lakini pia mwenendo wa Rais Samia na Zitto Kabwe pale Kigoma unazidi kudhoofisha kabisa imani waliyonayo wananchi dhidi ya upinzani uliopo.
 
Mhubiri 3:1-8
Kila jambo na wakati wake madhila anayofanyiwa Luhaga Mpina na ACT, CCM, Mahakama na INEC ni mapito ya kumkomaza kisiasi muhimu ajifunze kwa makini pia asisahau kuwa bado ana umri mdogo avute subra kungoja wakati wake ufike.
 
Mhubiri 3:1-8
Kila jambo na wakati wake madhila anayofanyiwa Luhaga Mpina na ACT, CCM, Mahakama na INEC ni mapito ya kumkomaza kisiasi muhimu ajifunze kwa makini pia asisahau kuwa bado ana umri mdogo avute subra kungoja wakati wake ufike.

Du! Aisee.. 😀​

 
Mhubiri 3:1-8
Kila jambo na wakati wake madhila anayofanyiwa Luhaga Mpina na ACT, CCM, Mahakama na INEC ni mapito ya kumkomaza kisiasi muhimu ajifunze kwa makini pia asisahau kuwa bado ana umri mdogo avute subra kungoja wakati wake ufike.
Kwahiyo Mpina achukulie hilo kama somo na njia ya kumkomaza? Je hiyo awamu nyingine unamaanisha atashinda kupitia upinzani ama atarudi nyumbani?
 
Hakika hili ni darasa tosha kwake na kuhusu ushindi haijalishi upo chama gani itategemea zaidi mvuto wake kisiasa na namna gani atajiuza kisiasa kwa raia.
Nina uhakika ataweza kumantain hivi japo sio rahisi.
 
Kubwa zaidi ni la kibaraka Zitto Kabwe kumpigia debe mgombea wa CCM Samia Suluhu Hassan
 
Back
Top Bottom