UTPC
Journalists' Union
- Apr 17, 2026
- 51
- 38
Sehemu ya pili ya ripoti hii ya uchunguzi, wananchi walieleza namna miundmbinu, jiografia ya wilaya ya Uvinza na hali ya kiuchumi kuwa chanzo cha tatizo la mdondoko wa wafunzi, katika makala hii ya tatu na ya mwisho, wananchi wanaeleza kuwa licha ya uwekezaji mabilioni ya fedha katika sekta ya elimu nchini, hali ya mdondoko wa wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na kushindwa kujiunga au kukamilisha elimu ya sekondari ni “bomu” linalosubiri kulipuka.
Wadau wa elimu, viongozi wa dini na wananchi wa wilaya hiyo wameibuka na kutoa suluhu zinazolenga kunusuru mustakabali wa watoto ambao wengi wao wanaishia kwenye vijiwe, masokoni na kujiingiza kwenye ndoa za utotoni.
Ibara ya 3. 2. 12 na 3.7.1 ya sera ya elimu ya mwaka 2014 (toleo la 2023) zinaeleza wajibu wa serikali kuhakikisha inajenga mazingira mazuri ya wanafunzi kujifunza ambapo inabainisha kuwa, “Serikali inawajibika kujenga madarasa, maabara, na nyumba za walimu ili kukidhi ongezeko la wanafunzi na kupunguza umbali mrefu wa kwenda shuleni”.
Ofisa elimu divisheni ya msingi na awali wa wilaya ya Uvinza, Hilary Bitwaye, anaeleza ili kuondoa changamoto ya kutembea umbali mrefu ambao ulitajwa na wananchi pamoja na mamlaka kama sababu ya mdondoko wa wanafunzi serikali imetoa zaidi ya milioni 600 kujenga sekondari mpya.
Anasema fedha hizo zimetengwa na halmashauri ya wilaya hiyo katika mwaka huu wa fedha 2026/2027 na kwamba ujenzi utaanza hivi karibuni ilipo shule ya msingi Ruchugi hatua inayotajwa kupunguza muda wa kutembea kwa wanafunzi na badala yake watasoma katika eneo hilohilo
Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la serikali lililotolewa na Waziri mkuu Mwigulu Nchemba alipokuwa bungeni mnamo mwezi Aprili, 2026 la kutenga bilioni 139.28 kupitia mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 4193 na matundu ya vyoo 13,943 huku serikali kuu ikitenga bilioni saba kwa ajili ya ujenzi wa maabara 233.
Kama suluhisho ofisa elimu sekondari wa wilaya hiyo, Julius Kakyama anaeleza kuwa kila ilipo shule ya msingi itajengwa sekondari na kwamba toka mwaka juzi halmashauri hiyo imefanikiwa kujenga sekondari saba ikiwemo Uvinza, Kamigoti, Kilando B, Mwela B na Mtego wa Noti ili kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi.
Kakyama anaiombe serikali kuwaongezea nguvu na kupata fedha kutoka serikali kuu ambazo zitaiwezesha halmashauri hiyo kujenga sekondari nyingine mpya 24 akiamini kwamba hatua hiyo itapunguza mdondoko wa wanafunzi wanaoshindwa kuingia kidato cha kwanza.
“Kuna watoto wanaacha shule kwa sababu ya umbali ambao baadae wanakwenda kutafuta pesa za kujikimu na wanarudi kuomba nafasi kabla ya miaka miwili ili waendelee na masomo, huwa tunawapokea lakini shule zikiwa karibu hawa wanaopenda kusoma watasoma bila changamoto,” anaongeza ofisa huyo.
Mwananchi wa eneo hilo, la Kamigoti Yahaya, anatoa suluhu kuwa wananchi wapewe elimu ya kutunza fedha kwa ajili ya watoto wanaomaliza darasa la saba akieleza kuwa, kuwe na mfumo wa lazima wa wazazi wanaoshindwa kuwapeleka watoto shuleni kwa wakati.
Aidha, anaongeza kuwa jamii inatakiwa kuacha kusubiri mavuno ya mwezi wa tatu na badala yake iweke kipaumbele cha elimu sawa na maandalizi ya sikukuu za Krismasi, Eid au mwaka mpya.
Msisitizo wa Kimigoti unaenda sambamba na wito wa Amisa George, ambaye anakiri kuwapeleka watoto shambani kutafuta riziki kutokana na ugumu wa maisha, akisisitiza kuwa wazazi wabebe majukumu yao.
Naye mzazi Raphaeli Bizunda anatoa hoja kuwa walimu waache kutoa adhabu kali zinazowakimbiza watoto kuendelea kujifunza, akitoa mfano wa sekondari ya Mazungwe ambayo watoto wamekuwa wakipatiwa adhabu nzito zisizoendana na kosa alilolifanya mtoto wala umri wake.
“Walimu na bodi ya shule wakae pamoja na wazazi ili kuweka utaratibu wa adhabu ambazo ni malezi na si mateso, ili kurudisha morali ya wanafunzi, tutengeneze mfumo ambao mwanafunzi atamuona mwalimu kuwa mlezi na si askari,” anafafanua Bizunda.
Ibara ya 3.8.1 ya sera hiyo Inasisitizwa kuwa Serikali na wadau watajenga mazingira salama yanayomlinda mtoto dhidi ya ukatili wa kijinsia na adhabu kali, mambo ambayo ni vyanzo vikuu vya wanafunzi kuacha shule.
Vilevile Yekonia Lalanika mkazi wa Kazuramimba, anasema miundombinu ya shule za sekondari ikiboreshwa hussusan uwepo wa madawati ya kukalia italeta chachu na hamasa ya wanafunzi kupenda shule
“Sasa hivi kuna mwamko wa elimu, watoto wengi wanasoma, sasa unakuta shule ya msingi alikotoka alikuwa anakaa chini, akifika sekondari anakaa tena chini, mwanafunzi anaona hakuna haja ya kusoma kwakuwa haoni utofauti wa sekondari na shule ya msingi,” anaeleza Lalanika
Anaongeza zaidi kuwa yapo madarasa ambayo watoto wanakaa hadi 200, kutokana na wengi wao wametoka shule nyingi za msingi na kukutana katika shule moja ya sekondari ya kata na kwamba kutokana na mazingira hayo mtoto anakosa hamasa ya kuendelea na shule na kuona ni bora abaki nyumbani.
Yasini Chuma, Shehe wa msikiti wa Shia Kazuramimba anasisitiza umuhimu wa kurejesha au kuongeza muda wa masomo ya dini shuleni akidai kuwa elimu ya dini inamjenga mtoto kuwa na nidhamu na heshima kwa walimu na wazazi.
“Bila imani, watoto wanapata elimu ya ‘kupiga mziki wa ho haa’ na wanakuwa na nidhamu mbovu katika jamii, serikali itenge muda mzuri wa watoto kujifunza elimu ya dini ili warejee katika msingi ambao umeharibika,” anaeleza shehe Chuma.
Suluhu ya Issa Bakari, inaegamia katika kampeni za hamasa zinazopaswa kuanzia ngazi ya kitongoji, ambapo kamati za ukatili na maafisa maendeleo ya jamii wanapaswa kuingia mitaani kuhoji kwa nini watoto hawapo shuleni.
“Tunapaswa kuanza na malezi kwakuwa katika familia hakuna malezi bora ya watoto, wazazi wanapambana na shughuli zao, mtoto anakosa muelekeo, anaamua kufanya anayoona kwake ni sawa, tunawaumiza watoto” anafafanua Bakari
Mwenyekiti wa kijiji cha Kazuramimba, Moshi Kamlonga, anapendekeza asasi za kiraia kutoa elimu ya makuzi na malezi kwa wazazi ili waone manufaa ya elimu kwa kizazi kijacho akisisitiza juu ya umuhimu wa tatizo la watoto kujiingiza kwenye michezo (Playstation), ubashiri na kurusha filamu jambo la ambalo limetajwa kuwa mwiba kwa elimu ya Uvinza.
Vilvile anashauri ujenzi wa vyuo vya ufundi kama VETA katika wilaya hiyo ili kuwapokea watoto ambao hawakuweza kuendelea na mfumo rasmi wa sekondari, badala ya kuwaacha mtaani wawe wavuta bangi na wanyang’anyi.
Naye Kijana Thomas Roma anabainisha kuanzishwe kampeni ya kuwakamata na kuwashitaki waajiri wanaotumia watoto wadogo kuuza mayai au kufanya kazi za ndani.
Ernest Daudi (huyu si Muhanga aliyetajwa katika makala ya kwanza), mjumbe wa kijiwe cha bodaboda, anasema wao wenyewe wameanza kujidhibiti kwa kutowaruhusu vijana chini ya miaka 20 kuendesha bodaboda ili kuwalinda dhidi ya makundi ya kihalifu na vitendo vya ulawiti vinavyolenga kuwarubuni.
Hamis Milambo mkazi wa Kazuramimba anapendekeza mabadiliko ya mitaala ili ifundishe ujuzi wa kujiajiri akieleza kuwa vijana wengi wanasema wanasoma lakini hawafanikiwi, hivyo elimu ya ujuzi ndiyo mkombozi pekee.
Shiti Ndungulu, mwenyekiti wa serikali ya mtaa, anahitimisha kwa kusema, “Serikali ni mimi na wewe.” anashauri wazazi kuacha kuitupia lawama serikali pekee na badala yake wafuatilie mienendo ya watoto wao kila siku ili kuzuia wasiingie “chaka” badala ya kwenda shule.
Akichangia hoja hiyo, mfugaji Ilankunda Stefano anasema ili kuepuka kuhamahama wafugaji watumie eneo la malisho lililotengwa kwa ajili ya mifugo yao huku wanaohama wakitafuta rutuba watumie mbolea kuboresha uzalishaji kwakuwa kuhama hama kunaharibu mustakabali wa maisha ya watoto na ya kwao pia.
Kwa upande wa ofisa maendeleo mkoa wa Kigoma, Msafiri Nzunuri anazitaka kaya zifanye kazi tofautitofauti ili zisitegemee kilimo pekee kama chanzo cha kipato, akitaja shughuli hizo zifanywe na wote baba na mama.
Anaongeza kuwa ili kupata mitaji ya kuendesha shughui hizo wajiunge katika vikundi vya ujasiriamali ili wapate mikopo inayotolewa na serikali isikuwa na riba inayotokana na asilimia 10 ya mapato kutoka halmashauri kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
“Ipo mikopo mingine ya riba nafuu inayotolewa na benki ya NMB, kiwango cha juu cha fedha ni Tsh. 4,000,000 ambayo inalipiwa asilimia 7 ya riba kwa mwaka fedha ambayo wakiitumia kufanya biashara na kilimo wanaweza kulipa madeni na kubaki na fedha za kuendesha maisha yao, ila lazima wafuate taratibu,” anafafanua Nzunuri
Anaongeza zaidi kuwa wazazi watenge pesa maalum kwa ajili ya shule na chakula akieleza kuwa kwa familia zilizothibitika kuwa haziwezi kuwasomesha watoto kutokana na uzalishaji duni serikali inashirikiana na wadau wengine ili kupata ufadhili wa kupata mahitaji ya msingi ikiwemo sare za shule.
Zaidi anaeleza kuwa wazazi wafanye kazi kwa bidii na wawajibike kwa watoto wao akidai sio kweli kwamba watoto wote wasiokwenda shule wazazi hawana fedha ni kwasababu hawana mwako na kwamba hakuna uwekezaji mkubwa kuliko elimu hivyo wazazi wawekeze kwa watoto wao
“Utelekezaji wa watoto sio jambo la kujisifia, mzazi wa kike na wa kiume wawalinde watoto wao, wazazi wakizisimamia familia zao kwa ushirikiano hapatakuwa na mtoto ambaye hatakwensa shule, wadumishe upendo ili watoto wasome na kutimiza ndoto zao”.
ANDIKO LA: Adela Madyane – Kigoma
Makala imeandaliwa na Mwandishi anayeshiriki katika programu maalum ya kukuza uandishi wa maslahi kwa umma (Public Interest Journalism Fellowship) inayoratibiwa na UTPC kwa kushirikiana na IMS.