Sekondari zisizo za amali zaingia mkenge kufundisha mtaala mpya

Usishangae mkuu,
Nilipotia mada nilikuwa sahihi kwamba sekondari kadhaa zisizo za amali zimeshaingia mkenge.
Huyo jamaa unayemshangaa ni mmojawapo waliouvaa mkenge.

Kibaha wameingia mkenge huo sekondari nyingi tu na hakuna wa kuwaamsha.
Ndiyo maana nimeshangaa. Sisi wengine ni business as usual.
 
Unachosema ni kweli, na siye huku mkuu wetu na mtaaluma walieleza hivyo kwenye kikao; tuanze kutumia mtaala na mihitasari mipya(syllabi), bahati nzuri tukawepo watu wenye ufuatiliaji na uelewa wa protokali za serikali, tukawaeleza mabadiliko ya syllabus huja na waraka wenye kuonyesha mpango wa utekelezaji.

Baada ya kujadiliana na kuwekana sawa baadae ilibidi mkuu aulize kwa Afisa elimu ambaye alieleza vyema kuwa mtaala mpya na mihitasari yote mipya iliyo tolewa na utekelezaji wake ni kwa shule chache teule. Zingine ziendelee na utaratibu wa zamani hadi waraka utakapotolewa.

Nikupongeze mtoa mada kwa kutanabahisha hili, ni kweli kuna watu wakisikia tu Jambo limeongelewa bungeni au kwenye vyombo vya habari, hukurupuka na kuanza utekelezaji bila ya waraka au miongozo ya utekelezaji wa Jambo husika na hivyo kuleta mikanganyiko.
 
Safari ya Elimu yetu bado inakipindi kigumu kufikia malengo sawa na Dunia inavyotaka.
 
WTF is amali?? Kwani neno “ufundi” lina shida gani?
Zanzibarization of Tanzania. Amali ni neno linalotumika Zanzibar kumaanisha ufundi. Mafunzo ya amali = mafunzo ya ufundi = vocational training.
 
Daaaa basi sawa tùipe muda close monitoring
 
Ni kweli. Hutakiwi kukldanganywa na watendaji wa halmashauri ya Kibaha.
 
Halafu vikekomaa na vinapenda pesaaaa.
 
Neno 'amali' ungejaribu kuliweka hata kwa kiingereza,tujue.
amali ni neno la wazanzibari linalovuka bahari kwa kasi kimatumizi kuja bara , huku sisi tunatumia maneno 'ufundi stadi' badala ya neno hilo amali

mathalan, veta ni vyuo vya ufundi stadi ila kwa zenji wanaita vyuo vya amali
 
Zanzibarization of Tanzania. Amali ni neno linalotumika Zanzibar kumaanisha ufundi. Mafunzo ya amali = mafunzo ya ufundi = vocational training.
Wamezingatia mazingira
 

Attachments

  • IMG-20240129-WA0000.jpg
    66.7 KB · Views: 5
  • IMG-20240129-WA0000.jpg
    66.7 KB · Views: 9
  • IMG-20240129-WA0001.jpg
    63 KB · Views: 5
kwani mtaala mpya lazima shule iwe na ufundi? Mtaala mpya hata masomo ya sayansi na arts bila ufundi Kuna mtaala wake mpya
 
Hatimaye Commissionerwa Elimu ametuma taarua ya kuzionya secondary zilizoingia mkenge tena akatishia kuzifutia registration iwapo zitaendelea kufundisha mkenge ziliouingia.
 
Amali ni nini na hizo shule ni zipi?

Kinyume na hapo hii ni chai kama chai zingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…