KERO Sekretarieti ya Ajira (ICT) wana tatizo la kutojibu email wanazotumiwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ninaomba kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, hasa upande wa TEHAMA (ICT), wawe wanapokea na kushughulikia kwa wakati barua pepe (email) tunazotuma.

Inasikitisha kwamba unatuma email yenye tatizo muhimu kwenye akaunti yako, lakini inapita mwezi hadi miezi bila majibu wala mabadiliko yoyote. Wakati huo huo, wao ndio wenye uwezo wa kurekebisha changamoto hizo. Ukipiga simu, mara nyingi ni kuahirishwa tu bila msaada wa moja kwa moja.

Hali hii inatunyima haki ya kuitwa kwenye usahili, kwani unaweza kuomba kazi ukaishia kuambiwa “not shortlisted” kutokana na tatizo lile lile ulilolipigia kelele kupitia email bila kufanyiwa kazi. Tunaomba mtusikilize na mtuhurumie, kwani nasi tunahitaji ajira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…