Career Mastery Hub
Member
- Mar 23, 2023
- 93
- 108
SEKRETARIATI IPITIE TENA NA KUREKEBISHA MAKOSA KWA WAOMBAJI WENYE SIFA
Na Josephat H +255 656 480 968
Sekretarieti ya Ajira inastahili pongezi kwa uwazi wake katika mchakato wa kutangaza majina ya walimu wanaostahili kufanya usaili. Uwajibikaji na uwazi huu huongeza imani kwa taasisi, kwani kila mwombaji ambaye hakuitwa amepewa sababu. Hata hivyo, kuna maeneo machache ambayo yanahitaji maboresho ili kuhakikisha usawa na haki kwa waombaji wote. Makala hii inalenga kutoa mapendekezo ya maboresho hayo.
1. Mapitio ya Waombaji Walioachwa kwa Sababu Zisizopaswa
Sekretarieti ya Ajira inapaswa kufanya mapitio ya baadhi ya waombaji ambao hawajaitwa kwa sababu ambazo hazikupaswa. Makosa ya kibinadamu au bahati mbaya yanaweza kutokea katika idara zinazopitia maombi wakati wa mchakato wa uchambuzi na uorodheshaji (screening and shortlisting phase).
Mfano: Kuna watu wanadai waliweka vyeti vilivyokuwa vimesajiliwa na mahakama au wakili lakini walitemwa kwa sababu ya "Academic certificate not attached" au "Academic certificate not Certified by magistrate/advocate." Inapotokea mwombaji ameomba kazi mbili zilizofungwa siku moja, lakini amekuwa shortlisted katika somo moja na not shortlisted katika somo jingine kwa sababu hizo, inaonyesha kuna makosa ya kiufundi yamejitokeza.
2. Uhalali wa Waombaji wa Fani Tofauti
Kwa mujibu wa tangazo la kazi, watu ambao hawakusomea ualimu kama taaluma ila wamesoma somo fulani la kufundishia wanaweza kuomba nafasi hizi na wamekidhi vigezo. Hata hivyo, wapo ambao wamekuwa shortlisted na wengine wenye vigezo sawa wamekuwa not shortlisted kwa sababu ya "Post Graduate Diploma in Education not attached."
Mfano: Mtu aliyesoma "Bachelor of Science in Mathematics" anaweza kuomba kazi ya ualimu wa Hisabati. Lakini baadhi ya watu wenye sifa sawa wamekataliwa kwa sababu zisizo sahihi, jambo linaloonyesha timu ya uchambuzi haijafahamu sheria vizuri.
3. Uhakiki wa Vyeti na Viambatisho
Kuna waombaji ambao wameambiwa vyeti vyao havikuthibitishwa na mahakama au wakili, ilhali walikuwa wameweka vyeti vilivyothibitishwa. Ni muhimu kwa Sekretarieti kuhakikisha wanafuatilia viambatisho hivyo kabla ya kutoa majibu ili kila mwenye haki apewe haki yake.
Mfano: Ikiwa mtu aliweka vyeti vilivyothibitishwa lakini bado alikataliwa, Sekretarieti inapaswa kupitia upya nyaraka hizo ili kuhakikisha hakuna makosa yaliyotokea.
4. Ushauri kwa Waombaji
Waombaji wanashauriwa kushughulikia maombi yao ya kazi kwa umakini, kufuata maelekezo na sheria zilizoorodheshwa kwenye tangazo la kazi. Kushindwa kufuata maelekezo ni kosa ambalo hakuna muajiri anayeweza kulikubali na usitegemee huruma.
Mfano: Hakikisha vyeti vyako vinavyosomeka na kuweka au kufanya kama ilivyoelekezwa kwenye masharti ya tangazo la kazi ili kuepuka matatizo baadaye.
5. Kukata Rufaa
Kwa wale ambao walikidhi masharti ya tangazo na kuweka kila kitu kama kilivyoainishwa kabla ya dirisha la maombi kufungwa, na wamekosa nafasi kwa sababu zisizoeleweka, wanayo haki ya kukata rufaa. Sekretarieti inapaswa kushughulikia rufaa hizi kwa haki na uwazi.
Mfano: Mtu ambaye aliweka vyeti vyake vilivyothibitishwa lakini bado hakuitwa, anapaswa kuwa na nafasi ya kukata rufaa na kupewa sababu kamili za kwanini hakuitwa.
6. Uwekaji Wazi wa Matokeo ya Usaili
Tunaiomba serikali kuweka wazi majibu ya usaili wa mdomo (oral interview) ili mtu aweze kujitathmini kwa namna alivyo fanya usaili na uhalisia wa maksi alizopewa. Hii itasaidia mtu kujua nafasi yake na kuona kama ni sahihi kutopangiwa kazi lakini kubaki kwenye kanzidata (database).
Hitimisho
Kwa kuhitimisha, ni muhimu kwa Sekretarieti ya Ajira kuboresha mifumo na taratibu zao ili kuhakikisha haki na uwazi kwa waombaji wote. Hili litasaidia kujenga imani na kuongeza ufanisi katika mchakato wa ajira.