Sekretarieti ya Ajira, kwanini mruhusu TRA kutangaza ajira zao? Naiona ile TRA ya makabila ikirudi kwa kasi

Lubengera

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2019
Posts
963
Reaction score
1,551
Sekretarieti ya ajira mmekuwa msaada mkubwa sana kwa vijana wasio na connection kupata ajira.

Niukweli usio pingika Sekretariet ya Ajira mko fair sana katika kutafuta watumishi wa Umma, hakuna upendeleo wala vimemo, anaye ajiriwa kimsingi anakiwa amefanya vyema kwenywe Interview.

Kitendo cha kurudisha ajira hizo kwenye Taasisi husika kinarudisha nyuma jitihada za kuondosha ukabila katika Taasis mbalimbali Nchini.

Sekretarieti ya Ajira, tunaomba mrudishe ajira za TRA kwenu, ambao watoto wetu wameshaweka nyaraka mbali mbali katika mfumo wenu wa ajira za umma.
 
Una hoja Mkuu.. Ila kama nakumbuka Mhe. Namba 1 aliwapa Kibali kwa madai kuwa walilalamika kucheleweshwa kwa mchakato wa kuwapata watumishi wapya
 
Meiner Meinung nach sollte sich PSRS mit allen Regierungsämtern befassen, einschließlich halbstaatlicher Regierungsämter. Diese TRA-Beiträge sollten tatsächlich über PSRS beworben werden
 
Nadhani ilikuwa ni swala kuwasisitiza Utumishi kuharakisha, na sio kuhamisha mazima.

PSRS wako fair sana kwa usaili, very fair, na hili ndio limenileta hapa kutetea vijana wasio ma connection.
Uko sahihi kabisa mkuu.. Ngoja tuone maana Mhe. Dr. Namba 1 alisema huwa anapitapita huku kusoma mawazo ya wadau..
 
1. Nawaza vijana kwenda kwa wanasheria tena kufuata certified copies za vyeti, wakati tayari PSRS waliwarahisishia, kwa maana ya nyaraka zote kupatikana kwenye tovuti ya Utumidshi.

2. Nawaza mambo ya connection na ukabila, hili ni jambo baya sana ambalo kimsingi PSRS kwa miaka ya hivi karibuni ilifanya vyema sana katika kupambana nalo
 
Meiner Meinung nach sollte sich PSRS mit allen Regierungsämtern befassen, einschließlich halbstaatlicher Regierungsämter. Diese TRA-Beiträge sollten tatsächlich über PSRS beworben werden
Kwa maoni yangu, PSRS inapaswa kushughulikia ofisi zote za serikali, pamoja na mashirika ya umma. Nafasi hizi za TRA zinapaswa kukuzwa kupitia PSRS.
 
Una hoja Mkuu.. Ila kama nakumbuka Mhe. Namba 1 aliwapa Kibali kwa madai kuwa walilalamika kucheleweshwa kwa mchakato wa kuwapata watumishi wapya
Ni kweli wana hoja bora hivyo mkuu, embu angalia watu tumeomba kazi hapo utumishi mpaka sasa tuna miezi sita hakuna usaili wowote tulio itwa kufanya, kitu ambacho sio kawaida ya recruitment yoyote kufanyika ni wao tu.
 
Sekretarieti ya ajira mmekuwa msaada mkubwa sana kwa vijana wasio na connection kupata ajira.

Niukweli usio pingika Sekretariet ya Ajira mko fair sana katika kutafuta watumishi wa Umma, hakuna upendeleo wala vimemo, anaye ajiriwa kimsingi anakiwa amefanya vyema kwenywe Interview.

Kitendo cha kurudisha ajira hizo kwenye Taasisi husika kinarudisha nyuma jitihada za kuondosha ukabila katika Taasis mbalimbali Nchini.

Sekretarieti ya Ajira, tunaomba mrudishe ajira za TRA kwenu, ambao watoto wetu wameshaweka nyaraka mbali mbali katika mfumo wenu wa ajira za umma.
Kwa Sasa Kuna Baadhi ya mashirika na taasisi yamepewa uhuru wa kuajiri Ili kupungiza ukiritimba.

Sema hivi hizo Ajira zisimamiwe na Sekretarieti.

Mwisho mtoto wa maskini unataka kuomba Ajira TRA? 🤣🤣
 
Kitendo cha kurudisha ajira hizo kwenye Taasisi husika kinarudisha nyuma jitihada za kuondosha ukabila katika Taasis mbalimbali Nchini.
Kwa sasa hivi kazi kwenye taasisi za fedha zote ni za hawa wadau.
 
Kwa maoni yangu, PSRS inapaswa kushughulikia ofisi zote za serikali, pamoja na mashirika ya umma. Nafasi hizi za TRA zinapaswa kukuzwa kupitia PSRS.
Mkuu inaonekana hujapitia mateso ya utumishi kukaa miezi nane na kadhalika huko na hakuna usahili ulioitiwa baada ya kuomba kazi Utumishi wewe .
 
Natamani watanzania wenzangu mngejua nguvu iliyopo nyuma ya kuruhusu TRA waajiri wenyewe. Kama ulishindwa kupata kazi TRA enzi za Ajira portal kwa sasa possibility ya kuajiriwa ni 5%, kwa sasa ni watoto, ndugu na jamaa wa political class tu.
 
Jamaa yangu mmja aliniambia amefila oral mara 2 tena baada ya kuwachimba mkwara hao TRA kwamba ni mtu wa Chama lakini hakutoboa.

Anasema hizo Ajira zikitangazwa Wanasiasa na wengine wanarudisha Watoto wao hata kama wako Ulaya,USA nk wanakuja na ndinga Kali kwenye interview harafu wewe mtoto wa kapuku kutegemea kupata?

Hapo labda kazi 600 zitashindaniwa Kwa Haki ila hizo 1,000 zitakuwa connection kama uhamiaji,BoT,NSSF, Ngorongoro nk
 
Una hoja Mkuu.. Ila kama nakumbuka Mhe. Namba 1 aliwapa Kibali kwa madai kuwa walilalamika kucheleweshwa kwa mchakato wa kuwapata watumishi wapya
Hiyo hoja Haina msingi Kwa sababu Kwa nini wacheleweshe kupewa vibali?

Nimeisikia mara kadhaa lakini Haina mashiko Kwa sababu Kwa nini Idada ya Utumishi icheleweshe? Sio tuu Kwa TRA Bali Kwa mashirika mengine ambayo yanalemga faida za Kibiashara,Sasa Bora hao lakini TRA ni taasisi ya Umma sio ya Kibiashara
 
Back
Top Bottom