Retired siyo sahihi kusema wote wanaomuunga mkono Lissu wanatukana, hapo unakosea na inaonekana una hasira sana. Ni lini uliitisha mkutano wa wananchi wanaomuunga mkono Lissu ukatukanwa na mkutano mzima? Hata baadhi ya wanaomuunga mkono Mbowe wana matusi vile vile. Mbona walikua wakimtusi Lissu kuwa ni mlemavu? Wacha hasira ndugu. Kama ni maandamano Mbona hata wakati Mwenyekiti Mbowe alipoitisha hao kina Mrema hawakujitokeza adi uwanyooshee kidole wafuasi wa Lissu? Twendeni taratibu tu, hasira hazijengi.
Siasa zimebadilika, naona unadhani bado watu wanaendekeza hizo siasa za hujuma. Mbinu zilizotumika zamani kuua vyama vya upinzini vingi mnaamini hata sasa zitafanya kazi?