Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Siku zote CHADEMA na vyama vingine vya upinzani, vimekuwa vikilalamikia mambo ya hovyo ya kukata majina ya wagombea wa upinzani wanaoonekana kuwa tishio dhidi ya wagombea wa CCM kwenye chaguzi mbalimbali.
Hayo yamefanyika sana hata kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa wa mwaka jana, na CHADEMA ikalalamika sana. Lakini jambo la ajabu ni kuwa CHADEMA hao hao waliokuwa wakilalamikia uchafu huo, chini ya katibu mkuu John Mnyika imefanya uchafu huo huo dhidi ya wagombea wa nafasi za ujumbe wa kamati kuu waliotamka wazi kuwa wanamwunga mkondo Tundu Lisu kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa. Wahanga wa uchafu huo ni dada mpambanaji ROSE MAYEMVA na PAMBALU.
Ikumbukwe kwamba wajumbe wa sekretarieti hiyo ya John Mnyika ni wale wenyeviti wa kanda walioalikwa na Mbowe nyumbani kwake, na kuelekezwa kutoa tamko kuwa wanamtaka Mbowe agombee tena nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.
Kwa sasa, ni dhahiri, chini ya Mbowe, role model wa CHADEMA, ni CCM.
Mnyika anatakiwa aulizwe ana haki gani ya kuihoji CCM, Serikali ya CCM, Tume ya Uchaguzi au TAMISEMI kuhusiana na kukata majina ya wagombea kupitia vyama vya upinzani, wakati sekretarieti yake inafanya uchafu huo huo?