Sekta ya elimu kuna uonevu sana!

Sekta ya elimu kuna uonevu sana!

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Kuna mwalimu anaanza na ngazi ya certificate na baadae anaenda kujiendeleza kwa ngazi tofauti tofauti.

Miongoni mwa kozi anazosomea ni stashahada au shahada za utaalam tofauti, mfano ukaguzi, uongozi, IT nk.

Na wengi hujisomesha wao wenyewe kwa gharama zao.

Lakini katika mazingira ya kazi, kunakuwa na hali ya kuchukuliwa kama mwalimu wa kawaida; hata likitokea suala linalohusu taaluma, huchaguliwa mtu asiye na hiyo taaluma.

Je, umuhimu wa walimu kujiendeleza kitaaluma au kitaalam una faida gani? Naomba mnisaidie kwa maoni.
Inaumiza sana.

Walimu wanaonewa sana! Hakuna kupanda madaraja kwa wakati, hakuna allowances, posho za usimamizi ni kidogo.

Bado anaamua kujiendelzea lakini hakuna anayeonesha kuthamini elimu yao!
Inaumiza sana!
 
Hicho kidiploma cha ukaguzi ndo unata uwe mdhibiti ubora wa elimu?

Kasome digrii kwanza ndo ukaweke na hako kakiperush ka adem kama sifa ya ziada.

Vikaguz vilivosoma kwa kuunga unga huwa natibuana navyo sana, nikikujua tu umeunga lzm nikusumbue.
Kwa lugha hii, naomba kwa Mwenyezi Mungu isije ikawa wewe ni Mtakwimu!
 
Hicho kidiploma cha ukaguzi ndo unata uwe mdhibiti ubora wa elimu?

Kasome digrii kwanza ndo ukaweke na hako kakiperush ka adem kama sifa ya ziada.

Vikaguz vilivosoma kwa kuunga unga huwa natibuana navyo sana, nikikujua tu umeunga lzm nikusumbue.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 mkuu, muonee huruma jamaa
 
Pole madam, hiyo kawaida huku tamisemi, huku hawaangalii vyeti, wanaangalia connection.
Mi nna bachelor, Ila nimeamua kuingia shamba, Bora nilime ufuta kuliko kuwaza sijui vyeti vitanisaidia chochote kwenye muundo....wataniheshimu nikiwa na pesa!
Tafuta biashara Fanya, kajiendeleze kielimu, Kama unataka cheo kuwa pia chawa....na Kwa mwanamke ukubali kuliwa.
 
Hicho kidiploma cha ukaguzi ndo unata uwe mdhibiti ubora wa elimu?

Kasome digrii kwanza ndo ukaweke na hako kakiperush ka adem kama sifa ya ziada.

Vikaguz vilivosoma kwa kuunga unga huwa natibuana navyo sana, nikikujua tu umeunga lzm nikusumbue.
Acha uhuni wew
 
Hapo shida Ni cheti chako Cha form four Unakuta una division four ya D3 then unalalamika !:re-sit kwanza Mkuu upate cheti kizuri
 
Kwani lazima uwe kiongozi mkuu?
Huwa nawashangaa sana watu ambao ni watumwa wa tuvyeo,jiongeze tu kwa kuwa na plan b Ili kuongeza kipato.
Elimu siku hizi si lolote wala chochote vinginevyo kama una amini ktk elimu walau jiendeleze upate elimu ya masters.
 
Hicho kidiploma cha ukaguzi ndo unata uwe mdhibiti ubora wa elimu?

Kasome digrii kwanza ndo ukaweke na hako kakiperush ka adem kama sifa ya ziada.

Vikaguz vilivosoma kwa kuunga unga huwa natibuana navyo sana, nikikujua tu umeunga lzm nikusumbue.
Inategemea na uwezo wako wa kufikiri ni wa kiwango gani!

Kuna sekta nyingine hata kuwa na certificate tu, ni sifa ya ziada ukiongezea na taaluma yako ya awali.
Tuache kudharau taaluma za ualimu! Kusoma sio kazi rahisi.
 
Siku waalimu mkijitambua mkaacha kutumiwa na kujidhalilisha mtaijua thamani yenu, until then endeleeni kudhalilika tu.
 
Back
Top Bottom