SoC04 Sekta ya Elimu

SoC04 Sekta ya Elimu

Tanzania Tuitakayo competition threads

BARAKAS SANGA

New Member
Joined
May 13, 2024
Posts
3
Reaction score
2
Ili kuboresha sekta ya Elimu Tanzania na kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji mashuleni hususani katika kipindi hiki cha mabadiliko ya sayansi na teknolojia na matumizi ya vifaa vya TEHAMA ni vyema Serikali kuhakikisha inaboresha mazingira ya kimtandao mashuleni

Uwepo wa huduma ya Wi-fi katika taasisi za Elimu Awali na msingi Ili kuwawezesha walimu na kuwarahisishia suala zima la ufundishaji na ujifunzaji mashuleni hii itasaidia Wanafunzi kujifunza kwa vitendo zaidi na kupata uelewa wa vifaa vya TEHAMA kuanzia ngazi ya chini ya Elimu.

Lakini pia uwepo wa semina kwa walimu za mara kwa mara na hii ni kwa walimu wote na sio kwa baadhi tu,kwani mwalimu anaweza asijifunze kitu kipya tangu aajiriwe ni kutokana na ufinyu wa semina zinazotolewa na kulenga baadhi yao tu na wengine kujikuta katika fungu la kukosa miaka yote yupo kituoni katika mazingira hayo hayo.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom