Sekta ya Habari Tanzania Vs Usalama wa Taifa

Sekta ya Habari Tanzania Vs Usalama wa Taifa

sopinta

Member
Joined
May 28, 2020
Posts
46
Reaction score
93
Kiukweli kabisa kama sekta ya Habari nchini ingetumika kiufasaa kama mataifa mengine yaliyoendelea katika sekta ya habari ingelisaidia taifa katika maswala mazima ya Usalama wa Taifa, mwandishi wa habari aliyekwiva ni zaidi ya Usalama wa Taifa, tuachane na hawa waandishi wa kupokea bahasha kuna waandishi wasioonekana wanaitwa Invisible Journalist , nchi kama USA, UK , Kanada , Urusi , Afrika Kusini , Rwanda , Nigeria wanawatumia sana ktk kuimarisha taarifa za kiuchunguzi , Tanzania sijui tunakosea wapi ? katika historia kubwa sana ya uvumbuzi taarifa pamoja na matukio makubwa yanafanywa na hawa Invisible Journalist na taarifa zao zinapokamailika zinatolewa ktk uwazi kwa lengo la kutoa changamoto kwa vyombo vya ulinzi na Usalama , CNN , Washton Post , The New York Time wanatumia sana IJ, Jamal Ahmad Khashoggi ni mfano mmoja wa Invisible Journalist na ametoa mchango mkubwa sana kwa Taifa la USA kabla ya kuingia katika mikono ya waasi , ni zaidi Intelligencia , kuna huyu mwingine Mganda anaitwa Shaka Ssali wa VOA .

K
wa mfano kwa Tanzania Usalama wa Taifa anatambulikaje ukiacha hawa wanaoonekana ......Uofisa Usalama wa Taifa (ushushushu) ni kitu gani? Kwa tafsiri rahisi, ushushushu ni taaluma inayohusu ukusanyaji, uchambuzi na uwasilishaji (kwa mamlaka husika) wa taarifa za kiusalama kwa njia za siri (clandestine methods).

Maeneo makuu ya kazi za Idara ya Usalama wa Taifa ni kukusanya na kuchambua habari za kiusalama zinazohusiana na ujasusi (espionage), uzandiki (subversion), uhujumu (sabotage) na ugaidi (terrorism).
 

Attachments

  • download.jpg
    download.jpg
    4 KB · Views: 8
  • 924488_360W.png
    924488_360W.png
    38.4 KB · Views: 8
Kiukweli kabisa kama sekta ya Habari nchini ingetumika kiufasaa kama mataifa mengine yaliyoendelea katika sekta ya habari ingelisaidia taifa katika maswala mazima ya Usalama wa Taifa, mwandishi wa habari aliyekwiva ni zaidi ya Usalama wa Taifa, tuachane na hawa waandishi wa kupokea bahasha kuna
P
Mkuu Sopinta, kwanza naunga mkono hoja, its true, waandishi wa habari wenye uwezo wa kufanya IJ, wanaweza kulisaidia sana taifa kama alivyosema kwenye bandiko hili.

Kwavile mimi ni mwandishi mwenye uwezo wa kufanya IJ, lakini pia ni mtetezi wa waandishi wa habari wapewe bahasha nene,
Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa - Pasco wa JF!
Hivyo sijapenda jinsi ulivyowabagua waandishi wa habari wa bahasha!.

Kwenye kundi la waandishi, pia tumegawanyika katika makundi makuu matatu
Waandishi wa habari wa wito ambao hawa ni wazalendo. Hawa ndimo waandishi wa habari wa IJ, wanapatikana.
Waandishi wa habari wa ajira, ambao hawa wameingia uandishi ili wapate kipato, kwai uandishi ni ajira, hawawezi kufanya IJ.

Kwenye hili kundi la waandishi wa wito, mimi nimo, media tumeisha jitolea sana kuisaidia serikali, na kiukweli tunaisaidia sana serikali, kwa kuripoti kwenye media mambo mbalimbali yanayoisaidia serikali.
Hii ni baadhi ya mifano.

Security alert kwa Serikali yetu, tuwe makini sana na Marekani: Kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga Kutu-Libya?

US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali?

Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija

WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?

Misaada yote hii tumeitoa humu jf, kwavile humu jf, wale 'jamaa' wamo na wametamalaki humu, then naamini lazima taarifa kama hizi, wanazifanyia kazi kwa kuzitumia as info tip.

Ungetaka tufanye nini zaidi?, tupige hodi pale Eagle House tumkabidhi Chief?.
P
 
Kwa tanzania hatuna hata Mwandishi mmoja wa aina hii?
Kikete hawezi kuwepo?
 
Kwa tanzania hatuna hata Mwandishi mmoja wa aina hii?
Kikete hawezi kuwepo?
Kikete ndio nani? Na kwa nini unajumuisha kuwa hakuna mwandishi hata mmoja wa aina hiyo?! Kwa jambo usilolijua kunyamaza kimya ni hekima.
 
Sijaona waandishi wakiandika kuhusu wizi wa billion 8.9 za chadema
 
Waandishi wa aina hiyo tunao, tatizo je, wanapewa uhuru wa kufanya kazi zao? mwandishi anapojihisi kuwa huru kufanya kazi yake ndipo anaweza kufanya kazi yake kwa ufasaha zaidi, hapo ndipo anapokuwa na ari ya kufanya habari za kiuchunguzi.

Bahati mbaya waandishi wetu wanalazimishwa kufanya kazi ya aina moja tu; kuwasifia watawala, hii inasababisha kwa kiasi kikubwa kuporomosha uwezo wao wa kiutendaji kwa kukosa ari ya kufanya kazi, hivyo wengi kujikuta wakiangukia kwenye kundi la bahasha za kaki bora maisha yaende.
 
Tunao waandishi makini sana japo sio wote. Tatizo tunavyo vyombo vya habari vyenye wamiliki wa vyombo hivyo wanaosukumwa na agenda zilizo kinyume na maadili ya uandishi. Mwandishi hata kama atakuwa na uwezo mkubwa kiasi gani, matakwa ya mmliki ndiyo utakuwa mwongozo wa kazi zake. Tatizo jingine wamiliki walio wengi wa vyombo vya habari ni wababaishaji wakubwa. Dhuruma ndio mtaji wao. Waandishi wanalipwa mishahara midogo mno na sio kwa wakati. Pia kuna baadhi hawalipwi kabisa na hivyo kuishi kwa kutegemea bahasha. Unataraji nini kwa mwandishi anayetwezwa na mazingira ya kazi kwa kiwango hicho.? Hata uwe na uwezo na ufanisi mkubwa kiasi gani'njaa itakutoa kwenye mstari. Sekta ya habari inahitaji maboresho makubwa ndipo tunaweza kunufaika na uwepo wa waandishi kwa kiwango tunachotarajia.
 
Back
Top Bottom