Sekta ya kahawa Tanzania yaimarisha utayari wa kuzingatia kanuni ya EUDR

Sekta ya kahawa Tanzania yaimarisha utayari wa kuzingatia kanuni ya EUDR

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), kwa kushirikiana na Taasisi ya Misitu ya Ulaya (EFI) na kampuni ya sheria ya NexLaw Advocates mapema aeptemba 15 mwaka huu iliandaa warsha ya pili ya wadau.

Warsha hiyo ilikuwa sehemu ya jitihada zinazoendelea za kuimarisha utayari wa sekta ya kahawa nchini Tanzania katika kukidhi matakwa ya Kanuni ya Umoja wa Ulaya dhidi ya ukataji miti (EUDR).

Warsha hiyo ilijikita katika kujadili matakwa ya kisheria yanayosimamia uzalishaji na biashara ya kahawa nchini Tanzania, hali halisi ya utekelezaji wa matakwa hayo, pamoja na hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kuhakikisha utiifu na kushughulikia maeneo ambayo yanaweza kusababisha kutokidhi vigezo vilivyowekwa.

Warsha hiyo ilijenga juu ya kikao cha kwanza cha wadau kilichofanyika mwezi Juni 2026, ambapo matakwa husika ya kisheria ya kitaifa yalipitiwa na kuidhinishwa.

Washiriki kutoka taasisi za serikali na sekta ya kahawa walishiriki uzoefu wao na kutoa maoni kuhusu hali ya utekelezaji wa matakwa hayo ya kisheria pamoja na uhalisia wa utekelezaji wa hatua zilizopendekezwa za kuhakikisha utiifu (due diligence).

Matokeo ya warsha hiyo yatachangia katika kuandaa Mfumo wa Utiifu wa Kisheria kwa Sekta ya Kahawa Tanzania, wenye lengo la kuwasaidia wadau kukidhi matakwa ya EUDR kuhusu uhalali wa bidhaa na uwezo wa kufuatilia asili yake (traceability)
 

Attachments

  • FB_IMG_1790002546822.jpg
    FB_IMG_1790002546822.jpg
    22.1 KB · Views: 9
  • FB_IMG_1790002567182.jpg
    FB_IMG_1790002567182.jpg
    28.2 KB · Views: 4
  • FB_IMG_1790002575455.jpg
    FB_IMG_1790002575455.jpg
    36.9 KB · Views: 7
  • FB_IMG_1790002589653.jpg
    FB_IMG_1790002589653.jpg
    51 KB · Views: 7
  • FB_IMG_1790002552541.jpg
    FB_IMG_1790002552541.jpg
    30.1 KB · Views: 10
  • FB_IMG_1790002664990.jpg
    FB_IMG_1790002664990.jpg
    67.2 KB · Views: 8
  • FB_IMG_1790002652417.jpg
    FB_IMG_1790002652417.jpg
    60.4 KB · Views: 8
  • FB_IMG_1790002641814.jpg
    FB_IMG_1790002641814.jpg
    75.7 KB · Views: 11
  • FB_IMG_1790002621588.jpg
    FB_IMG_1790002621588.jpg
    71.6 KB · Views: 8
  • FB_IMG_1790002608286.jpg
    FB_IMG_1790002608286.jpg
    54.8 KB · Views: 12
  • FB_IMG_1790002597072.jpg
    FB_IMG_1790002597072.jpg
    56.1 KB · Views: 8
  • FB_IMG_1790002631613.jpg
    FB_IMG_1790002631613.jpg
    57.1 KB · Views: 8
  • FB_IMG_1790002688296.jpg
    FB_IMG_1790002688296.jpg
    107.4 KB · Views: 10
Back
Top Bottom