kilimochetu_Tz
New Member
- Jul 28, 2022
- 3
- 3
Kilimo ni Uti wa mgongo katika nchi yetu ya Tanzania. Kilimo ndio chanzo cha chakula na ajira katika kaya nyingi zinazoishi katika nchi ya Tanzannia. Ili nchi yoyote iweze kuendelea basi sekta ya kilimo ni muhimu katika kuleta maendeleo ya Taifa hilo kama ilivyo Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo ili iweze kuendelea basi lazima sekta ya kilimo ifanye vizuri.
Katika Tanzania kilimo ni sekta muhimu kwa maendeleo ya nchi na watu wake kwa ujumla sababu inayofanya sekta ya kilimo kuwa muhimu zaidi hapa Tanzania ni pamoja na uwezo wa sekta hii kuajiri takribani ya watu zaidi ya 80% ya watu wote ndani ya Tanzania.
Umuhimu wa sekta ya kilimo katika maendeleo ya nchi unazidi kuongezeka ni pamoja na matumizi ya Teknolojia za kisasa kama vile matumizi ya mbegu bora na mashine za kulimia mashamba, kupandia na hata kuvunia na kuhifadhia mazao kwa ajili ya matumizi ya baadaye.
Shughuli za kilimo katika nchi ya Tanzania zinafanywa zaidi na wakulima wadogo ambao ni sawa na 90% ya shughuli za uzalishaji wa mazao inategemea wakulima wadogo wadogo.
Kwa hiyo ili sekta ya kilimo iweze kuendelea ni lazima mkulima mdogo aandaliwe vyema kupokea mabadiliko chanya ambayo yatakwenda kubadilisha mtazamo wake katika kilimo na hivyo kufanya kilimo cha kisasa zaidi kwa maendeleo ya kaya yake na taifa kwa ujumla.
Kwahiyo mkulima mdogo anahitaji mambo muhimu katika kufanya kilimo chenye tija zaidi kama vile zana za kisasa, mbegu bora, mikopo, masoko ya uhakika, ushauri wa kitaalum na taarifa za hali ya hewa,na hata wakati mwingine elimu ya ujasiriamali.
makala hii itaedelea...

Upvote
4