SoC04 Sekta ya Ujenzi na Ukuzi wa Uchumi wa Tanzania katika maendeleo endelevu

SoC04 Sekta ya Ujenzi na Ukuzi wa Uchumi wa Tanzania katika maendeleo endelevu

Tanzania Tuitakayo competition threads

lerienyaiya

Member
Joined
Aug 26, 2017
Posts
9
Reaction score
8
Tanzania na nchi za afrika kwa ujumla wake tumekuwa na uduni katika kukuza SEKTA ya UJENZI kwa MAENDELEO ENDELEVU pamoja na usalama wa nnchi zetu

1. SEKTA YA UJENZI ni nyenzo muhimu katika maendeleo ya taifa lolote Tanzania ikiwemo. Kati ya sekta inayotumia pesa nyingi katika mataifa yanayoendelea ni SEKTA ya ujenzi, hii ni kwa sababu nchi inakuwa katika Hali ya kujenga miradi mbalimbali ili kufikisha maendeleo na huduma kwa wananchi wake.

2. Sekta ya ujenzi ni suala la usalama kwa taifa lolote lile kuepuka kuvamiwa au kuhujumiwa na taifa kingine lile.

Ila kinachosikitisha hili kwa nnchi yetu halitazamwi hivyo bali linaonekana fursa ya kujipatia pesa maana ni sehemu ambayo hupitisha pesa nyingi na pia hutumika kusafisha pesa chafu.

Nini nashauri kifanyike ili tuweze kufaidi matunda ya sekta hii.
1. Kuanzisha bank ya kudhamini makandarasi. CRB wamejaribu kulitafutia ufumbuzi hili ila kiwango Chao bado ni kidogo sana. Nitolee mfano wachina wao Wana bank kabisa inayolinda makandarasi wao inayojulikana kama Construction Bank of China (CBC) mchina anaposhinda kazi popote Hana pressure ana uhakika wa kuwa financed maana hii miradi asilimia kubwa inaendeshwa na bank guarantee ndo maana leo wako na miradi mikubwa hapa.

2. Ulinzi wa nnchi.
Hatuombei lakini kuwapa makandarasi wa nje kujenga miradi yetu ya kimkakati ni kujiweka njia panda katika swala Zima la kiusalama.

Mimi sio mwandishi mzuri ila labda kama nitashinda naweza kutafuta njia ya kulielezea kwa mapana yake
 
Upvote 1
Back
Top Bottom