Sekta ya utalii inakua shilingi inapoteza thamani, hizi drama zitakuja kuisha lini?

Sekta ya utalii inakua shilingi inapoteza thamani, hizi drama zitakuja kuisha lini?

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa) imesaini mikataba minne ya uwekezaji wa utalii kupitia utaratibu wa Uwekezaji Mahiri (Swica) na kampuni ya Kitanzania ya Uhusiano International ICT Limited.

Mikataba hiyo inatarajiwa kuingiza mapato ya Dola za Marekani milioni 281.5 (sawa na Sh719 bilioni za Kitanzania) kwa kipindi cha miaka 20 ikiwa ni wastani wa Sh36 bilioni kwa mwaka, imesainiwa leo Jumatano Agosti 13, 2025.

Soma pia: Serikali ya Samia yapunguza viwango vya tozo za sekta ya Utalii Kwa asilimia 80%.inalenga kuvuti zaidi Watalii

Screenshot 2025-08-13 022054.png

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk Pindi Chana amesema uwekezaji huo utaimarisha sekta ya uwindaji wa kitalii na utalii wa picha, sambamba na kuleta ajira, kuboresha huduma za jamii na kuchochea maendeleo ya wananchi.

Balozi Dk Chana pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake madhubuti katika kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia filamu za Amazing Tanzania na The Royal Tour, zilizochochea ongezeko la watalii na wawekezaji.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tawa, Meja Jenerali mstaafu, Hamis Semfuko amesema Tawa imepiga hatua kwa kusaini mikataba minne mipya ya Swica na kufikisha jumla ya mikataba 13 kati ya 14 iliyopangwa sawa na asilimia 92.3 ya lengo, hatua iliyowezesha kukusanya zaidi ya Sh27.4 bilioni kati ya Januari 2024 na Agosti 2025.
 
Back
Top Bottom