Sekta ya Utalii Tanzania ijiandae kwa maisha ya Corona na baada ya Corona

Sekta ya Utalii Tanzania ijiandae kwa maisha ya Corona na baada ya Corona

Cvez

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2018
Posts
4,405
Reaction score
13,411
Janga la Corona mpaka sasa hivi limeathiri nyanja mbalimbali za uchumi. Ingawa mpaka muda huu sekta ambayo imeathiriwa zaidi na ipo ICU ni sekta ya Utalii. Nchi nyingi zimefanya lockdown, kuna kufutwa kwa safari za anga. Hivyo hoteli, migahawa, tax drivers, wakulima, wavuvi, tour companies na wale wote ambao kipato kilikua kinategemea utalii sasa hivi Mungu anawasaidia tu kwa maana hali utakua mbaya zaidi.

Kwa kampuni za utalii na hoteli sasa hivi wanakumbwa na issue ya cancellation. Na kwa issue unexpected kama hii anatakiwa afanye refund kwa wateja pia alipe mishahara kwa wafanyakazi. Kwa hoteli na kampuni kubwa za kimataifa wanaweza kujitahidi kufanya hivyo. Issue ni hizi kampuni zetu za kitanzania ambazo kulipa mishahara ya wafanyakazi kwa wakati ni mtihani, pia usimamizi mbovu wa fedha kwao ni issue. Ndio hapo utakuta director anataka akimbie mji, ana madeni ya wafanyakazi, anatakiwa afanye refund na pesa alishazitumia.

Pia nimeona kuna kampeni wamekuja nayo na slogan: "DO NOT CANCEL YOUR TRIP, POSTPONE". Yeyote aliyekuja na slogan hii Mungu amsaidie maana hajui alisemalo. Utalii sio hitaji muhimu la binadamu, kuna mahitaji mengine yatimizwe ndipo kiasi kinachobakia utalii ufanyike. Mbaya zaidi baada ya corona tutarajie global economic crisis, ambao utaambatana na mfumuko wa bei wa bidhaa muhimu. Hivyo kaa ukijua yule mgeni ni lazima afanye cancellation apate hela yake maisha yaendelee.

Jambo lingine tusitarajie kua utalii utarudi katika hali ya kawaida by June au August, hii issue mpaka ikae sawa at best ni baada ya miaka miwili. Kwa muda huo thamani ya dola na bidhaa sijui itakua kiasi gani, hivyo kama unaweza kubali cancellation sasa au uje kuifanya hiyo kazi kwa hasara.

MUHIMU: kwa kampuni za utalii sasa hivi ni muda sahihi wa kufanya marketing sio sales. Fanya digital marketing tengeneza contents nzuri kujenga brand ya kampuni yako. Katika hilo fanya promotion ya vivutio aidha iwe Serengeti, Udzungwa, Zanzibar, Mafia, Magoroto au popote pale. Cheza na human psychology show usionyeshe kua unataka pesa take sasa fanya kama unamjulisha vilivyopo Tanzania. Tengeneza brand yako muda huu, ikifika muda wa kufanya sales ushajijenga vyema. Swali, je unawatu wanaoweza kutengeneza contents nzuri? Kama huna tafuta au jifunze.

Mla Bata

Na wale waliokua wanataka kuanzisha kampuni za utalii muda ndio huu magari ya tour yatauzwa bei rahisi sana na wote mpo katika ground level huna haja ya kwenda trade fairs.
 
Mkuu, kiukweli industry imepata simanzi kubwa sanaa, kila mtu analia upande wake hakuna 'big boys" wala nani wote tupo ground level, tena kampuni kubwa ndio zimepata pigo kubwa hasa kwenye operation costs kulipa mishahara n.k, nawaza hali itakuwaje kama hakutokua na high season mwaka kuu, kuna watu hii itawaumiza zaidi.
 
Niwa kweli kwa upande mwingine ni faida kwa kampuni zinazoanza hasa ambazo hazina loads kubwa ya wafanyakazi hapa ndio muda wakuweka mambo sawa, kukimbizana na marketing na kujijenga katika kuandaa packages na connection za maana mpaka hali inarudi kawaida basi wote mnajikuta mnaanza upyaaa 😁😁.
 
Mkuu, kiukweli industry imepata simanzi kubwa sanaa, kila mtu analia upande wake hakuna 'big boys" wala nani wote tupo ground level, tena kampuni kubwa ndio zimepata pigo kubwa hasa kwenye operation costs kulipa mishahara n.k, nawaza hali itakuwaje kama hakutokua na high season mwaka kuu, kuna watu hii itawaumiza zaidi.
Mwaka huu hakuna high season hilo tusahau kabisa, tukipata watalii 500,000 tu ni jambo la kushukuru.
 
Mwaka huu hakuna high season hilo tusahau kabisa, tukipata watalii 500,000 tu ni jambo la kushukuru.
😤 Mungu aweke wepesi tu, naona kabisa kuna watu wanaenda kuanguka kipindi hiki.

Wale ndugu zangu wa "twanga maji, mlima bado upo" Porters wanaenda kupagawa.

Hotels tutaanza kuishi wenyewe.
 
😤 Mungu aweke wepesi tu, naona kabisa kuna watu wanaenda kuanguka kipindi hiki.

Wale ndugu zangu wa "twanga maji, mlima bado upo" Porters wanaenda kupagawa.

Hotels tutaanza kuishi wenyewe.
Hahaha sio mazuri imagine katika historia ya Tanzania ni kwa mara ya kwanza Serengeti na Ngorongoro hakuna mgeni hata mmoja. Wale Campsites na hotels porini watakuta ngedere wameweka kambi.

Kibaya zaidi Corona inaua wale big spendors wazee, hao pia ndio wananunua vito vya thamani aidha kwa kununua TZ au huko kwao..sekta ya madini nao itapigwa sana mpaka crisis ipite luxury goods nyingi zimeumia.
 
Dunia ipo kwenye lockdown, ngoja tusubiri hiyo mwisho wa mwezi marekani na ulaya watakapofungua shughuli za kiuchumi
 
Hiyo point nilikuwa sijaifikiria kabisa but yes! Wazee ni spenders wakubwa sanaa mzee na ndio wanaongoza kusafiri. Hapa mpaka industry irudi kwenye peak basi hotels huko porini utakutana na wanyama wa kila aina vyumbani😂😂
 
Dunia ipo kwenye lockdown, ngoja tusubiri hiyo mwisho wa mwezi marekani na ulaya watakapofungua shughuli za kiuchumi
Amen zifunguke mapema...
 
Hapa namuwaza mwajiri wa Tanganyika wilderness camps na kibo guides Arusha alie wekeza kwenye utalia tu... Msimu mgumu sana huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa msimu huu itabidi agharamie tu staff wachache wabaki huko kwenye Camps la sivyo atakuta matobo na wanyama washajimilikisha..... Biashara ndivyo ilivyo
 
Kwa hakika huo ndio ukweli kwamba tourism industry Tanzania imejifunga yenyewe kwakuwa wateja wa utalii ni watu wenye kujijali.

Wale Wachina waliokuja baada ya corona kuanza kuchanganya kwao si wadau wa utalii bali walikuja kwa malengo yao tu na utalii ni kama njia ya kuja Bongo.
Viongozi wetu wetu hawajafunga hii industry
 
Ni kweli Ila sio Jambo la kushabikia, kwa maana inatuathiri watanzania wote kiujumla,
Thanks
 
Utalii utaendea tu high season bado kuanza

Kuna Wazungu wa Nchi za scanavia na canada wenyewe wapo adcted na Tanzania yaani piga ua kwa mwaka lazima waje mara moja
 
Utalii utaendea tu high season bado kuanza

Kuna Wazungu wa Nchi za scanavia na canada wenyewe wapo adcted na Tanzania yaani piga ua kwa mwaka lazima waje mara moja
Watakuja kwa Ungo?.
 
Back
Top Bottom