Selelii awazima Lowassa na Rostam


- Maneno mazito sana haya mkuu.

Respect.

FMEs!
 
mafisadi lazima watafute mtoko mwingine hawawezi kukubali kushindwa hata siku moja
 
..Waswahili wana msemo wao "majuto ni mjukuu."

..wakati tunamchagua JK, hatukufikiria kabisa atamlipa vipi fadhila za Rostam Aziz.

Naam hatukujua kama Kikwete anastahili kumlipa fadhila yeyote yule kwa sababu wakati ule hatukujua kama lile kundi lililojiita la "mtandao" lilihusika na kukusanya mabilioni ya Kampeni za Kikwete kutoka kwa mafisadi mbali mbali wakiwemo akina Jeetu, Manji, Subhash Patel, Rostam na wengineo ili kuhakikisha anakuwa mgombea wa CCM. Ndiyo maana sasa tunataka yaliyojiri yote katika sakata la Richmond yaanikwe hadharani ili Watanzania tusifanye makosa ya kumchagua tena Kikwete kama Rais 2010.

Kumbuka kutenda kosa si kosa lakini kurudia kosa ni kosa. Kama ushahidi wote wa nini kilichojiri katika sakata la Richmond/Dowans ukianikwa hadharani sidhani hata huko CCM kama watataka Kikwete awe mgombea wao 2010.
 
Bubu Ataka Kusema,Mkandara,FMES,

..I believe we will not get to the bottom of this scandal bcuz Mwakyembe & Co, do not have the full support of the President.

..sasa pamoja na ukweli huo, I dont see "wapiganaji" wakija na plan B.

..vilevile zile kauli za "WAPIGANAJI" kwamba JK ndiyo amiri jeshi wa vita za ufisadi, naamini ni USANII tu. ingekuwa ni hivyo Rostam asingekuwa na jeuri ya kujihusisha na Dowans waziwazi kiasi kile.

..binafsi niko frustrated na serikali, Bunge, pamoja na "wapiganaji."
 

I believe we will not get to the bottom of this scandal bcuz Mwakyembe & Co, do not have the full support of the President.
Huu ndio ukweli wenyewe na ni katika frustration zetu tunatafuta mchawi wakati ni wazi kabisa kwamba serikali ya JK imeshindwa kusimamisha sheria. Na ajabu ni kwmba hakuna mtu hata mmoja anayemnyooshea kidole Mr. Presidaa isipokuwa vijembe vya nje.

Watu wengi walipenda sana kina Mwakyembe wafanya kama alivyofanya Sophia Simba. Kusema nje ya sheria wakati yeye anayomadaraka yote ya kuwachukulia hatua Mama kilango na Malecela..Kwa hiyo tumezoea sana Umbeya kusemana na kuwekana vidole vya uso na matusi mengi lakini tunashindwa kuufuata ukweli.
 
Bubu Ataka Kusema said:
Kumbuka kutenda kosa si kosa lakini kurudia kosa ni kosa. Kama ushahidi wote wa nini kilichojiri katika sakata la Richmond/Dowans ukianikwa hadharani sidhani hata huko CCM kama watataka Kikwete awe mgombea wao 2010.



BAK,

..sisi watu wa kawaida tunaweza kusema hatukujua hilo.

..lakini wapo watu ndani ya CCM walilijua hali lakini wakakaa kimya.

..CCM na "wapiganaji" wote wameshasema JK atasimama 2010 labda akatae mwenyewe. sasa ktk mazingira kama hayo huoni kwamba hawa "wapiganaji" wana chembe-chembe za usanii na ufisadi?
 
kama tume inaweza kubaini kuna tatizo halafu serkali haichukui hatua, sioni sababu ya kuendelea kuundwa tume kila kukicha. hizo pesa zinazolipwa kwa waheshimiwa wa tume nafuu wakanunue madawati ya wanafunzi wanokalia ndoo au wanaosoma wakiwa wamekaa chini.huu ni ubabaishaji katika serkali hii ya watanganyika.
 

- Hivi mkuu wewe kama mwanachi wa Tanzania ni lini utabeba responsibility yako na hizi ishu kwani Tanzania ni ya wapiganaji 11 tu? si yetu wote au wewe sio raia mwenzetu nini?

- I mean wapiganaji, wapiganaji kwani taifa lao wao tu?


Es!
 
Bubu Ataka Kusema,Mkandara,FMES,

..I believe we will not get to the bottom of this scandal bcuz Mwakyembe & Co, do not have the full support of the President.

Mimi sikubaliani nawe kwa sababu naamini kabisa kama Rais haoni umuhimu wa kuwachukulia hatua wahusika walioidanganya Serikali na kuingia mkataba ambao uliwalipa wakosaji hao $172 millioni bila kufanya kazi yoyote na pia wahusika hao kudharau ushauri wa wataalamu wa TANESCO ambao waliishauri Serikali kutoingia mkataba na Richmond kutokana na kutokuwepo rekodi zozote zile kuhusu kampuni hiyo na ufuaji umeme basi Rais huyu haitakii mema nchi yetu na Watanzania kwa ujumla bali anawatakia mema mafisadi ambao walimweka madarakani. Basi kiongozi huyu hatufai tena.

Tunakaribia kusherehekea miaka 49 ya uhuru wetu huko nyuma hatukuwahi kuona au kusikia Viongozi wa dini zetu kubwa mbili wakitamka hadharani kwamba nchi inaenda mrama lakini mwaka huu kwa mara ya kwanza wamefanya hivyo ili kuinusuri nchi yetu. Kama Rais anashindwa kuyatumia madaraka makubwa aliyokabidhiwa na Watanzania kuwashughulikia wavunja sheria wote basi kazi imemshinda na itakuwa bora abwage manyanga badala ya kung'ang'ania kuendelea kuwa madarakani.
 

- Mkulu Bob, saafi sana hii tumezoea umbeya na filimbi, hatuna utamaduni wa kujali sheria, kuanzia viongozi mpaka wananchi halafu tunalaumu wapiganaji tu, wapiganaji tu inachekesha kweli!

Respect.


FMEs!
 
Bubu Ataka Kusema,

..actually unakubaliana ni mimi!!

..lakini "wapiganaji" hawakubaliani na wewe.

.."wapiganaji" wameeleza bayana kwamba wanaunga mkono JK kugombea 2010.
 
- Hivi mkuu wewe kama mwanachi wa Tanzania ni lini utabeba responsibility yako na hizi ishu kwani Tanzania ni ya wapiganaji 11 tu? si yetu wote au wewe sio raia mwenzetu nini?

- I mean wapiganaji, wapiganaji kwani taifa lao wao tu?

Es!

Ahsante sana Mkuu! Yaani watu wamejiweka pembeni kabisa kama ufisadi wa kutisha ndani ya nchi yetu hauwahusu kabisa! Wapiganaji ni hao 11 tu wengine wote ni waangaliaji tu! Wamenawa kabisa mikono yao kama vile hawahusiki! Kweli baadhi ya Watanzania/Waafrika ndivyo walivyo!
 
Bubu Ataka Kusema,

..actually unakubaliana ni mimi!!

..lakini "wapiganaji" hawakubaliani na wewe.

.."wapiganaji" wameeleza bayana kwamba wanaunga mkono JK kugombea 2010.

- Sasa mamuzi binafsi ya wapiganaji kama wananchi yan uhusiano upi na Richimonduli? Kwa ni wewe mkuu si na wewe una maamuzi yako binafsi nani anasema kwamba maamuzi yako ni better kuliko ya mwingine?

- I mean sasa tufuatilie hata wapiganaji wamekula nini kama hizi ndizo standards mpya, yaani sasa hata maamuzi binafsi ya wapiganaji nayo ni ishu kwa taifa?

- Kwani aliyempa urais Kikwete in the first place ni nani sio sisi wananchi?

es!
 
Bubu Ataka Kusema,

..actually unakubaliana ni mimi!!

..lakini "wapiganaji" hawakubaliani na wewe.

.."wapiganaji" wameeleza bayana kwamba wanaunga mkono JK kugombea 2010.

Bado tuna muda mrefu sana kati ya sasa na October, 2010. Sauti za kumpinga Kikwete kutokana na sababu mbali mbali za kushindwa kuiongoza nchi yetu ikiwemo kushindwa kutimiza ahadi zake, kushindwa kupambana na ufisadi n.k. zikizidi kuongezeka ndani ya nchi yetu na hata ndani ya CCM, basi anaweza kabisa kuwekwa pembeni na kutafutwa mgombea mwingine toka CCM.
 
kama JK mwenyewe anawaogopa sisi tutafanya nini ni kupotezeana muda tu

Tanzania ni ya watanzania na wala siyo ya Kikwete, hivyo basi kama Kikwete ni mwoga watanzania tunajukumu la kuchukua dhamana tuliyomkabidhi na kuikabidhi kwa mtu aliyena uwezo.lakini swala la kukata tamaa hilo ni la mtu anayeelekea kushindwa.
Kwa hiyo wale wanaoelekea ukingoni kwa sababu mbalimbali wasiwakatishe tamaa wengine.
 

Mkuu Keil you have made my day..........thanks a lot

Ndugu yangu Mtanzania..........tumia approach nyingine.........hii ya Richmond..........ni MOTO........that would be my advise to you....

Kama Lowassa angekuwa "mwanaume wa Shoka"....."mwanaume namba moja"...........kama inavyodaiwa...........na kwamba Kamati ilimuonea.......haikumpa nafasi..............na kwamba "alidhalilishwa sana".........angeonyesha ni jinsi gani alivyodhalilishwa........kwa kupangua hoja za kamati ile moja baada ya nyingine...........halafu ndio angejiuzulu...........hapo atleast ningemkubali............lakini yeye akakimbilia kujiuzulu...............

leo na nyie mnaongezea eti hawakutoa maelezo yote (huku hamju yaliyomo kwenye ripoti ile).........na kwamba eti Ripoti ina mapungufu............kwa taarifa yako wakuu wanahaha ni jinsi gani ya kufunika funika yale yaliyoanikwa kwenye ile Ripoti ya kamati.......na ndio maana unaona inchukua muda kuchukua hatua...........Ripoti ile ni MOTO
 

acheni siasa hapa ripoti ipi iliyo MOTO..basi utakuwa ni moto ambao haaunguzi .ni muda gani tokea ripoti isomwe na hakuna la maana linalofanyika..mapak wahusika wanafikia umri wa kustaafu na wanaondoka wakikabidhiwa mafao yao...kweli tanzania ni kisima cha ngonjera
 
Keil,

Mimi nilikuwa hasa naongelea hilo suala la RA kufuatilia pesa na ndio maana nikasema wachunguzi waliobobea wanasema follow the money, atakayekutwa na pesa za wizi ndio mwizi.

Labda nifahamishe wapi report ya Mwakyembe na viambatanisho vyake wanaongelea hilo jambo?

Hayo mambo ya ofisi na sanduku la posta najua yamo kwenye report ya mwakyembe.

 

- Ripoti ya Mwakyembe iko wazi kwamba Caspian/Dowans ni Rostam, ambako hela za Richimonduli zilikuwa zikienda na ni Rostam aliyesaini mkataba wa Dowans na serikali,

- Rostam alisaini kwa Dowans na Mgonja kwa serikali, eti mnataka nini tena zaidi ya ushahidi wote huu? au ni wapiganaji ndio wenye makosa hapa?

Respect.


FMEs!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…