Ndugu yangu Mtanzania,
Ulisoma report yote ya Mwakyembe ama ulisimuliwa? Uliona viambatanisho vyote vya hiyo report? Kwanini unasema kwamba haya yaliyoandikwa kwenye gazeti la MwanaHalisi ama kwa maneno mengine maneno aliyoyasema Mbunge Selelii hayakuwamo kwenye report?
Hayo ndio mambo ambayo walitakiwa kuyaweka kwenye report ya Richmond lakini hawakufanya hivyo, why?
Kwenye kipengele walichokuwa wanaeleza kwanini walitaka kumhoji RA, walisema wazi kwamba kuna vitu walikuta ambavyo ni vya Caspian lakini vilikuwa vinatumiwa na Dowans, mfano, anuani ya posta, e-mail address, na baadhi ya wafanyakazi wa Caspian walikuwa ni wafanyakazi wa Dowans. Leo hii unakuja kutuambia haya hayakuwamo kwenye report? Hapa sikubaliani na wewe, ndiyo maana nikasema labda hukusoma report yote.
Au ulitaka waandike kwenye report kwamba walimshirikisha Rais? Kwamba walifanya utaratibu gani kumpa report mapema?
Kama wanachoandika sasa ni sahihi, ilikuwa muhimu mno kumhoji Rostam maana mahojiano chini ya kiapo cha bunge yangelikuwa na maana zaidi, huko ndiko kungelikuwa ni kumfunga paka kengere. Nashangaa pamoja na info wanazotoa sasa, walishindwa kutumia nguvu ya bunge kuwahoji hawa wahusika. Hata kama Rostam asingeenda kuhojiwa kwa mapenzi yake, kuna njia zingine ambazo zingemlazimisha yeye kuhojiwa.
Mimi nina amini kwamba kilichoandikwa ni sahihi na ndiyo maana Lowassa hakutaka kujibu hoja zao akakimbilia kujiuzulu. Kumbuka kwamba alipewa report a day kabla ya kuwasilishwa, so he had more than 48 hrs za kuipitia na kuangalia kama anaweza kujibu hoja. Kama hakuhusika na kwa jinsi ninavyomfahamu, angepangua hoja moja baada ya nyingine. The problem ni kwamba alishajua hana ubavu wa kujibu hoja hizo. Matokeo yake akaishia kujibu report kwa staili ya Sofia Simba (mipasho style) kitu ambacho kimeharibu jina lake mpaka leo na ndio maana ana haha kuangalia namna ya kujisafisha.
RA alikwepa kwa makusudi kabisa kuhojiwa na hiyo kamati kwa kuwa hakujua jamaa wana info kiasi gani na angejipeleka angejimaliza mwenyewe, ndipo akaja na hiyo janja janja ya kujifanya ana safari za kibiashara. Lakini ukweli ni kwamba aliwakwepa, hakutaka kwenda kichwa kichwa bila kujua jamaa walikuwa wanafahamu nini.
Hii kamati ilikuwa na nafasi ya kuisafisha serikali kwa kutoa ukweli wote lakini bahati mbaya wakaamua kulindana. Sasa wameanza kugombana ndio wanajifanya eti wanataka kutoa ukweli wote, huo ni usanii tu wa kisiasa wa kutaka kutudanganya wananchi.
Wameanza kugombana lini? Wameanza kugombana leo? Report ni ya 2008, na yalisemwa hayo yote na kuna viambatanisho lundo ambavyo hata sisi wengine hatujui vina nini. Ulitaka waseme nini?
Miaka mitatu tunapiga mduara kwenye jambo moja huku hali ya umeme inazidi kuwa duni na kuathiri uzalishaji na huduma zingine. Ifike mahali tulimalize hili suala na kuhangaika na mambo mengine kwa faida ya wananchi wote.
Ni kwa kuwa Kikwete na serikali yake wanaendelea kupiga chenga na wanaonekana kuzidiwa nguvu na mafisadi ndiyo maana bado tunaendelea kuongelea Richmond ambayo ilitakiwa iwe imemalizwa tangu mwaka jana, may be serikali ilihitaji miezi 6 kusafisha kila kitu. Hujiulizi kwanini wale wote ambao walitakiwa kuchukuliwa hatua mamlaka zao wameishia wameishia kustaafu, hata kama ni kabla ya umri wao. Bado utawabebesha wabunge lawama hizo?
Hii kamati ya Richmond wasalimishe documents zote walizo nazo kwa spika na polisi, ili vyombo vya umma vizipitie na kuchukua hatua pale inapobidi. Kutoa habari nusu nusu kwa faida zao kisiasa ni abuse of power. Walipewa hiyo kazi kwa niaba ya bunge na wananchi. Wanatakiwa kutuambia wananchi ukweli wote na hawana haki ya kuficha baadhi ya documents.
Pendekezo lako la mwisho limeniacha hoi, hivi wewe bado una imani na Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na TAKUKURU?
Kwani TAKUKURU walipofanya kazi hiyo mara ya kwanza walikuja na report gani? Excuse wanayotupatia ni kwamba walitumia sheria ya TAKURU and the deal was clean. Hivi pamoja na huu uchafu wote Lawyer Dr. Hoseah anaweza kuja kusema mbele za watu kwamba the deal was clean?
Tuje kwa Usalama wa Taifa, JK alijitetea kwamba alizuwia malipo akihisi kwamba inaweza kuwa ni kampuni fake. Je, Usalama wa Taifa walikuwa wapi kufanya kazi ya kuchunguza kama kampuni hiyo ilikuwa ni genuine ama fake? Kweli Rais wa nchi anashitukia deal, Usalama wa Taifa wamelala! Kwanini hawaku-act immediately baada ya kuona kelele zimezidi kwenye magazeti? Mpaka mtaalam RA akashituka na kuweka watu waliobobea kupika majungu akina Salva ili kusafisha hali hewa, UwT wao wapo tu, hao ndio wapelekewe documents ili waende kuzi-destroy? Kwani hivyo vyombo vya dola havijui akina Mwakyembe walipata wapi hizo documents? Wao kama wako serious si wangetumia hizo leads za report ya Mwakyembe ili kufuatilia na waanze kuwashughulikia wale wote waliohusika.
Wabunge na Kamati ya Mwakyembe walifanya kile walichoweza kufanya, tatizo ni serikali yetu inalinda mafisadi kwa nguvu zote na hili limejidhihirisha kwenye utekelezaji wa maazimio ya Bunge. Hakuna hata moja lililofanyika, yote ni usanii kwa kwenda mbele na bado wanapiga chenga mpaka leo.
Pinda alipochukua kiti cha PM alisema angepeleka report yeye mwenyewe na kwamba apewe miezi 6 tu. Leo ni miezi karibu 18, hakuna kitu. Labda wanasubiri Hoseah afikishe umri wa kustaafu ndipo wataenda kupeleka report Bungeni.