Selelii awazima Lowassa na Rostam

Selelii awazima Lowassa na Rostam

Kuandamana?? nani afanye huo ujinga wa kupigwa mabomu kwa kumsemesha kiziwi JK asiyeona hata nchi inakokwenda yeye anaona sawa tu

- Ohhh Safi sasa finally unaongea hoja kwamba Rais wetu ni kiziwi, lakini tusilaumu bunge kwa sababu limetimiza wajibu wake,

- ya Rais kiziwi then inamaana tunahitaji kunyamaza kuliko kuendelea kuwashambulia wabunge maana they did their job!

FMEs!

RA alikataa kutokea kwa hiari yake; kamati ya bunge ilikuwa na nguvu na uwezo wa kutumia njia zingine halali kisheria kuwalazimishiwa watuhumiwa kuhojiwa.

Kama wahusika wakubwa kwenye hili ni Lowassa na RA, ninashangaa kweli hii kamati ilishindwa kutumia nguvu zake kisheria kuwahoji hawa watu. Maneno ambayo wangeyasema mbele ya hicho kikao, yangelikuwa na nguvu na ingelikuwa hata rahisi kuwachukulia hatua za kisheria.
Mimi naona kamati ilifanya kile kilichotakiwa, wewe ukiitwa mahakamani akakata mahakama ina mawili ya kufanya kuhukumu kesi bila ushahidi wako au kukulazimisha kutoa ushahidi wako.
Hapa kamati iliona haina haja ya kumlazimisha yeye kaitwa, kaona safari zake za binafsi/biashara bora kuliko hiyo kamati na masuala ya kitaifa, wao wamehoji watu wengine wakapata walicho taka, kuhusu waziri mkuu, huyo ni very senior person, ndio maana wakasema ajipime yeye mwenyewe, kama aliona hakufanya kosa angebaki, na wala kamati haiku-muhukumu, walimwambia "ajipime", haya mengine unayosema ndio hayo kamati ya Bunge ilipoyapa serikali kuyafanya iwe kuwapeleka mahakamani, kutumia takukuru etc Utekelezajio wa maazimio ya Bunge.
Na kama ushahidi zaidi wana utaka kamati ya bunge ipo tayari kuutoa kwa vyombo vinavyo husika.
iwe mahakamani na kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.
Hii kesi au uchunguzi ilikuwa aidha ni ya kwanza au katika hizo chache au ndra kufanywa na Bunge na kutolewa maamuzi, na si wote walikuwa wanasheria hivyo hawakumalizia report kama hukumu ya mahakamani , bali kuitaka serikali ichukue hatua zifaazo kulimaliza hili suala, na baada ya hapo serikali ije na report ya utekelezaji. kumbuka hawa wabunge wanashughuli zingine za ki-bunge na kisiasa, sasa hayo mengine muda hakutosha amasivyo wange pewa mamlaka hayo ya kuwa mahakama, kazi yao ilikuwa kufanya uchunguzi na kutoa report. sio hukumu hiyo ni stage nyingine kabisa. no one had predicated vitu watakavyo kutana navyo huko.
 
So according to you mtetezi wa mafisadi if nothing is happening then we should all forget about mafisadi who're plundering the wealth of our beloved country while millions of our fellow Tanzanians are living in very poor conditions.

Kanywe Tusker wewe fisadi ambaye unataka RICHMOND ipotee katika mijadala ya Watanzania ili muendelee kuchota mabilioni. Watu wengine kwa kujikweza bwana! Duh! Who do you think you are!? Wabunge ambao ni wawakilishi wa Watanzania katika majimbo mbali mbali walikaa kumsikiliza Selelii bila kuchoka lakini wewe fisadi umeshachoka na sijui kauli yako hapa inamuwakilisha nani!? na huu mjadala wa RICHMOND unakukera sana unataka uachwe ili watu wakanywe Tusker! 😕 Kweli ukistaajabu ya Mussa...... Na wewe utajidai una mapenzi ya kweli na nchi yako wakati hutaki ufisadi uliokithiri ndani ya Tanzania ujadiliwe! Kanywe Tusker zako na tuache sisi tunaotaka kujadili hali ya nchi yetu tufanye hivyo.

- Mkulu Bubu, please do not waste your time and energy kwani mpaka sasa hujajua huyu ni nani mkuu? Please mkuu you are too big for this huyu uwe unatuachia sisi ndio tunaijua sana lugha anayoijua, halafu anakimbilia kule chini kulalamika kwamba anaonewa!

- Bubu you are too big for this!

Respect.

FMEs!
 
............- Haya maelezo yote aliyoyatoa Seleli yamo kwenye ripoti yao ya kamati,
Respect.

FMEs!

Mkuu napenda kusisitiza hilo hapo juu kuwa ni sahihi,...........watch out though kuna watu wana ajenda zao hapa...........na hii ni hatari
 
Mkuu napenda kusisitiza hilo hapo juu kuwa ni sahihi,...........watch out though kuna watu wana ajenda zao hapa...........na hii ni hatari

- Mkuu Ogah wala usiwe na wasi wasi, agenda yao ni Sophia Simba tunawajua, wamepiga mwamba maana Seleli ameweka facts as opposed na mipasho.

Respect.

FMEs!
 
- Bunge limetimiza kazi yake, sasa wewe utueleze unataka nini hasa? The only thing wananchi we can do hapa ni kuandamana kuwashinikiza Rais na Waziri Mkuu kuchukua hatua kufuatilia mapendekezo ya bunge, ikibidi kuwazomea na kuwarushia mawe unakumbuka last time haya yalipofanyika Mramba na Yona wakapelekwa Rumande kutunyamazisha!

- Sasa wewe utueleze unataka nini maana bunge limemaliza kazi yake tayari on the ishu?

FMEs!

Bunge limepewa mamlaka ya Kuidhinisha mipango yoyote ya muda mfupi au mrefu ya JMT. Katika kuidhinisha linanguvu ya kukataa kubadilisha au hata kutoa maelekezo ya nini kifanyike. Na likikataa (nguvu yake ya kusimamia) serikali (RAis) hawezi kuendelea na mpango huo. Wabunge wasipojua nguvu yao hii ndio sababu serikali wakati mwingine inajifanyia tu mambo yake.

Msingi wa nguvu hii ni kuwa Bunge ndio wawakilishi wa watu siyo Rais. Falsafa nzima ya utawala wa demokrasia ni kuwapa nguvu watu siyo mtu mmoja. Ndio sababu ya Magna Carta, mapinduzi ya Ufaransa na yale ya Marekani.

Katika Tanzania wabunge wetu wanataka kupoteza nguvu hii na kumwachia Rais cheki isiyojazwa. Hatuwezi na hatupaswi kuwaacha wabunge waache jukumu lao la kuisimamia serikali na hata kuilazimisha serikali kufanya kile sisi wananchi tunataka wafanye. This amounts to relegation of duty.

Kama serikali inaweza kufanya lolote bila kulazimishwa au kusimamiwa na Bunge, basi hatulihitaji Bunge! what for? kupitisha bajeti tu? Rais si anaweza kufanya hivyo yeye mwenyewe?

By M.M.Mwanakijiji

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...lele-za-kingunge-hazininyimi-usingizi-11.html

Mkuu ukisoma post namba 104 utajua kazi na Mamlaka ya bun
 
Wananchi watamshinikiza Rais au waziri mkuu kupitia wawakilishi wao yaani Wabunge
 
By M.M.Mwanakijiji

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...lele-za-kingunge-hazininyimi-usingizi-11.html

Mkuu ukisoma post namba 104 utajua kazi na Mamlaka ya bun
samahani kama tutakuwa tumipishana kwenye dhana ya post yako hapo juu aidha yapo sawa, au yapo tofauti, ni kwamba Kamati ya Bunge au Bunge halina mamlaka ya kuhukumu, labda hiyo kamati iapishwe kwenda kusimamia issue na kui-hukumu, lazima tutofautishe bunge linapo kaa kama kamati ya uchunguzi au ya kutoa hukumu. na hili litaelezwa kwenye hadidu za uundaji wake. Na kama wanatakiwa kuhukumu ni lazima waapishwe kutekeleza hilo.
Kumbuka wabunge waliapishwa kufanya kazi za kibunge na sio kutoa hukumu. hivyo hizi nguvu za bunge zinakuja kwenye mambo yanayo tokea kila siku, na kama bunge litakuwa lina upungufu wa facts basi wataitaka serikali kufanya hivyo na kuleta report ya utekelezaji bunge, kinyume cha hapo ndipo bunge linaweza kutumia mamlaka zake kulazimisha hicho kitu kwa kupiga kura au kutoa maazimio ya bunge.
 
Mkuu Mkandara,

Ni kweli wananchi tunataka ukweli; tunataka ukweli wote na wala sio nusu nusu.

Hayo ndio mambo ambayo walitakiwa kuyaweka kwenye report ya Richmond lakini hawakufanya hivyo, why?

Kwenye uchunguzi wowote, watu wanasema follow the money? Sasa kama walijua hata fedha zilikuwa zinatumwaje na nani alikuwa anafuatilia, mbona hiyo ndio ingelikuwa taarifa muhimu zaidi?

Kama wanachoandika sasa ni sahihi, ilikuwa muhimu mno kumhoji Rostam maana mahojiano chini ya kiapo cha bunge yangelikuwa na maana zaidi, huko ndiko kungelikuwa ni kumfunga paka kengere. Nashangaa pamoja na info wanazotoa sasa, walishindwa kutumia nguvu ya bunge kuwahoji hawa wahusika. Hata kama Rostam asingeenda kuhojiwa kwa mapenzi yake, kuna njia zingine ambazo zingemlazimisha yeye kuhojiwa.

Hii kamati ilikuwa na nafasi ya kuisafisha serikali kwa kutoa ukweli wote lakini bahati mbaya wakaamua kulindana. Sasa wameanza kugombana ndio wanajifanya eti wanataka kutoa ukweli wote, huo ni usanii tu wa kisiasa wa kutaka kutudanganya wananchi.

Miaka mitatu tunapiga mduara kwenye jambo moja huku hali ya umeme inazidi kuwa duni na kuathiri uzalishaji na huduma zingine. Ifike mahali tulimalize hili suala na kuhangaika na mambo mengine kwa faida ya wananchi wote.

Hii kamati ya Richmond wasalimishe documents zote walizo nazo kwa spika na polisi, ili vyombo vya umma vizipitie na kuchukua hatua pale inapobidi. Kutoa habari nusu nusu kwa faida zao kisiasa ni abuse of power. Walipewa hiyo kazi kwa niaba ya bunge na wananchi. Wanatakiwa kutuambia wananchi ukweli wote na hawana haki ya kuficha baadhi ya documents.
Mkuu wangu nawe unaingia mkumbo huu...
Ushahidi wote wakupe wewe wa nini ikiwa wewe sii mwamuzi?.. Hata hizo kesi za kawaida uchunguzi unapofanywa wananchi huwa hampewi kila kitu kwani kuna rights za mtuhumiwa ambaye he is not guilty until proven guilty na mahakama. Na unataka wasalimishe mara ngapi? hivi huna habari JK, Bunge na vyombo vyote vya sheria wanayo report hiyo au umewekwa kizani!..
Wakuu zangu hili swala la Mafisadi mnalichukulia mzaha sana na badala ya kutumia akili mnataka liwe swala la kihuni kihuni kama inavyokwenda sasa hivi..

Kamati ya Mwakyembe ilikuwa na haki zote kutoelezea kila kitu ila mbele ya sheria isipokuwa walichjoweza kufanmya ni kuhakikisha watuhumiwa kuwa hatiani...hatua iliyofuata hapo sii jukumu lao tena. Huu ndio utaratibu unaotumika sehemu zote duniani lakini wewe ukitaka upewe ukweli wote while wewe sii mwamuzi, kisha upande wa watuhumiwa (kina Lowassa) waitumie report ile kama imewahukumu kabla ya vyombo vya sheria..Yale machache tu yaliyokuwepo tayari imesemekana Lowassa hakutendewa haki iwe kutoa report nzima nje vy9ombo vya sheria!

Kwa mtu mwenye kuelewa utagundua kwamba Selali ameyazungumza haya kwa hasira ya ISIWE TAABU, kwani kazi mlonipa nimeifanya sasa mnataka kunigeuzia kibao. Na maadam inaonyesha wazi hakuna sheria ni uswahili mtupu basi madudu yenu ni hayo!
Leo wewe baada ya kuyapokea madudu hayo mnatafuta tena sababu nyingine ati kwa nini hakusema toka mwanzo! Imean kwa Wadanganyika hakuna laa maana kabisa, ni uswahili mtupu kiasi kwamba hata sheria tunazipuuza kwa uswahili.

Kisha basi mnawasema Wabunge kwamba hawafanyi kazi yao wakati hao wazuri kidogo mnawazomea na kina Lowassa na Chenge mnawapokea kwa ngoma na vifijo mkiiwaita mashujaa. Jamani hivi kweli nyie mnaitakia mema nchi hii au ni mawazo mgando yaliyonyingwa kwa umaskini wa hali na mali..
Samahani mkuu wangu, kwanza fikiria picha nzima ya sakata hili la Richmond na jinsi walivyoliharibu makusudi halafu wasomi kama nyie wenye exposure ya sheria za wenzetu wanavyofanya nanyi mnaingia ktk fuko hilo hilo la Udanganyika!..Nakuomba rudia kusoma report utangua kwamba Rostam hakutaka kuhojiwa kabisa...
Duh inasikitisha sana..inauma sana kuona wananchi ambao mlitakiwa kuwasukuma wabunge wetu kuwakilisha matakwa yenu ndio kwanza mnachagua upande wa Ufisadi..Mtanzania hutaki kusikia ukweli isipokuwa unachotaka ni kuwaondoa uhalali wapiganaji.. U have you own mission ambayo naifahamu vizuri...Usituingize sote mkuu wangu hiyo ni kazi yako mwenyewe kwa maslahi yako na wana Kyela.... Plse!

Hata mimi ningekuwa mbunge nisingejiweka ktk kundi la Wapiganaji kwa sababu wananchi wangu hawataki kusikia Lowassa na Rostam wakiitwa Mafisadi..yet mnawataka wachukue hatua fulani zisijulikana.
 
Mtanzania said:
Hii kamati ilikuwa na nafasi ya kuisafisha serikali kwa kutoa ukweli wote lakini bahati mbaya wakaamua kulindana. Sasa wameanza kugombana ndio wanajifanya eti wanataka kutoa ukweli wote, huo ni usanii tu wa kisiasa wa kutaka kutudanganya wananchi.

Mtanzania,

..I am 100% with you on this one.

..kama pamoja na ripoti ile bado Rostam anashughulika na Richmond basi kuna siri kubwa nyuma yake.

..kauli ya Mwakyembe kwamba kuna mambo wameyaficha ili kulinda heshima ya serikali inazua maswali mengi sana kuhusu ripoti yao.

..kwa upande mwingine naona kama "mafisadi" nao they are daring "wapiganaji" ktk suala la Richmond. wanafanya hivyo kuwapima kama wana uwezo wa kutoa ukweli wote kuhusu dubwana hili.

..najua inasikitisha/inakera...labda wananchi tufike mahali na tuwe "realistic", and resign to the fact kwamba, kitakachofanyika ni kutoa "fundisho" tu kwa watumishi wa serikali, lakini ukweli mzima kuhusu Richmond hautajulikana, na wahusika wakuu au masterminds wa Richmond hawatachukuliwa hatua yoyote.

..hii kashfa ya Richmond inafanana sana na ile kashfa ya Iran-Contra.

..vilevile ukikusanya mahela ya kampeni toka kwa wafanyabiashara wakubwa, basi itafika mahali watadai warudishiwe pesa zao. sasa miradi michafu-michafu kama Richmond ni njia mojawapo ya kufanikisha malipo hayo.

NB:

..Waswahili wana msemo wao "majuto ni mjukuu."

..wakati tunamchagua JK, hatukufikiria kabisa atamlipa vipi fadhila za Rostam Aziz.
 
Jokakuu,
Hiyo ni kazi ya utawala na vyombo vya sheria na sii kamati ya Mwakyembe..wao wamelisha ujumbe waliotumwa, kilichotakiwa ili kupata ukweli ni pale bunge au Takukuru ingewaita kutoa ushahidi mbele ya kiapo..Mnaifanya kesi hii kama vile kamati ya Mwakyembe ndio washtaka!
 
Mkandara,

..vyombo vya sheria vipi ndugu yangu?

..Rostam anafuatilia malipo ya Richmond/Dowans mpaka Hazina halafu unaleta habari za vyombo vya sheria?

..kinachoendelea hapa ni jitihada za kumrudishia Rostam pesa zake alizotumia kwenye kampeni za wanamtandao.
 
Ndugu yangu Mtanzania,

Ulisoma report yote ya Mwakyembe ama ulisimuliwa? Uliona viambatanisho vyote vya hiyo report? Kwanini unasema kwamba haya yaliyoandikwa kwenye gazeti la MwanaHalisi ama kwa maneno mengine maneno aliyoyasema Mbunge Selelii hayakuwamo kwenye report?

Hayo ndio mambo ambayo walitakiwa kuyaweka kwenye report ya Richmond lakini hawakufanya hivyo, why?

Kwenye kipengele walichokuwa wanaeleza kwanini walitaka kumhoji RA, walisema wazi kwamba kuna vitu walikuta ambavyo ni vya Caspian lakini vilikuwa vinatumiwa na Dowans, mfano, anuani ya posta, e-mail address, na baadhi ya wafanyakazi wa Caspian walikuwa ni wafanyakazi wa Dowans. Leo hii unakuja kutuambia haya hayakuwamo kwenye report? Hapa sikubaliani na wewe, ndiyo maana nikasema labda hukusoma report yote.

Au ulitaka waandike kwenye report kwamba walimshirikisha Rais? Kwamba walifanya utaratibu gani kumpa report mapema?

Kama wanachoandika sasa ni sahihi, ilikuwa muhimu mno kumhoji Rostam maana mahojiano chini ya kiapo cha bunge yangelikuwa na maana zaidi, huko ndiko kungelikuwa ni kumfunga paka kengere. Nashangaa pamoja na info wanazotoa sasa, walishindwa kutumia nguvu ya bunge kuwahoji hawa wahusika. Hata kama Rostam asingeenda kuhojiwa kwa mapenzi yake, kuna njia zingine ambazo zingemlazimisha yeye kuhojiwa.

Mimi nina amini kwamba kilichoandikwa ni sahihi na ndiyo maana Lowassa hakutaka kujibu hoja zao akakimbilia kujiuzulu. Kumbuka kwamba alipewa report a day kabla ya kuwasilishwa, so he had more than 48 hrs za kuipitia na kuangalia kama anaweza kujibu hoja. Kama hakuhusika na kwa jinsi ninavyomfahamu, angepangua hoja moja baada ya nyingine. The problem ni kwamba alishajua hana ubavu wa kujibu hoja hizo. Matokeo yake akaishia kujibu report kwa staili ya Sofia Simba (mipasho style) kitu ambacho kimeharibu jina lake mpaka leo na ndio maana ana haha kuangalia namna ya kujisafisha.

RA alikwepa kwa makusudi kabisa kuhojiwa na hiyo kamati kwa kuwa hakujua jamaa wana info kiasi gani na angejipeleka angejimaliza mwenyewe, ndipo akaja na hiyo janja janja ya kujifanya ana safari za kibiashara. Lakini ukweli ni kwamba aliwakwepa, hakutaka kwenda kichwa kichwa bila kujua jamaa walikuwa wanafahamu nini.

Hii kamati ilikuwa na nafasi ya kuisafisha serikali kwa kutoa ukweli wote lakini bahati mbaya wakaamua kulindana. Sasa wameanza kugombana ndio wanajifanya eti wanataka kutoa ukweli wote, huo ni usanii tu wa kisiasa wa kutaka kutudanganya wananchi.

Wameanza kugombana lini? Wameanza kugombana leo? Report ni ya 2008, na yalisemwa hayo yote na kuna viambatanisho lundo ambavyo hata sisi wengine hatujui vina nini. Ulitaka waseme nini?

Miaka mitatu tunapiga mduara kwenye jambo moja huku hali ya umeme inazidi kuwa duni na kuathiri uzalishaji na huduma zingine. Ifike mahali tulimalize hili suala na kuhangaika na mambo mengine kwa faida ya wananchi wote.

Ni kwa kuwa Kikwete na serikali yake wanaendelea kupiga chenga na wanaonekana kuzidiwa nguvu na mafisadi ndiyo maana bado tunaendelea kuongelea Richmond ambayo ilitakiwa iwe imemalizwa tangu mwaka jana, may be serikali ilihitaji miezi 6 kusafisha kila kitu. Hujiulizi kwanini wale wote ambao walitakiwa kuchukuliwa hatua mamlaka zao wameishia wameishia kustaafu, hata kama ni kabla ya umri wao. Bado utawabebesha wabunge lawama hizo?

Hii kamati ya Richmond wasalimishe documents zote walizo nazo kwa spika na polisi, ili vyombo vya umma vizipitie na kuchukua hatua pale inapobidi. Kutoa habari nusu nusu kwa faida zao kisiasa ni abuse of power. Walipewa hiyo kazi kwa niaba ya bunge na wananchi. Wanatakiwa kutuambia wananchi ukweli wote na hawana haki ya kuficha baadhi ya documents.

Pendekezo lako la mwisho limeniacha hoi, hivi wewe bado una imani na Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na TAKUKURU?

Kwani TAKUKURU walipofanya kazi hiyo mara ya kwanza walikuja na report gani? Excuse wanayotupatia ni kwamba walitumia sheria ya TAKURU and the deal was clean. Hivi pamoja na huu uchafu wote Lawyer Dr. Hoseah anaweza kuja kusema mbele za watu kwamba the deal was clean?

Tuje kwa Usalama wa Taifa, JK alijitetea kwamba alizuwia malipo akihisi kwamba inaweza kuwa ni kampuni fake. Je, Usalama wa Taifa walikuwa wapi kufanya kazi ya kuchunguza kama kampuni hiyo ilikuwa ni genuine ama fake? Kweli Rais wa nchi anashitukia deal, Usalama wa Taifa wamelala! Kwanini hawaku-act immediately baada ya kuona kelele zimezidi kwenye magazeti? Mpaka mtaalam RA akashituka na kuweka watu waliobobea kupika majungu akina Salva ili kusafisha hali hewa, UwT wao wapo tu, hao ndio wapelekewe documents ili waende kuzi-destroy? Kwani hivyo vyombo vya dola havijui akina Mwakyembe walipata wapi hizo documents? Wao kama wako serious si wangetumia hizo leads za report ya Mwakyembe ili kufuatilia na waanze kuwashughulikia wale wote waliohusika.

Wabunge na Kamati ya Mwakyembe walifanya kile walichoweza kufanya, tatizo ni serikali yetu inalinda mafisadi kwa nguvu zote na hili limejidhihirisha kwenye utekelezaji wa maazimio ya Bunge. Hakuna hata moja lililofanyika, yote ni usanii kwa kwenda mbele na bado wanapiga chenga mpaka leo.

Pinda alipochukua kiti cha PM alisema angepeleka report yeye mwenyewe na kwamba apewe miezi 6 tu. Leo ni miezi karibu 18, hakuna kitu. Labda wanasubiri Hoseah afikishe umri wa kustaafu ndipo wataenda kupeleka report Bungeni.
 
Mkandara,

..vyombo vya sheria vipi ndugu yangu?

..Rostam anafuatilia malipo ya Richmond/Dowans mpaka Hazina halafu unaleta habari za vyombo vya sheria?

..kinachoendelea hapa ni jitihada za kumrudishia Rostam pesa zake alizotumia kwenye kampeni za wanamtandao.
Kwa hiyo lawama zote unawashushia kamati ya kina Selali na Wapiganaji! yaani sielewi mkuu wangu point yenu hasa ni ipi.
 
Mkandara,

..we will never get to the bottom of this scandal.

..kwa mtizamo wangu yaliyofichwa na kamati yanaweza kuwa na umuhimu kuliko yaliyowasilishwa bungeni na kwa wananchi.

..ninashawishika kuamini hivyo kutokana na mwenendo mzima wa serikali na watu kama Rostam tangu kutolewa kwa ripoti ya Mwakyembe.

..this is our own Iran-Contra.
 
Mkandara,

..vyombo vya sheria vipi ndugu yangu?

..Rostam anafuatilia malipo ya Richmond/Dowans mpaka Hazina halafu unaleta habari za vyombo vya sheria?

..kinachoendelea hapa ni jitihada za kumrudishia Rostam pesa zake alizotumia kwenye kampeni za wanamtandao.

- Kosa la nani hili mkuu?

FMEs!
 
Mtanzania,

..I am 100% with you on this one.

NB:

..Waswahili wana msemo wao "majuto ni mjukuu."

..wakati tunamchagua JK, hatukufikiria kabisa atamlipa vipi fadhila za Rostam Aziz
.

- Finally, you make a lot of sense kuliko huko kwingine.

Es!
 
Jokakuu,
Mkuu wangu utaratibu wa Bunge mwakilishi husoma tu vifungu vya maelezo yote kwa ufupi lakini report nzima inaweza kuwa na kurasa 2,000.
Bunge (Spika) walipata report yote na wameikalia,, vyombo vya sheria wanayo report yote wameikalia, JK aliipata report nzima kwahiyo hizi habari za kusema kamati haikusema yote ni habari ambazo zinashindwa kuzingatia sheria. Kamati isigeweza kumhukumu Lowassa au Rostam ktk report ile kwa kusema ushahidi huo as a third party (hearsay)..Hapo isingekuwa tu wamepoteza kesi na pengine hata kuvuruga chama. Bunge ndilo lilitakiwa kuanzisha kesi hiyo na mashahidi waliotoa ushahidi waliokusanya wangeitwa kuhakikisha na confirm report nzima.. haikutoa hivyo..Kina Mwakyembe hawana makosa kabisa na nina hakika Mwakyembe ni mwanasheria anajua alichokifanya.
 
Ndugu yangu Mtanzania,

Ulisoma report yote ya Mwakyembe ama ulisimuliwa? Uliona viambatanisho vyote vya hiyo report? Kwanini unasema kwamba haya yaliyoandikwa kwenye gazeti la MwanaHalisi ama kwa maneno mengine maneno aliyoyasema Mbunge Selelii hayakuwamo kwenye report?

Kwenye kipengele walichokuwa wanaeleza kwanini walitaka kumhoji RA, walisema wazi kwamba kuna vitu walikuta ambavyo ni vya Caspian lakini vilikuwa vinatumiwa na Dowans, mfano, anuani ya posta, e-mail address, na baadhi ya wafanyakazi wa Caspian walikuwa ni wafanyakazi wa Dowans. Leo hii unakuja kutuambia haya hayakuwamo kwenye report? Hapa sikubaliani na wewe, ndiyo maana nikasema labda hukusoma report yote.

Au ulitaka waandike kwenye report kwamba walimshirikisha Rais? Kwamba walifanya utaratibu gani kumpa report mapema?

Mimi nina amini kwamba kilichoandikwa ni sahihi na ndiyo maana Lowassa hakutaka kujibu hoja zao akakimbilia kujiuzulu. Kumbuka kwamba alipewa report a day kabla ya kuwasilishwa, so he had more than 48 hrs za kuipitia na kuangalia kama anaweza kujibu hoja. Kama hakuhusika na kwa jinsi ninavyomfahamu, angepangua hoja moja baada ya nyingine. The problem ni kwamba alishajua hana ubavu wa kujibu hoja hizo. Matokeo yake akaishia kujibu report kwa staili ya Sofia Simba (mipasho style) kitu ambacho kimeharibu jina lake mpaka leo na ndio maana ana haha kuangalia namna ya kujisafisha.

RA alikwepa kwa makusudi kabisa kuhojiwa na hiyo kamati kwa kuwa hakujua jamaa wana info kiasi gani na angejipeleka angejimaliza mwenyewe, ndipo akaja na hiyo janja janja ya kujifanya ana safari za kibiashara. Lakini ukweli ni kwamba aliwakwepa, hakutaka kwenda kichwa kichwa bila kujua jamaa walikuwa wanafahamu nini.

Wameanza kugombana lini? Wameanza kugombana leo? Report ni ya 2008, na yalisemwa hayo yote na kuna viambatanisho lundo ambavyo hata sisi wengine hatujui vina nini. Ulitaka waseme nini?

Ni kwa kuwa Kikwete na serikali yake wanaendelea kupiga chenga na wanaonekana kuzidiwa nguvu na mafisadi ndiyo maana bado tunaendelea kuongelea Richmond ambayo ilitakiwa iwe imemalizwa tangu mwaka jana, may be serikali ilihitaji miezi 6 kusafisha kila kitu. Hujiulizi kwanini wale wote ambao walitakiwa kuchukuliwa hatua mamlaka zao wameishia wameishia kustaafu, hata kama ni kabla ya umri wao. Bado utawabebesha wabunge lawama hizo?

Pendekezo lako la mwisho limeniacha hoi, hivi wewe bado una imani na Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na TAKUKURU?

Kwani TAKUKURU walipofanya kazi hiyo mara ya kwanza walikuja na report gani? Excuse wanayotupatia ni kwamba walitumia sheria ya TAKURU and the deal was clean. Hivi pamoja na huu uchafu wote Lawyer Dr. Hoseah anaweza kuja kusema mbele za watu kwamba the deal was clean?

Tuje kwa Usalama wa Taifa, JK alijitetea kwamba alizuwia malipo akihisi kwamba inaweza kuwa ni kampuni fake. Je, Usalama wa Taifa walikuwa wapi kufanya kazi ya kuchunguza kama kampuni hiyo ilikuwa ni genuine ama fake? Kweli Rais wa nchi anashitukia deal, Usalama wa Taifa wamelala! Kwanini hawaku-act immediately baada ya kuona kelele zimezidi kwenye magazeti? Mpaka mtaalam RA akashituka na kuweka watu waliobobea kupika majungu akina Salva ili kusafisha hali hewa, UwT wao wapo tu, hao ndio wapelekewe documents ili waende kuzi-destroy? Kwani hivyo vyombo vya dola havijui akina Mwakyembe walipata wapi hizo documents? Wao kama wako serious si wangetumia hizo leads za report ya Mwakyembe ili kufuatilia na waanze kuwashughulikia wale wote waliohusika.

Wabunge na Kamati ya Mwakyembe walifanya kile walichoweza kufanya, tatizo ni serikali yetu inalinda mafisadi kwa nguvu zote na hili limejidhihirisha kwenye utekelezaji wa maazimio ya Bunge. Hakuna hata moja lililofanyika, yote ni usanii kwa kwenda mbele na bado wanapiga chenga mpaka leo.

Pinda alipochukua kiti cha PM alisema angepeleka report yeye mwenyewe na kwamba apewe miezi 6 tu. Leo ni miezi karibu 18, hakuna kitu. Labda wanasubiri Hoseah afikishe umri wa kustaafu ndipo wataenda kupeleka report Bungeni.

- Strong point!

Es!
 
Mkandara,

..we will never get to the bottom of this scandal.

Hivi ndivyo wanavyotaka watuhumiwa wote katika sakata hili la Richmond/Dowans ili mafisadi hao waendelee kupeta na malipo yao ya $172 milioni ambayo hawakuyafanyia kazi maana ukweli ni kwamba hawakuzalisha umeme hata tone.

Lakini kwa Watanzania tulio wengi na tunaotaka kuona kwamba mafisadi wanachukuliwa hatua za kisheria zinazowastahili na pia ufisadi kukomeshwa ndani ya nchi yetu ili tuweze kupata maendeleo ya kweli tunataka kujua ukweli wote wa nini kilichojiri katika sakata la Richmond. Kama Kikwete kwa namna moja au nyingine anawaogopa kuwachukulia hatua wahusika wote wa Richmond/Dowans wakiwemo Lowassa na Rostam basi hatufai kuwa kiongozi wa nchi yetu. Ana madaraka makubwa ya kuweza kumchukulia hatua za kisheria mkosaji yeyote ndani ya nchi yetu kama kuna wavunja sheria wengine ambao anawaogopa basi hafai kabisa kuiongoza Tanzania.
 
Back
Top Bottom