Self employment opportunity in networking marketing business

Self employment opportunity in networking marketing business

Mr II

Senior Member
Joined
Feb 19, 2009
Posts
158
Reaction score
17
As the world is changing from Industrial age to information age where less and less people to be employed as the current trend is showing. A new opportunity is to learn how to employ yourself in the highly growing business of Networking Marketing.

This is an opportunity which many people don't see it because many people were not trained to identify opportunities in the traditional schools.

Come and employ your self, learn how to build your own business, prepared your true retirement plan and residual income and personal development not provided elsewhere.

For more information please contact +255 689 417 472/756 514 644/715 514 644
 
Self employment??? What kind of seif employment is this? Kuwasaidia wazungu kuuza bidhaa zao making us their dumping place? Lete mawazo yanatupelekea tuzalishe na kuexport siyo network marketing! Labda hizo bidhaa uzalishe ukiwa tz tuwauzie wazungu na siyo sisi tuwasaidie kuuza bidhaa zao! Lama kwenye traditional school hawakufundisha kujiajiri kwa hiyo kwenye modern school wanafundisha kuuza bidhaa za wanaojiita whitemen? Hamasisha uzalishaji was ndani tuwazie wao tukize uchumi, watu wajiajiri kwa kuzalisha siyo kuuza bidhaa za watu weupe tu!
 
Self employment??? What kind of seif employment is this? Kuwasaidia wazungu kuuza bidhaa zao making us their dumping place? Lete mawazo yanatupelekea tuzalishe na kuexport siyo network marketing! Labda hizo bidhaa uzalishe ukiwa tz tuwauzie wazungu na siyo sisi tuwasaidie kuuza bidhaa zao! Lama kwenye traditional school hawakufundisha kujiajiri kwa hiyo kwenye modern school wanafundisha kuuza bidhaa za wanaojiita whitemen? Hamasisha uzalishaji was ndani tuwazie wao tukize uchumi, watu wajiajiri kwa kuzalisha siyo kuuza bidhaa za watu weupe tu!

Kweli mkuu your right Mimi najiuliza why waafrica ni watu wakupokea tu kila kitu bila hata kufikiri, when will we stop being colonized by this white mens this forever living and there network marketing is shit
 
Ni kweli kabisa lakini tatizo siyo FLP. Natamani kama wanaojibu hapa wachukue muda na kusoma kidogo dunia inakotoka na kuelekea. Networking marketing ni mfumo tu wa kufanya biashara.hata ukiukataa sasa kwa bidhaa za FLP na makampuni mengine ya Mtandao (networking Marketing) utautumia tu kwenye bidhaa na huduma zingine. swali la kujiuliza ni kwamba utaukataa na kwenye bidhaa na huduma nyingine kwa vile huupendi kwa sababu zako?. Kwa taalifa yako hata makampuni mengine yamesha anza kuutumia. Mfano wa makamuni hayo hapa Tanzania ni makampuni ya simu kama Zantel na pia mengine kama Vodacom na Tigo yapo mbioni kuanza kuutumia mfumo huu kusambaza huduma zao. Swali la kujiuliza ni kwamba utakataa kutumia huduma zao kwa vile wanatumia mfumo wa networking marketing?by the way huu fumo hata wewe huwa unautumia mara nyingi bila kujijua. Maandiko matakatifu yanasema kuwa 'watu wangu wanapotea kwa kukosa maalifa' unaelewa maana yake?. huko ulikotoka ulikataliwa sana kama hapa. sababu kubwa watu wengi huwa hawapendi vitu vipya kwani wanapenda 'business as usual'. Naomba someni kidogo mjifunze kabla ya kuzungumzia kitu. Wewe acha watu watengeze vipato kwa kujiajiri. Huu mfumo kwa sasa unasaidia watu zaidi ya 2m hapa TZ kupata vipato vya ziada wewe unayepinga una taalifa hiyo? pia serikali ya TZ inapata kodi zaid ya 20bn kila mwaka, unajua hilo!,baada ya miaka 10 utajua makosa uliyofanya kwa kukataa mambo usiyojua na hukutaka kujifunza! nashauri watu wafanye tafiti kwanza ndipo wazungumze!
 
Well mi nataka kuanza kuuza asali kwa mtindo huo. Pia tambua kuwa matajiri wengi wa mlm sasa ivi tanzania wamewekeza pesa kwenye secta nyingne kama viwanda na real estate. Kama una masha zaidi whatsap me 0752 693 692
 
Hongera. WW unaesema unataka kuuza asali kwa mtindo huo mm nakusifu angalau na ww utakuwa mbunifu (innovative) kwa ss utakuwa umeanza kubadilika na kufuata dunia inakokwenda.Maana kuna watu hapa wanakataa tua na kusahau huu ni mfumo tu wakufanya biashara ambao hata mwenye biashara nyinge anaweza akautumia na kufaidika zaidi kuliko kuendelea kutumia mtindo wa kizamani wa kusubiri mteja aje ofisini kwako au kwenye duka au biashara yako. Mtindo mpya mfuate alipo na mwonyeshe huduma yako au bidhaa yako. na faida kubwa ya mfumo huu unafanya wateja wawe waaminifu kwa bidhaa na huduma kwani wanafaidika nayo kwa kugawiwa faida inayotokana biashara kuliko kuwa watumiaji wa huduma au walaji tu. Wataalamu wa biashara dunia wanasema ktk karne ya 21 makampuni na biashara nyingi zitaanza kuutumia mfumo huu. Mimi sishangai hali hii kwani nimesoma historia ya biashara hii, hata nchi zilizo endelea huko nako mfumo huu waliupinga?sababu ni kuto jua.Lakini mfumo umeendelea na watu wanaendelea kufaidika nao. Hata hivyo msishangae kesho au kesho kutwa mabenki, makampuni ya bima na huduma zingine wataanza kuutumia hapa TZ.kwa hiyo uamuzi ni wako mwenyewe kuamua kujifunza huu mfumo ufaidike nao au kuacha tu mambo yaende. lakini ukweli ni kwamba baada ya miaka 20 ijayo wengi wataujua na kuanza kuutumia. lakini swali ni kwamba utakuwa umepoteza kiasi gani kwa kuto kuutumia na kuongeza kipato? kuna mtaalamu mmoja wa falsalfa aliandika hivi 'A wise man makes his own decision while a fool follows other people's views!yaani mtu mwenye busara hufanya maamuzi yake mwenyewe na mpumbavu hufuta mawazo ya watu wengine. Wewe upo upande gani?
 
Katika dunia ya sasa every thing is possible kuwa muuzaji, mtengenezaji au msambazaji zote ni chaini lakini pia hela unsayoipata inaweza kuutoa uchumi ws nchi mfano ktk uwekezaj na ulipaji kodi. MLM unatakiwa uangalie ktk 3D. Mnyororo wake unafaidisha wangapi
 
'A wise man makes his own decision while a fool follows other people's views!

If i decide to follow your views and join your FLP im going to be a fool!!!!!!????
 
Ni kweli kwamba inatupasa tuzalishe wenyewe hizo products na kuziuza mpaka nje ya nchi, tatizo hatujafikia bado viwango vya kuzalisha bidhaa kama za FLP/GNLD, so meanwhile inatubidi tuwe tegemezi. ishu hapa usiitizame FLP/GNLD kama FLP/GNLD coz najua una Alergy nayo, tizama hizo products zao ni za viwango vya juu sn and thus why hata bei hua juu, its for only those who can afford it.So mkuu usiitizame sana kama njia ya kutengeneza kipato jali afya yako na ya wengine then kipato kitakuja tu chenyewe
 
Kama kuuza bidhaa za njee ni tatizo mbona hizo za kichina na zingine zilizo jaza masoko yetu hamwoni ni tatizo?. cha maana ni kwamba kama huna chako cha kuuza. tafuta njia uuze hata cha wenzako ili upate kipato. Kama mngejua kuwa bidhaa za nje zimefa watu wengi wajiajiriwengi msingekuwa na wasiwasi. Nilichogundua baada ya kuwa mjasiliamali ni kuwa shule tulizosoma zimetuhalibu sana kwa kuto na kanunu au theories ambazo hazifanyi kazi yaani theries and realities are quite different. Na nilipokuwa academician au shule nilifundishwa kuwa sababu kuwa ya umasilikini ni kuwa watu wamekosa fulsa! kumbe baadya kufanya mwenyewe nimegundua ukweli nikuwa wengi hatujafundiswa kutambua fulsa. kwa maana zimejaa kila kona katika nchi yetu lakini hatuzioni.na nikakumbuka mwandishi mmoja aliandika kuwa ' there is gold everywhere, but people are not trained to see it' yaani dhahabu au fulsa zimejaa kila mahali isipokuwa wengi hawajafundishwa kuziona au kuzitambua. Kwa bahati mbaya hao mnao waona wasomi ndio pengine vipofu wakubwa wa kutambua fulsa. na wengi elimu zetu huishia tunapomaliza vyuo. kumbe vyou vimefundi vitu vichache sana vingi vipo mtaani huko. na mwandishi mmoja alifafanua na kueleza kwa nini wasomi wengi sio matajiri na akasema kwa kuwa sababu ni nyingi ila kubwa ni kukosa financial education kwa shule zetu zinatufundisha kwenda kuajiriwa tu na sio kuajiri.Ushauli wangu kama kuna wasomi hapa tujaribu kusoma elimu ya ujasiliamali na ufanya kwa vitendo sio wa vitabuni.Dunia ijayo ni wajasiliamali na wanaotegemea kuajiliwa tu watakufa maskini!
 
Mr II Well sayed Kama humaanishi forever living, lakini kama unamaanisha hao sema nifute coment yangu
 
Last edited by a moderator:
hakuna kitu kibaya kama kugeuzwa waKala halafu unajiita umejiajiri wakati huna mchango wowote neither branding,standard setting na mengineyo mengi yanayo kuwa involve na product production
huwezi sema umejiajiri wakati siku supplier akikata supply huwezi endelea na supply.
 
Mchango upo labda tatizo ni uwezo wa kuchanganua mambo kama serikali inapata kodi na waliojiajili wanapata kipato kiliko wewe unaejidai umeajiliwa na kulipwa mshahara mdogo na kufanya kazi masaa mengi. Kama tatizo ni uwakala hizo bidhaa za kichina na zingine zilizo jamaa madukani hao wanaouza siyo mawakala? nadhani tunakosa uwezo wa kutathimini mambo.kama unaweza kuanzisha kiwanda wewe mwenyewe itakuwa bora. lakini nina ushahidi wa watu walioanza kama mawakala wakuuza bidhaa toka njee na wakajifunza na kuanzisha vyakwao. Kumbuka historia za viwanda zilianza hivyo. lazima uanzie mahali furani. mfano wachina na mataifa mengine machanga huwa nawanunu bidhaa na huiangalia na kuanza kuiga na kutengeneza. Wewe endelea na ajira yako na usijifunze ujasiliamali na usubiri kustaafu na hapo utaelewa kuwa pengine bora ungeanza miaka 10 iliyopita. Kama unafanya hizo biashara za kizamani za peke yako peke yako ujue dunia imebadilika, biashara za kisasa zinafanywa kwa team work or networks. Lakini nashauri muwe munasoma hata vitabu au mwingie kwenye mitandao mjue dunia inakokwenda!
 
Huu mfumo wanaotumia Forever, GNLD, nk ni mzuri katika kuuza ingawa napinga sana watu wa hizi kampuni kutuaminisha kwamba ukiingia tu huko unakuwa comfortable na utajiri. Kibaya zaidi wakati unaingia kuna products itabidi uzinunue. Uhuni mwingine wa hizi kampuni ni kuwa na tour za kuwadanganyia watu wao.
Binafsi nakubaliana kuwa mfumo wao wa kulipana kwa commission uko poa sana na kwa mfanyabiashara yeyote ni lazima kuuiga ili kuongeza mauzo.
 
Kinachoshangaza wanatumia nguvu nyingi sana, halafi kama kwa nguvu hivi. Kama hii biashara inalipa kwa haraK mpaka kupelekea mtu kutajirika kwa haraka, nadhani watu wengi sana wangejiunga na kupigiana mapende ili wa win zaidi.

Halafu pia ukiufutilia mlolongo wake ni kama inaweza kufika wakati watu wakaacha kujiunga ikawa kama Desi tu. Inaonekana inatumika nguvu kubwa sana kuwaingiza watu katika muundo huu biashara. Lakini naamini kazi yoyote nzuri hukimbiliwa na watu na wala sio hiyo kazi kutafuta watu.

Tujifunze sana ili kubaini prons na cons zake. Hasahasa haiwezi kuja kuishia kama desi pale products zao zikiingia mkenge kwa kuporomoka soko?
 
Back
Top Bottom