Selfika na JF: Snap it. Show it

Ngoja nichochee ugomvi , hayo ndiyo mambo ninayoyapendaga πŸ˜‚ πŸ˜‚

Labda wadada wa humu mliwahi kumkataa mwamba ndio maaana anatema moto mkali .

Nakumbuka enzi za shule tupo ghetto na machizi tulikuwa tunajadili Pisi Kali za shule na kuzithaminisha akatajwa demu mmoja Pele machizi wote kama 8 tulimsifia ni Pisi ila jamaa mmoja peke yake akawa anaabisha na kumkandia kinyama kuwa ni demu mbovu wakati huyo demu alikuwa Pisi πŸ”₯ πŸ”₯

Kila tukipiga stori za Pisi mwamba anamkamdia huyo demu mpk tukawa tunashangaa tukawa tunahisi labda mwamba ana chuki zake binafsi au alimtongoza akapigwa kisu kikali , tukimwambia mwamba Madai hayo alikuwa anaakataa anasema demu ni mbovu tu wakati akipite barabarani kila sehemu watu weweeeeeeeh kafungasha haswa si yuko portable na rangi sio poa !!πŸ˜‚πŸ˜‚

Mwisho wa siku tukagundua kwa taarifa za uhakika jamaa kumbe aliwahi kumtongoza akakataliwa vibaya mno ndio maana anachuki za kinyama kwa yule demu . Baada ya kugundua tulicheka sana tukawa kila tukimuona jamaa tunamcheka πŸ˜†
 
Hizi ballistic kama Iran ngoja nikufollow nipate update zaidi πŸ”₯πŸ˜‚!!

Nilichelewa sana kujua huu Uzi , siku hizi nitakuwa naweka bando kwa ajili ya huu uzi πŸ˜‚
 
Tunyooke kama rula πŸ˜† walionikataa waje waseme hapa waweke na chati zangu hapa wala mods wasiwahukumuπŸ˜†
 
Mimi nakupasha kama wakili wao..!!

Acha kushindana na watu wanaoingia period kila mwezi, au wewe ni anko T unataka kuchambana humu??
Sishindani na watu , wala sina shida na mtu, ni mada tu kama mada zingine ndio maana mods wanaziacha labda zinagusa tu ila sina nia ya kumtageti mtuπŸ˜†
 
Huo ndo ugonjwa wa min sasa 😹😹😹

Kila akianzisha uzi anaponda wadada wa selfika. Mpaka tunajiuliza min kuna mdada kamkataa humu?

Mwanaume rijali hawezi kuponda wanawake hata siku moja..!!
 
Sema nini….. Mi akili za wanaume baadhi huwa zinanichekesha sana.

Yall normalize bullying men, mtu akikujia lala nae kiulalo ulalo, Iweje mtu akubully umwache atambe? Wadada mnaowanyamazia wanaume ambao mna bifu nao mnawapa nguvu.

Mkiwa mnachat nao piemu wenzenu wanakusanya mafaili ninyi mna play safe, please play dirt kusanya risiti na wewe akikumwaga unamwaga na yeye akalilie kwao.

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Huo ndo ugonjwa wa min sasa 😹😹😹

Kila akianzisha uzi anaponda wadada wa selfika. Mpaka tunajiuliza min kuna mdada kamkataa humu?

Mwanaume rijali hawezi kuponda wanawake hata siku moja..!!
Hahaha sijaponda na nyuzi naziweka chitchat , na wapo wadada mpaka ndugu zangu humu , hivyo ni hisia zako tu.
 
Mimi nakupasha kama wakili wao..!!

Acha kushindana na watu wanaoingia period kila mwezi, au wewe ni anko T unataka kuchambana humu??
Mimi nimekoma kushindana na Wanawake humu nakumbuka Kuna siku nilijichanganya wewe Dada ulinichamba vibaya mno na kunitukana .

Kwa hasira nikakuanziashia Uzi wa MaLove kuwa nakupenda na nikaweka challenge kuwa hakuna mrembo Jf zaidi yako kama yupo aje , ukaja kwenye huo Uzi tena kunichamba na kunitukana mpaka nikawa nacheka mwenyewe nikaamua nikuache tu πŸ˜‚ πŸ˜† πŸ˜‚
 
Aki mmeanza kulewa mapema sana vijana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…