Seli za damu hazizalishi damu

Joined
Feb 10, 2013
Posts
15
Reaction score
0
NDUGU WANA JAMII, NISAIDIENI NIFANYEJE ILI NIPOMNE HILI TATIZO!

KIPINDI NIPO MDOGO, KABLA SIJAFIKISHA MIAKA 18, NILITOLEWA DAMU KTK HARAKATI ZA KUCHANGIA DAMU SALAMA, BILA KUJUA, NA KWA ELIMU NDOGO NILIYOPEWA NA WAHUSIKA SIKUWA NA UELEWA WOWOTE JUU YA KUTOA DAMU, VIGEZO NA MAHITAJI MENGINE.HAYA YALITOKEA NIKIWA SHULE

KIUFUPI SIKUWA NA VIGEZO VYA KUTOA DAMU KWASABABU NILIKUWA BADO MDOGO, DAMU YANGU ILIKUWA HAITOSHI. NA HATA KILO ZANGU ZILIKUWA PUNGUFU. MAPEMA BAADA YA KUTOLEWA DAMU, NILIKOSA NGUVU, NA NIKAWA NAUGUA SANA IKIWEMO KUPUNGUKIWA DAMU, NILIPIMA KTK HOSPITALI MOJA KUBWA HAPA NCHINI, KWA MSAADA WA MADKARI WA NJE. MAJIBU WALIYONIPA NI KUWA MWILI WANGU HAUWEZI KUZALISHA DAMU, SELI ZANGU ZA DAMU ZIME COLLAPSE, HAZIWEZI KUZALISHA DAMU YA KUTOSHA MWILINI.

NINA MIAKA MITANO SASA NA TATIZO HILI, NA MSAADA NINAOPATA TOKA KWA MADKTARI NI KUZISHITUA SELI ANGALAU ZIWEZE KUZALISHA KIASI KIDOGO CHA DAMU( WAO KITAALAMU WAMENAMBIA INAITWA REFRESHMENT), NA NIMESHAFANYIWA MARA MBILI, AMBAPO DAMU YANGU HUSAFISHWA NA KURUDISHWA MWILINI. NA PIA HUWA NATUMIA VIDONGE KUMEZA KWA AWAMU, AMBAVYO VINAUZWA GHARAMA SANA, WAKATI MWINGINE NAISHIA KUNYWA JUICE YA REBENA NA ROZELA KWA WINGI BILA MAFANIKIO. SIRUHUSIWI KUONGEZWA DAMU YA MTU YEYOTE AU KUTOA DAMU.

HALI HII INANISABABISHIA KUUMWA NA KICHWA SANA KUPITA KIASI, NA WAKATI MWINGINE HOMA NDOGO NDOGO HUPELEKEA MATATIZO MAKUBWA IKIWEMO B.P KUSHUKA.

NAHISI KIFO KINANIKABILI, NAOMBENI MTU YEYOTE MWENYE MSAADA WA NAMNA YA KULIMALIZA TATIZO HILI ANISHAURI, NIFANYE NINI, NITUMIE NINI(HASA KAMA KUNA VIRUTUBISHO ASILIA) KTK KUNUSURU UHAI WANGU.

NAOMBA TUWASILIANE KUPITIA kyakukumyensa@gmail.com

MUNGU AWABARIKI SANA.
 
Mimi ni Dr ila maelezo yako sijakuelewa, kwa hiyo tatizo linalokusumbua ni nini, ulipopima damu yaani hb huwa inakuwa ngapi, na express nini hasa kinkusumbua yaani dalili au kama maumivu n.k ili tujue diagnosis ni ipi.
 
Nimepita kukupa pole kwa tatizo lako. Naamini hapa JF utapata ushauri utakao saidia kupata nafuu ya kudumu au kupona kabisa. Nimeguswa sana na habari ya tatizo lako, zaidi MUNGU akupe moyo wa subira na akufanyie wepesi ktk kupata msaada. Pole sana Ndugu!
 
mimi ni dr ila maelezo yako sijakuelewa, kwa hiyo tatizo linalokusumbua ni nini, ulipopima damu yaani hb huwa inakuwa ngapi, na express nini hasa kinkusumbua yaani dalili au kama maumivu n.k ili tujue diagnosis ni ipi.

asante sana dr. Kwa sasa nina miaka zaidi ya mitano nasumbuliwa na upungufu wa damu,(wakati nipo mdogo niliwahi pata tatizo pia la damu wakati wananiongezea wakafanya makosa kidaktari hewa ikaingia ikasababisha kuwepo kwa gap, na hilo gap ndo linapelekea seli zisizalishe damu- hicho ndoo kiini cha tatizo-nashindwa kukuelezea kitaalamu kwa sababu sii taaluma yangu, ila ndhani utanielewa.) kama nilivyokueleza kueleza mwanzo, niliwahi kutoa damu nikiwa mdogo, na wazazi waliwahi shauriwa na daktari nisitoe damu, hawakunitaarifu, hapo ndipo tatizo likaongezeka, na hii ni kwa sababu nilikuwa na damu kidogo(maelezo ya dr. Kwa wazazi wangu), baada ya kutoa damu tu tatizo likawa kubwa, na dr. Akanambia kuwa seli zangu za damu haziwezi kuzalisha damu, na nahitajika niendelee kufanyiwa refreshment ya damu mpaka seli zitakapoanza kuzalisha damu. Dr. Amezuia nisiongezwe damu ya mtu yeyote. Ni miaka zaidi ya 8 sasa, sijaona mafanikio yoyote.(maelezo haya huwa napewa na wazazi wangu na daktari anayenisaidiaga kusogeza siku zangu)

matatizo ninayoyapata ni
1. Kuumwa kichwa sana kupita kiasi
2. Kizunguzungu
3. Kuchoka sana
4. Na wakati mwingine sijisikii kula kabisa
5. Kuwashwa sana mwili mzima
6. Matatizo ya hedhi kubadilika muda wake, na wakati mwingine sipati kabisa
7. Damu nilipima mara ya mwisho ilikuwa 23

matatizo haya hutokea kwa awamu, wakati mwingine nakuwa mzima kabisa, ila inafikia wakati nashindwa hata kusimama

asante sana
 
Mkuu, mimi pia ni daktari kwa taaluma, ila maelezo yako yananipa maswali zaidi kuliko majibu..........
Swali la kwanza, hapo kwenye nyekundu, sijaelewa kabisa...... kwa sababu seli za damu zinatengenezwa kwenye bone marrow(uboho wa mfupa), na sio kutoka katika seli za damu, labda useme kwamba bone marrow inatengeneza abnormal cells ambazo haziwezi ku-divide vizuri, na je ni seli zote za damu zimeathirika?maana kuna seli nyekundu, nyeupe na chembe sahani,na zote ni seli za damu,kama utaweza kunijibu hili itanisaidia kujua ugonjwa wako
Kwenye blue hapo-sijawahi kusikia kitu kama hicho in my carrier as a doctor...... are you sure ndo inaitwa hivyo? na ilifanyika wapi? hapa hapa bongo?kama ni bongo ilikuwa ni muhimbili?
kwenye green-je unakumbuka jina la hiyo dawa??inaweza kunipa clue ya ugonjwa wako....
kwenye yellow-kama shida ni kwenye seli za damu, hata unywe rozella kiasi gani haisaidii...... unazidi kunichanganya kwa kweli kujua shida ni nini, ulishauriwa ivo na daktari?
natamani kukusaidia ila thread yako inaniachia maswali zaidi nashindwa hata pa kuanzia kaka
 
Dah...... hapo kwenye nyekundu umeniacha kabisa............. sijaelewa kabisa hiyo mechanism ya tatizo....... kitaalamu nashindwa ku-grasp kilichosemwa hapo, labda my colleague Muciprocin@ atakuwa ameelewa.....
hapo kwenye green-hizo symptoms zote ulizozitaja ni kwa sababu ya upungufu wa damu-anaemia- na hazitusaidia kujua kisababishi za tatizo lako!!!
Na hiyo damu ya 23 ilikuwa katika unit gani?? is it gram per liter or gram per deciliter?(i know unaweza usijue ilikuwa kwenye units gani)...... ila usipotaja units tunashindwa kuelewa kama ulikuwa na upungufu wa damu au la
 
Last edited by a moderator:
mkuu, mimi pia ni daktari kwa taaluma, ila maelezo yako yananipa maswali zaidi kuliko majibu..........
Swali la kwanza, hapo kwenye nyekundu, sijaelewa kabisa...... Kwa sababu seli za damu zinatengenezwa kwenye bone marrow(uboho w

asante dr. Kupata maswali zaidi ni mwanzo wa kupata suluhu. Kiukweliu ni vigumu kunielewa, ila hayo ndio maelezo ninayopewa na wazazi pamoja na daktari ambaye huwa anashughulikia tatizo langu. Kiutaalamu kwa kweli siwezi kukudanganya,sijui inatakiwa itajwe/itolewe maelezo vipi, ila ndivyo nilivyoambiwa, pengine kwa kuwa ni taaluma yako waweza niambia vizuri nini hufanyika ktk mfumo huo, kikubwa ni mimi kuweza kupata damu ya kutosha mwilini na matatizo niliyoorodhesha hapo juu yakaisha.

Nimeshafanyiwa hiyo refreshment(kama wanavyoiita) mara tatu sasa, na natakiwa kila baada ya miaka mi 3 nifanyiwe hivyo, ni kwamba process hiyo huwa ni kama nakatwa fahamu kabisa, damu inasafishwa na baadae naendelea na life yangu. Ina kera sana ndugu yangu na inachosha sana, kwa sababu sioni matumaini yoyote.

Baada ya hiyo process huwa natumia dawa inayoitwa aerometrophine ambayo niliambiwa inasaidia kuzalisha hiyo damu kwa kiasi.

Lakini dr. Hali inazidi kuwa ngumu kwangu. Mbaya zaidi nimeambiwa kuwa sitaweza hata kubeba mimba kwa siku tisini ikitokea napata mimba sasa hivi kwa sababu sina damu ya kutosha na mwili wangu hauzalishi damu. Nifanyeje?

Asante.
 
mleta thread napenda upitie thread inayoelezea ...jinsi ya kujieleza kwa daktari.
Nahisi kama maelezo yako yamekaa kihadith hadith hivi.
Hata mimi ni Dr lakini sijakuelewa.
 

Dr mimi mwenyewe napata shida kumuelewa huyu pt wetu, lakini nafikiri tutamwelewa tu. Hapo anapozungumzia hewa nahisi anazungumzia air buble ambapo nilitegemea apate air embolism na hii hutokea very rare, katika carrier yangu sijawahi ona air embolism. Na hizi symptoms kwa kweli ni za anemia tu, lakini kwa hiyo Hb iko chini sana huyu atakuja kuishia kwenye heart failure. Sasa Dr nafikiri tumshauri hivi amwone haematologist pale Muhimbili kama yupo Dar, au akuone wewe ingawa sijui ulipo ila waweza mwelekeza. Mimi nipo mkoa wa Ruvuma. Fanya utakaloweza coz tatizo lako linahitaji face to face discussion
 
Last edited by a moderator:

DAWA HIYO INAITWA aerometrophine

HICHO KITENDO WAKATI MWINGINE WANAKIITA BLOOD CIRCULATION, ILA HUWA WANAITOA DAMU YANGU YOTE NA WANAIRUDISHA IKIWA WAMEISAFISHA (SIJUI KITENDO KINAITWAJE KWA KWELI), NA HUWA SINA FAHAMU KWA WAKATI HUO, NA MARA NYINGI HUWA HAWAPO TAYARI KUNIELEZA KINACHOTOKEAGA.

HIYO HOSPITALI MIPO HAPA TANZANIA, NA NI YA SERIKALI, NAOMBA NISIITAJE JINA, ILA IPO KANDA YA KASKAZINI
.
 
hebu niambie wewe uko wapi?? kama uko pande za kaskazini hebu fanya utaratibu tuwasiliane ili tuonane kwa msaada zaidi, maana nahisi kwa maelezo ya kwenye keyboard hatuelewani....... you need face to face to face consultation, au kama upo dar ni vizuri zaidi nikuunganishe kwa haematologist hapo muhimbili akuone
 
Dada yangu maelezo yako unayopewa na madaktari na matibabu unayopewa sijawahi kuyasikia i medical practise. May be i need to go back to my notes and researches ila nahisi huwa wanakufariji tu. Unahitaji kwenda hospitali ya rufaa au ya mkoa na kuwaambia kabisa unataka kuonana na either specialist wa hematology au internal medicine. Nina wasi wasi wasi na utaalamu wa huyo daktari anayekutibu.!
 

23 gram/ decilitor
 

asante dr.
 

NIPO KANDA YA KATI, SINGIDA, ILA KAMA UTAKUWA TAYARI KUNISAIDIA NAWEZA KUKUTAFUTA ULIPO, TAFADHALI NIJULISHE UNAPATIKANA HOSPITALI GANI, NA NAMNA YA KUKUPATA DR. kyakukumyensa@gmail.com
 
NIPO KANDA YA KATI, SINGIDA, ILA KAMA UTAKUWA TAYARI KUNISAIDIA NAWEZA KUKUTAFUTA ULIPO, TAFADHALI NIJULISHE UNAPATIKANA HOSPITALI GANI, NA NAMNA YA KUKUPATA DR. kyakukumyensa@gmail.com

duh! Mkuu singida x ray ni anasa kwa wagonjwa ndo kuna hiyo machine ya kushtua celi za damu(japokuwa sijawahi kukisikia)? Hii ni hatari! Am sorry kuna vitu siwezi kuongea hapa for the sake of my senior or junior coligi.
 
jamani madokta msaidieni.kiukweli namuonea huruma.mambo ya sijui kusafishwa kama si uzima huo,ni vizuri ipatikane tiba kabisa.mleta mada usichoke kuhangaika ipo siku utapona tu.na vile vile jaribu ku google ili upate information zaidi
 
Asanteni sana madaktari wetu.
Pole sana mgonjwa.
 
Asanteni sana madaktari wetu.
Pole sana mgonjwa.

watanzania wengi wanaangamia kwa kutopata ushauri kutoka kwa watu sahihi. Hii inatokana na serikali kushindwa kuboresha mazingira ya kazi kwenye hospitali za umma ili wahudumu sahihi wawepo mahali hapo. Kwani watu wengi wanakimbilia mjini kwa kuogopa kwenda kuwa kama waganga wa kienyeji huko wilayani. Vipimo vingi vya muhimu kama xray,fbp, rbg, rft, lft vimekuwa kama anasa kwa wagonjwa wa kitanzania wakati ni vipimo vya mwanzo tu ili kujua tatizo la mgonjwa. Tunahitaji kuendelea kuishinikiza serikali kuangalia upya aina ya huduma wanazopewa watanzania.
 
Nyalotsi hayo yote ni ukweli
je utaendelea kuwapigia kura hao hao?

 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…