Sema Kweli Hata Kama Watu Wataipuuza Au Kuikataa

Sema Kweli Hata Kama Watu Wataipuuza Au Kuikataa

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,237
Reaction score
1,744
Eze 2:7 SUV
[7] Nawe utawaambia maneno yangu, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana.

Agizo alililopewa nabii Ezekieli ni kusema na Israeli waliokuwa wanaasi na walio wagumu wa mioyo. Kazi yake ilikuwa kuhakikisha ujumbe wa Mungu unawafikia watu hawa, bila kujalisha watasikia na kuchukua hatua ya kutoka katika eneo lisilo sahihi au watabaki hapohapo.

Kazi ya mjumbe wa Mungu au mtumishi wa Mungu ni kusema neno la Mungu, ule ujumbe wa Mungu aliopewa kupitia neno anapaswa kuusema waziwazi bila kuwa na shaka yeyote.

Ujumbe wa Mungu hupaswi kupotoshwa, bila kujalisha kupokelewa kwake ni ngumu, unapaswa kutolewa ulivyo, ndio hupaswi kupindishwa kwa sababu yeyote ile.

Msemaji wa Mungu anapaswa kumsikiliza Mungu zaidi na sio mazingira yao na watu wao wanaoipinga kweli au kuikataa, akifanya lile jukumu alilopewa na Mungu atampendeza.

Tofauti na mjumbe mwingine wa Mungu anaweza kuhangaika kuwapendeza wanadamu na si yule aliyemtuma, jambo ambalo linakuwa gumu sana.

Ujumbe wa Mungu huhitaji waoga, unapaswa kutangazwa na watu jasiri, na ujasiri hauji wenyewe unahitaji kujaa neno la Mungu ndani yako na kujazwa na Roho Mtakatifu.

Kutangaza kweli sio kana kwamba ni hiari, ni agizo la Mungu kwa kila mtumishi wake, kile anakuagiza unapaswa kukifanya vilevile.

2 Tim 4:2-4 SUV
[2] lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. [3] Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; [4] nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
Kazi ya mjumbe wa Mungu ni kupanda na kumwagilia, kazi ya kuotesha kilichopandwa ni Mungu mwenyewe, neno la Mungu linapaswa kupandwa kwa wingi kwa watu, matokeo ya kuotesha hilo neno ni ya Mungu mwenyewe.

1 Kor 3:6-7 SUV
[6] Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. [7] Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.
Jukumu la mtumishi au mjumbe wa Mungu ni kusema, na si kulazimisha watu wasikie, anapaswa kupaza sauti yake kwa watu, wasikie au wasisikie sio wajibu wake, wajibu wake ni kusema mbele yao wasikie.

Tunajua upinzani upo katika kusema ule ujumbe wa Mungu, lakini unapaswa kukumbuka hata Yesu mwenyewe alikutana na upinzani wa namna hiyo.

Mt 23:37 SUV
[37] Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!
Pamoja na upinzani mkali, tunaona wazi Yesu alitimiza kusudi la kutangaza Ufalme wa Mungu, hakuangalia upinzani, aliangalia jukumu alilokuwa nalo kwa ulimwengu.

Tangaza kweli ya Mungu siku zote bila kupunguza chochote, bila kujalisha watu hawataki kukusikia kile unasema, hilo sio jukumu lako la kuwalazimisha wakusikie na kukufuata. Mengine mwachie Mungu, kazi yako ni kufikisha ujumbe wake.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari neno
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Back
Top Bottom