uandishi wako umejaa Story zisizo na umuhimu katika marketing na lugha isiyoeleweka kwa wanunuzi. pia kuandika kiswanglish. bora basi andika kiswahili na tafsiri kwa english. hapo mwanzo nimeangalia sioni sembe au hiyo njano ndo sembe?
View attachment 560260
Hii storage system hapo chini tafadhari usiioneshe kwa wateja, hata magunia ya dagaa hayapangwi hivyo sembuse unga wa kula bila kuosha. umesema una vibali vya TBS na TFDA sidhani kama hata bwana afya wa halmashauri walitembelea godown lako wakakuta umepanga hivyo na wakakupa kibali. Ngoja nieendelee kuchungulia pengine ntaiona nembo ya TBS.
Hivi kweli hujui kuwa roba kukaa sakafuni na kugusa ukuta linapenyeza unyevunyevu unaosababisha kupungua ubora wa bidhaa na kupelekea kuishi wadudu hata sumu kuvu??
View attachment 560257
Unrelated issues. Kama unafadhili timu au kama wafanyakazi wako ndio wanatimu, nadhan haya na mambo yote yanahusu kujitolea katika jamii yakae kwenye sehemu maalumu ya "CSR'' tafuta kiswahili chake.
Nembo iliyoko kwenye mifuko ya unga haionekani popote kwenye website na hivyo kuleta hisia kuwa aliyetengeneza mfuko alijiwekea yeye ama aliyetengeneza website hakujiongeza kuweka nembo ya kampuni.
View attachment 560259
MWISHO;
Wazo la kuwa na website lilikuwa zuri lakini aliyetengeneza hana uzoefu na hajiongezi.