SEN: Fursa hii mlangoni, tunajitambulisha kwenu kama Taasisi

SongambeleEN

Member
Joined
Mar 23, 2013
Posts
25
Reaction score
12
Hodi hodi Wanajamvi
Kama ilivyo jadi yetu, si busara kukaribia jamvini kabla hujakaribishwa, na ndio maana sisi kama SEN tumeamua kuja kugonga mlango kwanza.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana na kushirikiana nanyi katika mtandao huu wa kijamii- Jamii Forums -"The Home of Great Thinkers"-. Sisi kama SEN (Songambele Entrepreneurial Network) tutakuwa tunashirikiana nanyi katika mambo yote yanayohusiana na biashara pamoja na ujasiriamali.

SEN ni taasisi isiyo ya kiserikali inayoendeshwa na mtandao wa wanachama wake ambao wengi wao ni wafanyabiashara, wajasiriamali (wanaochipukia na wenye shughuli zao), wataalamu wa fedha, sera, TEKNOHAMA na ujasiriamali. Mtandao huu hauna ushirika na chama chochote cha siasa bali wanachama wetu wanavyama vyao na hilo hatulikatazi. Hii inatokana na ukweli kwamba tofauti zao za kiitikadi hazihusiani na malengo yetu ya kuwawezesha wanachama wetu kujikwamua katika lindi la umasikini kwa kutumia mbinu za kijasiriamali

Ujasiriamali ndio dhana mpya na ni vyema kila mtu akaanza kuitathmini dhana hiyo na kujitathmini binafsi juu ya Ujasiriamali. Hii inatokana na ukweli kwamba nyakati zimebadilika na ujasiriamali ndio njia iliyo sahihi zaidi kama mtu anatamani mafanikio ya kweli maishani.

Aksanteni, na tunawatakia weekend njema
SEN - "nurturing ideas, empowering entrepreneurs"-

Unaweza kutufuatilia kwenye twitter kupitia link hii http://twitter.com/SongambeleEN
 
They call it JF, we call it Home. Karibu sana SEN.
Binafsi nimevutiwa sana na huduma mnazozitoa japo bado hamjawa specific; Ninaomba muwe specific, ni huduma gani haswa mnazozitoa na ni kwa sehemu gani? Kama nimewaelewa vizuri mmesema huu ni mtandao wa wanachama, je ni vigezo gani vinavyotumika kuwapata hao wanachama?
 
Back
Top Bottom