KIFO CHA MUTULA KILONZO SASA NI KILELE CHA UTITIRI WA VIFO TANGU 'SHAHIDI MWANAKIJIJI' HADI 'WAZIRI WA HAKI NA KATIBA' WALIOPATA AMA KUGUSA AU KUGUSWA NA KESI ZA ICC
Nilipata kumfahamu Mutula Kilonzo kama mwanasheria shupavu aliyependa sana kusema ukweli hata nani awe amesimama mbele yake.
Wakati huo huo alikua ni mwanasiasa machachari lakini mwenye nidhamu ya hali ya juu kwa viongozi wake ama wa chama au serikali alimradi tu hkuna yeyote atakaekua amevuka mistari yake mekundu (set of own distinguishing principles) aliyojiwekea katika maisha yake.
Yote juu ya yote, kiongozi huyu aliyepata kushika sana mafaili ya ICC kutokana na wadhifa aliokua nao, Mutula Kilonzo hakuondoka kwa kupenda sana katika wizara hiyo inayoendana na taaluma yake ya sheria aliyoisomea hapa hapa UDSM ila ilibidi ahmie Wizara ya Elimu ambamo ametumikia hadi mauti ilipompata.
Kule katika wizara ya mwanzo kidogo msimamo wake ulionekana kuwa ni mkali kupindukia kwa kuonyesha kiu ya hali ya juu kutaka kuona waathirika wa machafuko ya 2007 wanapata haki bila kujali kabila wanakotoka.
Kwa wale waliopata kumfahamu Mutula Kilonzo na asivyoambilika kitu chochote kile when it comes to DEFENDING JUSTICE, they would unanimously nod in approval that it is exactly this type of uncompromisable stance that largely formed the bottomline that eloquently defined his person and professionalistic conservatism throughout his life as a distinguished attorney.
Hakika namlilia Mutula Kilonzo huku nikisema sala za kheri kwake na pumziko ya milele umjalie e Bwana; Amina.