Kigaila Mwandishi
New Member
- Sep 23, 2022
- 2
- 0
Mgombea wa nafasi ya MNEC toka mkoa wa Arusha, mfanyabiashara wa madini Ndugu, Gabriel Sendeu baada ya kuona nguvu yake ya fedha haiwezi kumsaidia kushinda nafasi hiyo amechagua kutumia ukabila kutafuta kura kwa wajumbe.
Sendeu Laizer siku ya juzi akiwa kwenye kikao na timu yake ikiongozwa na Mbunge wa zamani na Mwenyekiti wa CCM mstaafu mzee Lekule Laizer, Mbunge aliyechaguliwa juzi wa bunge la Afrika Mashariki, James Millya na wajumbe wengine kutoka Arusha akiwemo Mwenezi wa Arusha mjini Ndugu Anthony Maswi.
Kwenye kikao hicho walikubaliana kuwa ili kushinda uchaguzi huu wanahitaji kutumia zaidi siasa za ukabila kwasababu Mgombea wao ni mmasai na kundi kubwa la Wajumbe ni wamasai.
Hivyo watumie hoja hiyo ili kuweza kuwashinda wapinzani wao wakubwa ambao ni pamoja na MNEC anayetetea kiti chake, Mhe Daniel Pallangyo na Mgombea mpya anayeonekana kuwa na nguvu ya ushawishi aitwaye Gesso Bajuta.
Na katika hoja zao zingine wanasema kuwa Mgombea wao Ndugu Sendeu Laizer hajui siasa na wala hana uwezo wa ushawishi kwa wajumbe.
Na hata mjumbe mmoja kutoka Longido akasema kuwa Ndugu Sendeu amekuwa ni mtu mbinafsi sana ambaye hata akiwa kwenye Kata yake ya Mundarara na hata Longido ni mtu ambaye hana msaada kwa watu hata kutoa salamu kwake ni changamoto hivyo watafute namna ya kutengeneza hilo lisije likatumiwa na wapinzani wake.
Hoja hii wanayotaka kuileta ya Ukabila ingekuwa na nguvu kwa nafasi zingine zilizogombewa hata Mhe James Millya asingepata nafasi ya kuwakilisha Nchi katika bunge la Afrika Mashariki hivyo yeye kama Kiongozi anayewakilisha Nchi alipaswa kuunganisha Watu na sio kutengeneza utengano kati yao,na kama akiendelea kutengeneza utengano huu inaonyesha wazi kuwa hatoshi kuwakilisha Nchi kwenye Bunge la Afrika Mashariki.
Ukabila huu pia ungekuwa unasaidia Ndugu Anthony Maswi asingepata nafasi ya Uenezi Mkoa wa Arusha.
Jambo kubwa kuliko yote anayetafuta sio Laigwanan au Kiongozi wa Wamasai ila anatafuta MNEC wa mkoa wa Arusha atakayewawakilisha WanaArusha kwa ujumla wao na sio kabila moja.
Hayati Mwalimu Nyerere alishawahi kusema Kiongozi yeyote atakayetumia Ukabila au Udini hafai kuwa Kiongozi hata wa familia yake hivyo hata hawa wanaotumia hoja ya Ukabila hawafai kuwa Viongozi wa Chama hiki.