Senegal bila Mane ni kama Simba bila Chama

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Niliongea kauli hii mapema leo kijiweni nikabezwa na kutupiwa maneno ya ukali, huku Watanzania wenzangu wakijigamba kuwa Senegal ni moto wa kuotea mbali bila hata ya Mane kuwapo.

Wakati wa mchezo wa Iran na Uingereza nikarudia tena kauli yangu na nikawatahadharisha kuwa mpira Duniani umegawanyika katika makundi matano ki uwezo;
1)Mpira wa Ulaya
2)Mpira wa America ya Kusini
3)Mpira wa Asia
4)Mpira wa Waarabu
5)Mpira wa Afrika

Ni vigumu au si rahisi sana kutoboa nyie wa kundi la chini kumshinda aliyeko kundi la juu yako, labda kwa yale makundi mawili ya juu lakini kwa yaliyobaki kiukweli bado kuna kazi kubwa ya kufanya.

Wenzetu walitutangulia mapema katika uwekezaji na pia walisaidiwa sana na hali zao za ki uchumi, lakini tujipe moyo tufurahie michuano hii ya Quatar 2022, lakini kusema nchi moja wapo ya Afrika kufika hata nusu fainali ni ndoto.

Afrika tuwekeze kwenye mchezo wa kandanda tukianzia na kuwajenga watoto wakiwa wadogo kwenye utamaduni mzima wa kandanda, tulete wakufunzi toka nchi tofauti zilizopiga hatua waje kufanya mafunzo ya muda mrefu tuzalishe vizazi na vizazi vyw wachezaji bora.

Kikubwa Mungu ametujaalia vipaji vya ukweli Waafrika, ni sisi tu kuviendeleza. Tuache rushwa na kupunguza siasa, vita vya wenyewe kwa wenyewe n.k, siku moja tutashinda.

Mungu ibariki Afrika.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Ni yanga bila feisal..hv ushawahi imagine yanga bila feisal mpaka sahizi yanga wangekuwa wamepoteza mechi na azam na hii wangetoa draw na kmc na kagera pia..??ombeni sana wale matajiri wa chamanzi wasifanikiwe kuvunja mkataba wamchukue,mtapata tabu sana.
 
Senegal pale wanawachezaji wazuri tuu tena kutoka club kubwa ulaya , shida ni " makosa ya kiafricka"
 
Well said

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo hapa ndo umekubali kuwa Simba bila Chama haiwezi, au ndo umekana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…