Senegal: Boti iliyobeba Wahamiaji 200 yapotea kwenye maji

Senegal: Boti iliyobeba Wahamiaji 200 yapotea kwenye maji

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Waokoaji wa Uhispania wanaendelea na msako wa mashua hiyo karibu na Visiwa vya Canary ambapo inadaiwa haijulikani ilipo tangu ilipoanza safari zaidi ya wiki moja iliyopita.

Kundi la misaada la Walking Borders linasema boti hiyo ya wavuvi ilisafiri kutoka Mji wa Kafountine, Kusini mwa Senegal uliopo kilomita 1,700 kutoka Tenerife, ikidaiwa pia ilikuwa imebeba Kundi la Watoto kadhaa.

Wakati huohuo, boti nyingine mbili zilizobeba watu 65 na 60 nazo zinadaiwa kupoteza kwenye maji hivyo kufanya idadi ya watu ambao hawajulikani walipo ndani ya wiki moja kuwa zaidi ya 325.

#########

Migrant boat from Senegal carrying 200 people missing off Canary Islands

Spanish rescuers are searching waters off the Canary Islands for a boat carrying at least 200 African migrants who went missing more than a week ago.

The aid group Walking Borders says the fishing boat sailed from Kafountine, a coastal town in southern Senegal that is roughly 1,700km (1,057 miles) from Tenerife.

The group says many children are on board, Spain's Efe news agency reports.

Two similar boats carrying dozens more people are also said to be missing.

The boat carrying about 200 people left Kafountine on 27 June, heading for the Canary Islands.

Spain's maritime rescue service told Efe that a plane had joined the search.

There are few details about the other two boats. Reuters news agency quoted Helena Maleno of Walking Borders as saying that one has about 65 people on board, the other up to 60, which would bring the total number of people missing across the three boats to more than 300.

The news comes just weeks after Europe saw one of its worst Mediterranean migrant shipwrecks, when an overcrowded trawler sank off the Greek coast.

At least 78 people were confirmed drowned, but the UN reported that up to 500 were still missing.

The voyage from West Africa to the Canary Islands is among the most dangerous routes for migrants, not least because they usually sail in simple dugout fishing boats that are easily tossed by powerful Atlantic currents.

Last year at least 559 people died at sea attempting to reach the Spanish islands, the UN's International Organisation for Migration (IOM) says. The death toll for 2021 was 1,126.

The IOM quotes Spain's Interior Ministry as saying 15,682 people arrived irregularly in the Canary Islands in 2022, a decrease of 30% compared to 2021.

"Despite the year-to-year decrease, flows along this dangerous route since 2020 remain high compared to prior years," the IOM says.

Source: BBC
 
Sisi tulilaniwa vibaya sana...angalia tulivyohangaika na kile chombo na angalia watu 300 na kitu wameshakufa hao na hatujali
 
Sisi tulilaniwa vibaya sana...angalia tulivyohangaika na kile chombo na angalia watu 300 na kitu wameshakufa hao na hatujali
Halafu zitaibuka nchi za kiafrika na kuanza kulaani nchi za ulaya kwamba hazikufanya jitihada za kutosha kuwaokoa watu wao.
 
Hao waopoaji wa spain nadhani wakiwakuta hai wanawalamba shaba. Mani anataka wahamiaji haram nchini kwake?
Kama Lampadusa walikuwa wanatoboa chini wazame

Utumwa unauzwa huu wa sasa unajiuza
 
Halafu zitaibuka nchi za kiafrika na kuanza kulaani nchi za ulaya kwamba hazikufanya jitihada za kutosha kuwaokoa watu wao.
Waafrika na viongozi wao kama Museveni hawajawahi kuwa na akili, wao wanachojua ni matumizi ya maguvu tu.
 
Wahamiaji 300 watoweka baharini.jpg

Muktasari:​

  • Waokoaji nchini Hispania wanaendelea kutafuta boti tatu zilizotoweka katika bahari ya Atlantiki karibu na Pwani ya Afrika Magharibi waliokuwa wanatoka nchini Senegal zikiwa na zaidi ya watu 300.
Hispania. Zaidi ya watu 300 waliokuwa wakisafiri kwa boti tatu za wahamiaji kutoka Senegal kwenda visiwa vya Canary nchini Hispania wamedaiwa kutoweka.

Kwa mujibu wa shirika la misaada la wahamiaji la Walking Borders la Hispani liliripoti tukio hilo la kutoweka jana Jumapili, Julai 9, 2023.

Shirika la Habari la Reuters, lilisema boti mbili za mwanzo ziliondoka nchini Senegal siku 15 zilizopita moja ikiwa na takriban watu 65 na nyingine ikiwa na watu kati ya 50 na 60.

Boti ya tatu iliondoka nchini humo Juni 27 ikiwa na takriban watu 200 ambapo jumla ni zaidi ya watu 300 ambao inataarifiwa wamepotea wakijaribu kufika nchini Uhispania.

Ofisa wa shirika la misaada la wahamiaji la Walking Borders la nchini humo, Helena Maleno alisema boti zote tatu ziliondoka mji wa pwani uitwao Kafountine kusini mwa Senegal, ambayo ni takriban kilomita 1,700 (maili 1,057) kutoka Tenerife, moja ya visiwa vya Canary.

"Familia zina wasiwasi mkubwa. Kuna takribani watu 300 kutoka eneo moja la Senegal. Wameondoka kwa sababu ya kukosekana kwa utulivu nchini humo," alisema Maleno.

Inaelezwa visiwa vya Canary vilivyoko nchini Hispania ambapo ni karibu na Afrika Magharibi vimekuwa kivutio kikubwa cha wahamiaji wanaojaribu kufika nchini humo.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), takribani wahamiaji 559 walifariki dunia baharini mwaka jana wakijaribu kufika visiwa vya Hispania.

Shirika hilo linasema kwa mwaka 2021 idadi ya vifo ilikuwa watu 1,126.

chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom