Senegal imeapa kukata rufaa ya uamuzi wa CAF kuwapoka ubingwa wa AFCON 2025

Senegal imeapa kukata rufaa ya uamuzi wa CAF kuwapoka ubingwa wa AFCON 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) limethibitisha kupokea uamuzi uliotolewa na Kamati ya Rufaa ya CAF kuhusu kupokwa ubingwa wa Kombe la Mataifa la Afrika 2025

1773814545688.png
FSF imepinga rasmi uamuzi huo ambao wanaona hauna msingi wa kisheria, upo kiholela na hauna uwiano.

FSF inaamini kuna Ukiukaji mkubwa wa kanuni za kifungu cha 82 na 84 cha kanuni za CAF zilizohalalisha maamuzi hayo

FSF imeeleza kuwa mwamuzi wa mechi hiyo alitumia uamuzi wake wa kuchagua kusimamisha mechi kwa muda na sio kusitisha kabisa. Mchezo ulianza tena, penati ilipigwa, na matokeo ya haki yalipatikana

1773814596453.png
Lakini pia wanaamini Utekelezaji wa kifungu cha 84 ni dhuluma. Wachezaji wa Senegal walirejea uwanjani na mwamuzi alithibitisha hilo, mechi ikaendelea hivyo kifungu cha 84 hakiwezi kufanya kazi

Soma: Senegal wapokwa ubingwa wa AFCON 2025 na CAF, apewa Morocco

FSF imewaandikia barua CAF ikitaka wasimamishe utekelezaji wa uamuzi huu na kusitisha taratibu zote za kutoa kombe kwa Morocco ikisubiri usuluhishi wa mwisho lakini pia imeeleza nia yake ya kwenda kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) ndani ya saa 48 zijazo ili kutengua uamuzi huu.

Kwenye barua hiyo FSF imeomba kupata ripoti ya waamuzi na maafisa wa mechi hiyo ndani ya masaa 24, isipopata itafungua kesi ya dharula CAS.

=====

STATEMENT FROM SENEGAL FA

The Senegalese Football Federation has strongly condemned CAF’s decision, describing it as:

“Unfair, unprecedented, and UNACCEPTABLE… bringing disrepute to African football.”

FSF confirms it will take the matter to the Court of Arbitration for Sport (CAS) in Lausanne as they move to defend the rights and interests of Senegalese football.

They also reaffirm their commitment to integrity and sporting justice, promising to keep the public updated on developments.

1773817261460.png

1773817276604.png
 
CAF wahuni tu ni kama TFF wamekumbatia VAR ndani harafu wanawahukumu marefa kwa kupitia Azam Tv
 
Back
Top Bottom