John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
#TeamSenegal imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuifunga #TeamMisri kwa penati 4-2 katika mchezo wa fainali ulichezwa kwenye Uwanja wa Olembe jijini Yaounde, Cameroon.
Timu hizo zilimaliza dakika 120 za mchezo huo kwa suluhu ya 0-0, hivyo kwa matokeo hayo ya penati #TeamSenegal imetwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza baada ya kucheza jumla ya fainali tatu za AFCON.
Mchezo huo ulikuwa wa ushindani mkali lakini #TeamSenegal ndiyo ambao walitawala muda mwingi.
Fainali hiyo iliwakutanisha mastaa wa Liverpool, Mohamed Salah na Sadio Mane ambao Mane alishindwa kufunga bao la mapema kwa #TeamSenegal baada ya kukosa penati katika kipindi cha kwanza.
#TeamMisri walikuwa wakiwania taji lao la nane baada ya kuwa wametwaa mara saba (1957, 19591, 1986, 1998, 2006, 2008 na 2010), wakati #TeamSenega waliingia fainali mara mbili (2002 na 2019) na kuishia kuwa washindi wa pili kabla ya ubingwa huo wa kwanza kwao.