Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Shirikisho la Soka la Senegal limemfuta kazi kocha mkuu Pape Thiaw na benchi lake lote la ufundi baada ya kutolewa katika hatua ya 32 bora, wiki chache tu baada ya kusaini mkataba mpya kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia la FIFA.
Senegal ilikuwa ikitarajiwa kuwa miongoni mwa timu zitakazowania ubingwa wa Kombe la Dunia, baada ya kuifunga Morocco katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Januari 2026. Hata hivyo, walikuwa na kampeni ya kusikitisha, wakipoteza mechi zao mbili za mwanzo za hatua ya makundi dhidi ya Ufaransa na Norway.
Soma: Pape Gueye atangaza kususia Timu ya Taifa ya Senegal kama benchi la ufundi halitabadilishwa
Katika hatua ya 32 bora, Senegal walipoteza uongozi wa mabao 2-0 huku zikiwa zimesalia dakika tano kabla ya mchezo kumalizika dhidi ya Ubelgiji, ambao ulisawazisha na baadae kushinda kwa mabao 3-2 baada ya muda wa nyongeza.
Gazeti la kila siku la Ufaransa, L'Equipe, limeripoti kuwa Patrick Vieira, mshindi wa Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa na mzaliwa wa Dakar, Senegal ni mmoja wa wanaotajwa kuchukua nafasi ya
Thiaw, mwenye umri wa miaka 45.
Shirikisho la Soka la Senegal limetangaza kuwa litafanya mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu.