Seneta Methu, akiwa mbele ya Rais Ruto: Rais Ruto nakuheshimu ila sikuogopi...

Seneta Methu, akiwa mbele ya Rais Ruto: Rais Ruto nakuheshimu ila sikuogopi...

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
Seneta John Methu alimkabili Rais William Ruto wakati wa ibada ya mazishi ya Mbunge wa Ol Kalou marehemu David Njuguna Kiaraho katika Kaunti ya Nyandarua.

Wakati wa ibada hiyo, Methu alimwambia Rais kuwa anamuheshimu lakini hamwogopi. Kauli hizo, ambazo pia zilijumuisha ukosoaji wa utendaji wa serikali, zilisababisha timu ya vyombo vya habari kwenye hafla hiyo kumzima kipaza sauti kabla hajamaliza hotuba yake.

Mbunge huyo alianza kwa kudai kuwa marehemu Kiaraho alikuwa amewaonya viongozi wa eneo hilo dhidi ya kujiunga na chama cha United Democratic Alliance (UDA), akisema ni chama kibaya, kabla ya kumgeukia Rais na kusema kuwa hamwogopi.

“Wakati tuliingia chama cha UDA, mheshimiwa Kiaraho alituambia hiyo chama ni mbaya hataingia, akaingia Jubilee, na watu wa hapa Ol Kalou mkamchagua. Kwanza kabisa mheshimiwa William Ruto, bado mimi ndio John Methu. Sijabadilika, Bado mimi ni Methu wa zamani,” Methu alisema

“Na Ile maneno mheshimiwa Kwenya unaogopa ati nisiseme hapa, sitasema lakini ukinisukuma sana nitasema. Mimi nataka nikuambie nikiwa hapa kwasababu sijakuona kwa siku mingi kama Methu nakuheshimu sana mheshimwa rais. Nakuheshimu kama mzazi lakini nataka nikwambie sikuogopi.“

Mzozo huo ulizidi pale Methu alipomtambulisha aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kama “Naibu Rais wa wananchi.” Baada ya kipaza sauti kuzimwa, Mbunge wa Kinangop Thuku Kwenya aliingilia kati, na afisa wa itifaki alimtoa Methu jukwaani.

 
Back
Top Bottom