Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Bunge la Seneti la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) limepitisha uamuzi wa kumuondolea aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila, kinga ya kutoshitakiwa, hatua inayomfungulia njia ya kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma mbalimbali zinazomwandama.
Joseph Kabila, ambaye alirithi uongozi wa taifa hilo mwaka 2001 baada ya kuuawa kwa baba yake, Laurent-Désiré Kabila, alikabidhi madaraka kwa njia ya amani mwaka 2019, na kumuunga mkono rais wa sasa, Félix Tshisekedi, katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini humo.
Pia soma > Kabila: Uongozi mbaya wa Rais Tshisekedi umezididsha mzozo
Katika kikao kilichofanyika Alhamisi, Mei 22, 2025, takriban maseneta 90 waliunga mkono hatua hiyo, huku watano pekee wakipinga. Spika wa Seneti, Jean-Michel Sama Lukonde, alitangaza rasmi kuwa Seneti imeidhinisha Kabila kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, na hivyo kumvua kinga aliyokuwa nayo.
Kinga hiyo ya kudumu ilitokana na hadhi ya "Seneta wa Maisha" aliyopewa baada ya kuondoka madarakani, hatua iliyomkinga na mashitaka yoyote ya kisheria.
Mwendesha Mashtaka wa Jeshi la DRC ndiye aliwasilisha ombi kwa Seneti kumuondolea Kabila hadhi hiyo, kwa lengo la kuanzisha mchakato wa kisheria dhidi yake.
Kabila (53) anatuhumiwa kuwaunga mkono waasi wa kundi la M23 linalopambana na majeshi ya serikali na kudhibiti maeneo kadhaa yenye utajiri wa madini katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.
Hivi karibuni, Kabila ambaye amekuwa akiishi nje ya nchi tangu kuachia madaraka, alijitokeza hadharani na kumkosoa Rais Tshisekedi kuhusu namna anavyoushughulikia mgogoro wa mashariki mwa DRC. Pia alitangaza mpango wa kurejea nchini kusaidia katika juhudi za kutafuta suluhisho la kudumu kwa mzozo huo.
Pia soma >