Haya mambo yananifanya nisisome mwaka huu, nina watu wamenishauri nisiingie UDSM ni kugumu masupervisor wanasumbua, kuna watu wanajua wanaandika sana na wako vzr upstairs ila wanakwamishwa na supervisors. Mtu anatuma kazi inakaa miezi mitatu na majina yao ninayo, na wengine wanasumbua wanakubaliana na supervisor wakienda kwa discussant anataka afanye anachotaka yeye, ukinde kwenye study committee unabdilishwa tena sasa wenyewe kwa wenyewe hawajielewi wanavuruga watu alaf ukichelewa kumaliza kwa wakati una lipa ada mpya. Nimepata nafasi ila siendi UDSM bora niende Ardhi.
Lakini pia nimeshauriwa na mfanyakazi wa hapo akisema usisome hapa UDSM utachizika.
Kwa hiyo hao UDSM wanajikuta wakina nani hv kwa mfano? Sitaki tena kusoma PHD hapo, bora Ardhi. Na kama uko hapo unasoma PHD muda ukipitiliza usikubali kama ni uzembe wa supervisor au wasimamizi, mil 4 ni nyingi sanaa kwa kweli, msikubali kudhulumiwa kabisaaa.
UDSm sio sehemu nzr ya kusoma PHD hata ujitahidi vp utasumbuliwa tuu na ukichelewa kumaliza kupitia hiyo waraka wao utalipa ada tena full hadi ukonde ubaki mfupa.