voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,935
Ilikuwa rahisi zaidi Rais angetutangazia idadi yetu, kwa kulihutubia taifa, na Dunia nzima kupitia vyombo vya habari.Na tungeelewa bila kuharibu mapesa ya walipa kodi.
Badala Kutumia Mamilioni kama sio mabilioni, eti kisa Sherehe ya kutangaza Matokeo ya Sensa,Ni ubadhirifu mkubwa kwa pesa za Watanzania.
Ni kwa utajiri gani ilionao nchi hii hadi kufikia kuwa inafanya Sherehe zisizo na tija kama hizi,kila mwezi hapa nchini?
Hivi hao wafadhili wanaotoa hizo fedha na kuifadhili miradi hii,huwa wanafurahia sherehe kama hizi?
Hivi tunafurahia kipi baada ya kujua idadi yetu nchi nzima?
Tulipaswa kufanya sherehe kama hizo endapo tungekuwa walau tumefanikiwa kuzifuta mojawapo ya kero kubwa za kitaifa kama vile "Umaskini",:Ujinga","Njaa" na "Maradhi".
Lakini tunaposherehekea kuwajua watanzania wanaoteseka bila hata kuwa na Uhakika wa mlo wao!
Huku tukishindwa kupata suluhisho la utatuzi wa matatizo lukuki yanayoliandama taifa!
Huu unakuwa ni ubadhirifu mwingine tena mbele ya rais wa nchi mwenyewe akishuhudia!
Serikali inayotumia mabilioni ya pesa kutuhesabu raia,ambao hata milo miwili ni tatizo!
Serikali inayotumia mabilioni kwa gharama za kututajia idadi ya watanzania,mpaka na helkopta zinarushwa!
Serikali ya matabaka Mawili moja la Walamba "Asali" na Walamba "Shubiri"
Serikali ya matabaka ya "Walala Hai" na
"Walala Hoi"
Serikali ya matabaka Mawili ya "Wapanda Bodaboda" na "Wapanda V8"
Serikali ya matabaka mawili ya "Royal Tour" na "Roho Tua"
Halafu anatokea Mtu asie na "SHAKA" na kutuambia tumuunge mkono "Queen Safari"
Mambo haya yakiendelea kuachwa yalivyo.
Alamsikhi!