Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Sensa ilipoanza nilisema walioandaa sensa hawajawahi kushiriki sensa, hii ilitokana na aina ya maswali yakiwemo ya uchuro, yaani umewahi kufiwa humu ndani.
Leo nimeulizwa namba ya mita ya umeme, nategemea watarudi tena kuuliza namba ya mita ya maji. Kingine ni je, unategemea kuifanyia matengenezo nyumba.
Ni nini faida ya swali hili kama si kuchoshana tu, hivi kuna nyumba isiyofanyiwa matengenezo! Kwa ujumla maswali yaliyoulizwa leo tayari yako kwenye sensa halisi ya mwanzo, kama nilijibu nyumba yangu ina choo cha shimo basi hiyo nyumba ipo kweli japo leo hawakuuliza aina ya choo.