Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Semina zinazoendeshwa nchi mzima Kwa makarani wa sensa, zingeweza kupangwa vizuri tungeokoa pesa nyingi za umma na kuzielekeza kwenye maeneo mengine.
Mfano kulikuwa na ubaya gani kama wajumbe wa nyumba kumi na wenyeviti wa serikali za mitaa ,ambao ninauhakika wanawajua watu wao vizuri zaidi ,ndio wangepewa jukumu la kuhesabu watu Kila mtu Kwenye mtaa wake? Nini kingekosekana?
Nina uhakika Hawa wangepewa semina zoezi lingefanikiwa zaidi Tena Kwa mda mchache sana.mikusanyiko ya maseminari mikoa na wilaya zote Tena semina wanakaa mpaka siku tatu au nne na kwingineko mpaka Tano, wanalipwa posho na malazi.
Mimi naona kulihitajika mbadala Ili kuokoa pesa za umma,zoezi la sensa ni la siku Moja tu lakini semina zinafanyika wiki nzima hayo ni matumizi mabaya ya pesa, wakati mwingine tuwatumieni Hawa viongozi wa mitaa, itasaidia zaidi kuokoa gharama na kusafirisha watu Kwa ajili semina tu