Tanzania ni miongoni mwa taifa linaloyoshiriki katika mchakato wa kupata idadi ya raia wake kwa mfumo wa sensa. Sensa ya watu na makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo sensa ya mwisho kufanyika nchini kabla ya mwaka huu 2022 ilikua sensa ya mwaka 2012 na kufikisha jumla ya sensa sita kufanyika nchini baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, na mwaka 2002. Serikali huitaji idadi ya raia wake kwaajili ya maswala mbalimbali ya kitaifa kwani takwimu hizo huelezwa hutumika katika upangaji wa maendeleo na faida nyingine nyingi.
Mwaka huu 2022 serikali imetumia kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 400. Kiasi hiki cha fedha ni kikubwa sanaa kulinganisha na faida itakayotokana na kujua idadi ya raia kwani zipo sehemu nyingi ambazo pesa izi zingeweza kutumika na kuleta chachu ya maendeleo pasipo kuadhiriwa na kutojua idadi kamili ya raia. Mfano idadi ya wanachuo wasio na mikopo elimu ya juu inafahamika imetumika vipi kuwapatia ufumbuzi wa kuwapatia mikopo ikiwa serikali haina fedha za kutosha kuwapatia mikopo wote, ni wazi sio kila takwimu ni muhimu kwenye maendeleo kama hakuna mipango au ukwasi toshelevu.
Naamini zipo njia nyingi na nyepesi za kupata makadirio sahihi ya idadi ya raia wa Tanzania kwani hata kwa kuratibu tuu vizuri idadi ya uzazi na vifo unaweza pata ongezeko la raia kwa mwaka husika kwani tunayo idadai ya raia tuliyoipata pitia sensa za awali. Ni kuchukua idadi ya waliozaliwa au kuhamia na kutoa idadi ya waliofariki au kuhama na kupata idadi ya ongezeko au punguzo la raia na njia nyingine nyingi kama kweli serikali itaweka utaratibu sahihi wa kutaka kupata idadi kamili ya raia wake pasipo kufanya sensa ya watu na makazi.
Njia nyingine ambayo serikali
ingeweza kupata idadi ya raia wake pasipo sensa ni kupitia mchakato wa utambulisho wa uraia uliofanyika nchi nzima. Kila Mtanzania mwenye miaka 18 alijitokeza na kutoa taarifa zake muhimu kwa makarani wa NIDA kwanu utaratibu ungewekwa vizuri kwa kutumia gharama zile zile wangeweza kuboresha namna ya ufanyaji wa zoezi lile likasaidia pia kupata idadi ya raia na makazi kwa kuokoa gharama ambazo zinatumika kwenye sensa.
Njia nyingine ambayo serikali ingeweza kupata idadi ya raia wake pasipo kutumia gharama kubwa na za ziada ni kupitia zoezi la uandikishaji wa posti kodi na majina ya mitaa kwani waliajiriwa watu na kuzunguka nchi nzima kila nyumba na mtaa kutoa namba za nyumba na majina ya mitaa ilishindikana vipi kupata pia idadi ya watu wa sehemu izo na idadi ya makazi kama kila nyumba na mtaa ulifikiwa na idadi ya makazi zilifahamika pitia zoezi hilo. Hapa serikali pia ingiweza kuua ndege wawili kwa jiwe moja na kuokoa pesa nyingi.
Vilevile waatalamu wangeweza kutumia makadirio tuu kujua ongezeko la watu na makazi na kuokoa fedha hizo na kuja kufanya sensa hata baada ya mika 20 kwani makadirio hayo yanaweza yasipishane sana na uhalisia utakaopatikana kwenye sensa huku wakijikita kwenye kutatua matatizo ya raia ambayo hayaathiriwi na kutokujua idadi ya raia.
Kabla ya serikali kutumia sensa kama sehemu ya kupata idadi ya raia naona walipaswa kutumia idara ya takwimu ya taifa kupata taarifa muhimu za watanzania wenye uhitaji au sehemu muhimu serikali ipeleke nguvu za fedha na miradi ya maendeleo. Mfano idadi ya wahitimu wanaomaliza vyuo naamini serikali inayo na ikitaka inaipata pasipo sensa kwanini pesa hizi zinazotumika kwenye sensa wasipewe mikopo ya riba nafuu vijana hawa au kuandaliwa mipango itakayo wawezesha kiuchumi.
Malengo ya serikali katika ufanyaji wa sensa hii ndo imenifanya kuwaza na kuona hakuna faida kubwa ya mfumo huu wa sensa pamoja na kuigharimu serikali gharama kubwa ya raslimali fedha, watu na muda kwani haijawahi kubainishwa wazi ni mipango ipi ya maendeleo iliyokwamishwa kwa serikali kutojua idadi kamili ya raia wake ila ipo miradi mingi iliyoshindikana kwa kukosa fedha na mingine ikishindikana kwa kukosa tuu ubunifu. Mfano kujua idadi ya vijana nchi nzima wasio kua na ajira au wasio na elimu inasaidia vipi kuwasaidia kama pesa iliyotengwa kwajili ya vijana haijawahi kutosha ata idadi ndogo ya waombaji wa mikopo husika.
Pamoja na serikali kua na idadi ya raia kupitia sensa mbalimbali bado pamekua na changamoto ya kutimiza mahitaji ya raia hao kutokana na idadi ya raia. Mfano idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa darasa la kwanza, kidato cha kwanza na sita inafahamika ila serikali imeshindwa kutimiza kiwango cha fedha kwaajili ya ujenzi wa miondombinu ya shule kama madarasa na madawati na hata uwiano kati ya waalimu na wanafunzi haikakisi viwango vinavyopaswa, sasa sensa itaweza saidia kwenye hili wakati lipo wazi, na hapo ndo nawazwa kwanini pesa zote za sensa zisingetumika katika elimu, changamoto hii pia ipo kwenye idara na wizara nyingi kwani hata kwenye afya linafanana na mfano huo wa elimu, naona ni wakati wa serikali kutatua kwanza changamoto ambazo zinaonekana kwa macho kabla ya kutafuta takwimu na idadi ya watu.
Bado kama taifa tunapambana na maadui watatu ujinga, maradhi na umasikini ambapo bado tunaweza kukabiliana na maadui hawa pasipo kujua idadi ya raia kwani bado hatujawahi pata ziada ya fedha au bajeti ikarudi serikalini kwa kutosheleza idadi ya watu hivyo sio busara kupeleka pesa kwenye kutafuta idadi ya raia ambao shida zao zipo wazi na unaweza zitatua pasipo kujua idadi yao. Mfano ni Mbunge yupi alishawahi kuja na kero mpya au shida mpya inayowakabili wananchi mbali ya zile tuzilizozizoea kama ubovu, achakavu au ukosefu wa miondombinu, shida katika elimu au afya na nyingine nyingi ambazo nyingi zinaweza tatuliwa pasipo sensa ya watu na makazi.
Idadi ya wakulima, viwanda, mito, maziwa na sehemu muhimu za vyanzo vya maji yanayoweza kutumika katika kilimo inafahamika, sehemu zenye rutuba na maeneo makubwa ya kilimo Tanzania zinajulikana, idadi na aina ya mazao ya chakula na biashara yanafahamika na hata takwimu za mavuno ya nafaka na mazao yote zipo ila changamoto kubwa ni masoko ya uhakika na bei yenye tija ndo kilio cha wakulima wengi pamoja na ukosefu wa chanzo cha uhakika cha maji kweli na hili tunahitaji sensa kuyatatua? Hapana ni nia ya dhati na mikakati ya muda mfupi na mrefu na fedha yanaweza kuamaliza haya na hapa ndo idadi kubwa ya Watanzania wanategemea sekta hii ilikua pia ni busara pesa zilizotengwa kwa sensa zingeingizwa huku na kutumia akili nyingine ya kupata makadirio ya idadi ya watu kwani pesa iliyotumika kwa sensa mwaka huu unaweza kopesha wakulima 40,000 kila mmoja ukampa mtaji wa shilingi za kitanzania 10,000,000 binafsi naona ingekua na msaada mkubwa katika kuwaondoa vijana wengi na wananchi katika kujikwamua kiuchumi kuliko faida inayopatikana kwenye sensa.
Bado naamini maendeleo yanaweza patikana hata pasipo kupitia michakato mikubwa ya kisayansi kama sensa inayogharimu fedha nyingi huku ukiwa bado una safari ndefu ya kutatua kero za za awali ambazo pamoja na kua na idadi ndogo ya raia katika takwimu bado hapakua na utoshelevu wa kifedha. Kabla ya Raisi wa nchi wapo wasaidizi wengi sana wanaoweza kuakisi hali halisi ya sehemu wanazoishi kiuchumi pasipo kuathiri fedha za ziada na wakawa na makadirio halisi ya idadi ya wahitaji.Ukiwauliza watendaji wa mitaa ni nyumba ngapi hazina vyoo salama na maji watakupa idadi kamili, ukimuuliza Daktari mkuu wa wilaya akupe idadi ya vizazi hai na vifo kwa mwaka fulani anaweza kukupatia na kutumika katika maendeleo pasipo sensa, hivyo hivyo katika idara mbalimbali kwani ata afisa ardhi na makazi anajua ametoa vibali vingapi vya ujenzi ni kuweka na kusimamia utaratibu utakao wezesha kupata takwimu sahihi pasipo gharama mpya.
Hitimisho;
Ukweli zipo baadhi ya faida za sensa katika taifa changa kama Tanzania ila ni ndogo kulinganisha na gharama zinazotumika katika zoezi hili kwani hakuna uhaba mkubwa wa takwimu mbalimbali zinazoweza kutumika katika maendeleo ambazo zinakosekana kwa kutumia vyanzo vingine vya kupata takwimu kwani unaweza kutafuta idadi ya raia sehemu ndogo tuu ambayo unaelekeza huduma yako unayohitaji kupata idadi kamili ya raia na kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo ungetumia kuhesabu maeneo ambayo hutayafikia kihuduma kwa muda husika huku ukiwa na makadirio ya idadi ya nchi nzima kama njia tajwa huko juu za kupata idadi ya raia hazitutumika.(Andiko langu halijalenga kukosoa sensa yetu ila emelenga kutoa mawazo mbadala katika hili kwani sensa ni kwaajili ya maendeleo na ni muhimu ndio maana sikutoa chapisho langu mapema kipindi cha sensa ilivyokua ikifanyika)

Upvote
5