Habari nyote
Niende tu moja kwa moja katika hoja yangu na nianze na swali rahisi kabisa, Kuna umuhimu gani wa kufanya sensa ya watu na makazi wakati tukiwa katika kipindi kigumu sana cha ongezeko la bei katika mahitaji mengi ya watanzania na duniani kote?
Natambua umuhimu wa sensa ya watu na makazi kwa nchi yetu lakini napata ukakasi kuamini kuwa sensa hii ni muhimu sana kuliko watanzania wenyewe!
Siku za karibuni, tumeshuhudia ongezeko kubwa la bei kwa bidhaa mbali mbali kama vile mafuta ya kupikia, petrol, diesel, mafuta ya taa, sabuni aina zote, vyakula nk.
Lakini Nchi ya Tanzania Iko kimya kabisa kuzungumzia suala hili kwa mapana yake.
Namsikia mama akisema ni kutokana na Covid 19 ambayo haipo kwa sasa/imepungua lakini sababu nyingine ni mgogoro wa kivita kati ya Russia na Ukraine ambayo ndiyo sababu kubwa kwa sasa inayozungumziwa kila pahala.
Viongozi wetu tulio waamini wanashindwa hata namna ya kumshauri Rais, athari za ongezeko la bei katika nchi yetu. kinachoshangaza zaidi ni kutokuwa na backup plan ya What if bei duniani zikiongezeka, Tanzania ifanye nini kuzuia suala hili, wachumi wa nchi hii walio wengi wako kimya. Waziri wa fedha anatabasamu tu.
Sioni sababu ya kwanini, Tanzania ijikite katika sensa ya watu na makazi, kwa kutumia pesa nyingi sana kwa zoezi hili ambalo lingeweza kusubiria wakati mzuri zaidi hapo baadae na fedha hizo zikawekwa katika kupunguza mfumuko wa bei hasa kwenye mafuta ya aina zote!
Bado napata ugumu kuamini kuwa sensa hii ni muhimu zaidi kuliko namna ya kuthibiti mfumuko wa bei, kwa kutumia fedha hizo kuwezesha wakulima wakubwa, wafugaji wakubwa kuendelea kutoa huduma bila kuathiri bei.
Karibu tujadiliane tuone, Je Sensa ni muhimu sana kuliko hali za watanzania?
Nini kifanyike.