SoC02 Sensa ya watu na makazi 2022

SoC02 Sensa ya watu na makazi 2022

Stories of Change - 2022 Competition

0768404968

New Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
3
Reaction score
0
Maana ya sensa: Ni utaratibu wa kitakwimu wa kuhesabu, kuchambua na kutunza kumbukumbu za watu na makazi. Kwa mjibu wa sensa nchini Tanzania, ilianza baada ya nchi kupata uhuru. Hivyo imekuwa Kila baadae ya miaka kumi kunakuwa na zoezi la sensa ya watu na makazi. Sensa Ina umuhimu sana katika Kila taifa hususani Tanzania kwa sababu ni kichocheo kikubwa Cha maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Maendeleo yanakujaje? Maendeleo yanakuja hasa kwa kuangalia uwiano uliopo katika uzalishaji au kipato Cha mtu mmoja kwa kulinganisha mchango wake katika kipato Cha taifa, yaani kwamba je, mtu anazalisha kiasi Gani na anamchango Gani kwa kile kipato anachokizalisha. Nashukuru time ya taifa ya takwimu za watu na makazi kwani wanaofanya hivi kwa lengo la;

1. Kuangalia makundi ya watu, ambao ni kundi la watu tegemezi kama vile wazee wenye umli WA miaka 60 na kuendelea, lakini pia Kuna kundi la watoto, Kuna watu wenye ulemavu WA viungo na akili, na pia kubwa zaidi kuangalia nguvu kazi ya taifa na jamii kwa ujumla. Hii inasaidia Serikali kutambua uwepo makundi tegemezi na watu wanaoweza kufanya kazi kwa kuhusishanisha mahitaji ya Kila mmoja na mchango wake katika maendeleo ya taifa.

2. Kutoka huduma Za kijamii, sensa inalenga kuangalia upana WA uhitaji wa huduma Za jamii na upatikanaji wake. Mfano WA huduma Za jamii ni kama vile hospitali, Shule, maji, Barbara, umeme, chakula pamoja na mitandao ya kijamii au mawasiliano. Serikali Ina lenga kufikisha huduma hizi katika Kila sehemu inayokalwa na watu.

3. Kuangalia mtawanyiko wa watu nchini. Mjibu wa Serikali ni kutambua maeneo yaliyo na mkusanyiko mkubwa WA watu na pia kuangalia maeneo yasiyo kuwa na mkusanyiko mkubwa WA watu hivyo kupanga tathiini ya huduma zinazohitajika mahalo husika.

4. Kufanya tathiini ya sensa iliyopita na sensa ijayo, kuangalia hasa maendeleo yaliyokuwepo kwa kuyahisishanisha na maendeleo yaliyopo na kapanga tathimini ya maendeleo kwa miaka kumi ijayo.

5. Kuangalia Hali ya vizazi na vifo. Sensa inasaidia kujua ongezeko la watu na pia kujua idadi ya vifo vilivyotokea ndani ya miaka kumi iliyopita, kwa kubainisha visababishi au vyanzo vya vifo hivyo, eidha ni maradhi, ajali, kupigwa au kwa namna yoyote Ile. Na hii ni kwa lengo hasa la kujua namna ya kupunguza vifo hasa kwa mama na mtoto katika kipindi Cha izazi. Serikali ililenga kiwahesabu watu wote pamoja na rasilimali walozonazo.

Lakini, kumetokea na changamoto kubwa sana la sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 iliyofanyika kuanzia tarehe23/8/2022. Baadhi ya changamoto hizo ni kama zifuatazo:
(a) Kufanya tathimini ya majenjo; ni kweli kujua idadi ya nyumba zilizopo nchini ni jambo zuri na ni la muhimu sana hasa katika kujua kama ni jenjo la namna Gani, Lina sofa zipo au hadhi Gani.

Changamoto iliyokuwepo hapa ni kwamba wananchi wengi waliokuwa wanajiuliza kwa Nini tunaulizwa gharama za majengo yetu wakati huo Serikali haijanyoosha mkono wake kumsaidia ujenzi, vifaa vya ujenzi vinapanda bei Kila inapoitwa Leo na hata haiangalii mtu WA chini ananafasi Gani katika makazi, lakini pia wengine waligoma kuweka tathimini ya ukweli kwa kudhania kuwa Serikali wanataka kufanya kitu Cha tofauti Cha sitofahamu kuhusiana na majengo kwani haijawahi kutokea. Lakini pia wapo watu waliosisitiza nyumba zao zihesabiwe na kuweka msisitizo kwa Serikali kuwa waangalewe kwani sehemu wanazoishi SI nyumba balo ni vibanda tu vya kijikinga na hatari, hivyo wakaomba kusaidiwa. Swali kwa Serikali.

Majibu ya Serikali yamekuwa hivi kwamba wanataka kuangalia endapo zipo nyumba zinazokidhi hadhi ya kimataifa. Je Hilo ndilo jibu kwa wananchi? Ndiyo zipo baadhi lakini ni kwa asilimia ngapi? Serikali itoe majibu mazuri ya kumridhisha raia kwa sababu ukisema nyumba zinazokidhi hadhi ya kimataifa ni kivipi umemsaidia mtu wa chini afikie viwango hivyo au ndo yaleyale ya kuendelea kamdidimiza chini?
Tafadhali Serikali itafute namna ya kuwainua watu wake.

(b) Maswali yaliyoulizwa katika kishikwambi megine yalikuwa hayana tija. Laiti watakwomu wangechambua Maswali ya muhimu sana na hasa kujua Hali halosi ya maisha yake, Pato lake kwa mwaka, Hali ya kiafya hasa kwa magonjwa sugu kama vile UKIMWI, kisukari TB na magonjwa mengineyo hii ingesaidia sana namna ya kuweza kawasaidia watu walio na uhitaji sana. Wapo watu ni wazima lakini Hali Yao ya kimaisha ni ya shida sana hivyo wangeulizwa Hali zao za kimaisha Ili katafuta utaratibu mzuri WA kuweza kuwasaidia.

(c) Ghalama ya sensa imekuwa kubwa sana, sensa ya mwaka huu imekuwa na Ghalama za Hali ya juu mno ukilinganisha na Pato la taifa, mfano kununua vishikwambi, kuchapisha machapisho mbalimbali lakini pia malipo kwa watu wote waliohusika na swala Zima la sensa. Serikali imetumia pesa sana kiasi kwamba unaweza kukuta baadhi ya mambo yakakwama kutokana na uhaba WA pesa na tozo kuendelea kuongezeka.

Mwisho, sensa ni nzuri na ni muhimu kwa taifa letu, lakini Serikali inapopanga mkakati WA kufanya sensa kwa madhumuni ya maendeleo basi iharibu kupunguza bei ya vitu, mfano pembejeo za kilimo, kuongeza beiya mazao, kufikisha huduma Za jamii mahalo pasipokuwa na huduma in lakini pia iangalie namna ya kumuinua mtu wa Hali ya chini.

Asanteni sana Wana jamii forum kwa shindano hili. Karibu kupiga kura, kuhoji na pia kunikosoa pale nisipofanya vizuri! Ni mara ya kwanza kuandika makala hii. So I am not perfect on it!!
 
Upvote 0
Back
Top Bottom