Jerlamarel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2021
- 843
- 2,525
Hii ni sensa ya watu na makazi, lengo kuu la sensa ni kupanga maendeleo ya muda mrefu. Unapoingiza siasa kwenye dodoso utaishia kupata data ambazo ni useless ndani ya mwaka tuu.
Pia kuna data zingine ambazo tayari serikali na vyombo vyake wanazo, sikuona haja ya kuwepo kwenye dodoso, ni kuwachosha makarani tuu na kuifanya kazi ya sensa kuwa ngumu sana na inayoboa kwa anayehojiwa.
Moja ya maswali ambayo ni useless kwenye dodoso la mwaka huu ni kama yafuatayo:
1. Namba ya simu
Kila siku watu wanabadili namba, baada ya mwaka tuu nusu ya data hizi huenda ziwe useless.
2. Mahali unaposhinda
Mahali mtu anaposhinda inasaidia nini kwenye maendeleo ya taifa? Hizi data ndani ya mwaka tuu zitakuwa obsolete maana asilimia kubwa hawatakuwa wanashinda pale pa mwanzo.
3. Kitambulisho na namba ya NIDA
Hizi data tayari zipo NBS. Kuziuliza tena kwenye dodoso ni kuwachosha makarani tuu.
4. Kitambulisho cha ujasiriamali
Huu mradi ulishasitishwa siku nyingi. Unawekwa kwenye dodoso kwa lengo gani wakati toka mwendazake aondoke na wenyewe ukasitishwa na hivi vitambulisho havitambuliki tena?
5. Simu janja na Kompyuta
Hizi data zote ziko pale TCRA, wao ndiyo wanajua exactly namba ya hivi vifaa vilivyopo hewani. Kwa vyovyote vile data watakazopata makarani hazitaendana na za TCRA maana siyo wote watatoa data kamili, kwa maswali yalivyo mengi watu wataamua kufupisha kwa kujibu "HAPANA SINA".
6. Uzazi na vifo
Hizi data zinatumwa kila mwezi kwenye wizara zinazohusika. Kuziuliza tena kwenye dodoso ni kuwachosha makarani tuu.
7. Anuani ya makazi
Hili zoezi limefanyika juzi tuu. Kwa kuwa visimbuzi vinatumia GPS nilitegemea kila kikifika kwenye kaya husika basi automatically kidetect kama nyumba ina anuani ya makazi ama laah.
Ongezeeni mengineyo...