Sensa ya Watu na Makazi: Tuliulizwa kama unafuga ng'ombe, mbuzi, kuku. Lakini kwanini hatukuulizwa kama unafuga Nguruwe na Mbwa?

Sensa ya Watu na Makazi: Tuliulizwa kama unafuga ng'ombe, mbuzi, kuku. Lakini kwanini hatukuulizwa kama unafuga Nguruwe na Mbwa?

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Ina maana kama Taifa hatuhitaji kujua hali ya ufugaji wa huu mfugo utupatiao kitimoto kilicho mkipenzi cha wengi?

Je, hakuna mpango wa kuendeleza ufugaji wa nguruwe? Je hakuna haja ya kujua tuna mbwa wengi kiasi gani?

Kama ni hivyo tutapangaje mpango wa kuwachanja mbwa dhidi ya kichaa cha mbwa kama hatuhitaji kujua hali na kiasi cha ufugaji wa mbwa??
 
Hakukuwa na mengineyo mwisho? Ungempa taarifa karani ili dodoso liboreshwe siku nyingine.Onesha uzalendo.
 
Panya, sungura,senene nk mbona wewe umewasahau.
... majini na wewe umeyasahau. Ingesaidia kupata picha ya kiwango cha ushirikina, uganga, na ulozi nchini na kuweka mipango ya kupambana imani za kishirikina ambazo ni tatizo linalozidi kuota mizizi nchini!
 
Hata huko Iringa hawakuulizwa kuhusu ufugaji wa kile kitoweo chao?
Kama hivyo basi next time dondoo za maswali zirekebishwe ili ziendani na mazingira ya mahali watu walipo
 
Mama, kama atakuwa anagive a damn kwa kila jambo (kitu ambacho sidhani maana angekuwa ameshakasirika na kuachilia mbali), atafika 2025 au 2030 akiwa amechoka sana. Usipouelewa huu uzi unaweza kudhani ni wa kawaida tu, kumbe una jambo zito mno la giza nyuma yake mtoa mada amelenga liibuke katikati ya mjadala.
 
Unataka karani muisilamu aulize kuhusu nguruwe! Labda ungesema mchuzi wake.
Kuhusu mbwa nalo ni haramu kumuuliza muisilamu.
Kwani serikali ina dini? Kwani kuuliza kwenye dodoso kama kaya in mifugo hiyo na hiyo kaya ikajibu haina hapo tayari itakuwa umetenda dhambi? Tuna safari ndefu sana ya kujikomboa kifikira.
 
Ina maana kama Taifa hatuhitaji kujua hali ya ufugaji wa huu mfugo utupatiao kitimoto kilicho mkipenzi cha wengi? Je hakuna mpango wa kuendeleza ufugaji wa nguruwe? Je hakuna haja ya kujua tuna mbwa wengi kiasi gani? kama ni hivyo tutapangaje mpango wa kuwachanja mbwa dhidi ya kichaa cha mbwa kama hatuhitaji kujua hali na kiasi cha ufugaji wa mbwa??
Kwani kondoo wametaja?
Ng'ombe
Mbuzi
Kondoo
Punda
Nguruwe
Kuku.
WOTE HAO WAMERAJWA
KWENYE DODOSO.
 
Unataka karani muisilamu aulize kuhusu nguruwe! Labda ungesema mchuzi wake.
Kuhusu mbwa nalo ni haramu kumuuliza muisilamu.
Sasa dini na dodoso za kujua idadi ya wanyama vina uhusiano gani mi naona kama maslahi ya nchi yataelemea itikadi flani huoni nchi inaweza isifike popote kimaendeleo. Kwa maana mtu kujua mfano kama una nguruwe au laah kuna punguza ama kuongeza nini kwenye dini yake. mi naona mtazamo wako ni very pesmistic in nature
 
...huoni nchi inaweza isifike popote kimaendeleo. Ukitaka kujua tulipo tazama nchi zilizopata Uhuru nyuma yetu, utajua sisi tupotupo tu, wenzako uchaguzi ukiisha wanaanza lampeni za uchaguzi ujao! Kwao muhimu ni madaraka, maendeleo ni yao ya binafsi ya utajiri.
 
K
Mkuu mbingunikwetu, naunga mkono hoja, tena ule mwezi, mauzo huwa yanashuka!.

Japo hakukuwa na swali kuhusu jamaa hawa kwenye dodoso, lakini kazi ya kuboresha ufugaji huu inaendelea

P

..kazi ya kuboresha ufugaji huu! huu upi?
Hata huko Iringa hawakuulizwa kuhusu ufugaji wa kile kitoweo chao?
Kama hivyo basi next time dondoo za maswali zirekebishwe ili ziendani na mazingira ya mahali watu walipo
Iringa hao wadudu wanajitegemea kutafuta chakula na kulala.
 
Back
Top Bottom