Watutengenezee tuzitumie hata kurudishiana chenji, tunadhulumiana sana hizi senti senti huku mitaani.Hizo senti zenye thamani ndogo mkuu utazitumia kununulia nini katika hali ya sasa? Zilifaa wakati ule pesa yetu ikiwa na nguvu. Na mara nyingi utakuta hata gharama ya kuzitengeneza ni kubwa kuliko hata thamani yake. Ni hasara tupu !!!
[emoji3591][emoji3591][emoji3591] Ngoja wachumi waje wafafanue zaidi. Mimi sijui kitu [emoji2221][emoji2221][emoji2221]
Sawa watengeneze hata ya milioni lakini nadhani hizi sarafu za senti zinahitajika kwa chenji.Uchumi unakuwa. Muda si mrefu tutakuwa na noti ya Tsh.100000/=
KisunguraThumni
Nani anazikataa ikiwa ni pesa halali,?! Mimi nadhanizinasaidia kutoa chenji, an kuondoa dhana ya kuibiana, muhudumu dukani akikwambia sina chenji, an asipokurudishia chenji mnaweza kabana mashati. Mi nashaurizirudishwe hizi sarafu.Ni ishara ya kuwa pesa yetu imepungua thamani. Wewe unazungumzia senti wakati sarafu mpaka za shilingi 10 hakubaliki mtaani. Yaani sarafu ya mwisho inayokubalika kwa sasa ni shilingi 50, na kama tukisonga hivi hata hiyo ya 50 haitakubaliwa
Garama ya kuunda sarafu moja ya senti moja ni kubwa kuliko thamani yake.Swali langu nimeshindwa kuliframe vizuri. Nilitaka kufahamu hapo zamani tulikuwa na senti zinazunguka kwenye circulation ya pesa huku mitaani, lakini ghafla zilipotea, na sifahamu ni kwanini.
Nchi zingine hata walio tutawala bado wanatumia hizo senti, ukienda Ulaya yote, hata Marekani kuna senti kwenye mzunguko wa pesa zao.
Huku kwetu ziko kwenye mahesabu lakini hazipo physically, nataka kufahamu je, hii nayo ni njia ya kukuza uchumi kwa BoT kutotoa sarafu za senti tena, au tatizo ni nini?
Tunao wachumi wazuri humu na wataalamu wa masuala ya fedha, mtusaidie kwanini tuliziondoa sarafu za senti kwenye mzunguko wa pesa zetu?
Hamuoni tunadhulumiana, unakuta unaenda kutoa muamala una senti, lakini unapewa pungufu, unadai 100.15 mtu anakupa 100.00. Kwanini hatuoni kwamba hili ni tatizo kwenye pesa yetu?
Huko nyuma tulikuwa na senti tano, senti kumi, senti ishirini, senti hamsini, shilingi moja, shilingi tano, noti ya shilingi kumi, noti ya shilingi ishirini, noti ya shilingi hamsini, na noti ya shilingi mia moja.
Nataka kuuliza hizi senti kwanini tunaziondoa? Zina faida yoyote au ni hasara tu kuwa nazo?
Unadhani marekani na mataifa tajiri mengine wao hawaoni hizo gharama za utengenezaji wa hizo sarafu ndogo ndogo na kuendelea kuziweka kwenye circulation ya pesa zao?Garama ya kuunda sarafu moja ya senti moja ni kubwa kuliko thamani yake.
Tena walipoondoa zenye matundu ndio waliharibu zaidi kwasababu zile za matundu watu walizivaa kama shanga au zilitumika kama washeri za kufungia bolti.