Senzo alikuzwa sana kiuhalisia hamna kitu. Viongozi wetu wanaongea pembeni ila hawawezi mwambia Usoni

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
"yanga hii haina tofauti na yanga ile ya bila senzo. Viongozi tukikaa nao wanalalamika kuwa jamaa hana mchango,msaada wowote na hata walimwajiri ni kama wanashindwa wafanye nini naye.

anapenda sana starehe ila kiutendaji hana jipya hasa kwa sasa anaonekana kuwadharau wote na kujiona yeye pekee ndo katika yanga anaufahamu mpira.

sisi yanga tulitegemea angekuwa anatushauri jinsi ya kuendesha team kisasa, kupata wachezaji wazuri,makocha wazuri n.k


Hana mikakati yoyote endelevu zaidi zaidi tu hupenda kusema mimi nlipokuwa team xxx nlifanya 1,2,3... Tunapomwambia tupe mikakati hapa sasa tunaelekea wapi anakosa majibu.

Kiukweli hata maboss wenyewe wamepunguza sana kumshirikisha mambo amebaki tu kama ceremonial coz ni aibu kwa sasa kusema tulikurupuka. Ni bora tungemchukua mwinyi zahera. Si huyu jamaa.

Au pengine kuna mambo yanamkwamisha?au simba kipindi kile walikuwa wanamkuza tu kupitia manara but hamna kitu? Yanga tunahitaji kujenga team tena kimkakati.bila hivyo tutapata shida mbeleni.

Siku zote huwa naongea ukweli wacha nichukiwe. Ni kwamba either hatuna kazi za senzo kufanya pale kwetu au senzo haoni kazi za kufanya pale kwetu.

Kama tungeweza mchukua cr.magori wa simba tungekuwa tumelamba dume kuliko hili galasa la south africa ambalo lilikimbilia kwetu baada ya kupata taarifa linataka temwa simba kwa kutoona mchango wake.

Ni bora yanga tungeajiri watu kama akina sekilojo chambua,ally mayai n.k watanzania wenzetu wenye kuufahamu mpira. But huyu tumelamba galasa. Alijengwa na simba kisiasa tu hamna kitu pale."

Haya yameandikwa na Mwanayanga katika group la whatsapp la Wanayanga. Si maneno yangu. Ni copy and paste.
 
Senzo wa watu mnamtupia mzigo wa bure tu..
Jamaa sio mtu wa vyombo vya habari anajua kazi yake, tumuache afanye kazi yake tunajua anapambana sana kuhusu mchakato wa kuibadilisha yanga muundo wake, hawa wanaopiga kelele halishindwa kuisadia Yanga miaka yote, Wenye akili wanajua tulipotoka, tulipo, na tunapokwenda.
 
"yanga hii haina tofauti na yanga ile ya bila senzo. Viongozi tukikaa nao wanalalamika kuwa jamaa hana mchango,msaada wowote na hata walimwajiri ni kama wanashindwa wafanye nini naye..
Yaani unachosema ni sawa na kusema "Serikali ya Kidiketa ya North Korea, inamlaumu Mtalaamu wa Masuala ya Demokrasia kwa sababu walitarajia angekuwa anawashauri jinsi ya kuendesha serikali"!

Man, huyo Mtalaamu wa Demokrasia wa North Korea ameenda hapo kuwashauri wabadili mfumo wa uendeshaji kutoka mfumo wa kidikteta hadi mfumo wa kidemokrasia unaoangalia rule of laws!
 
Kafanya kazi gani? Kuuza kalenda? Kufanikisha usajili wa Fiston?
 
Si Vyura walijisifu kuwa Wamempiga KO Dewj kwa kumnyakua Senzo kutoka Simba?
 
Senzo ni boya, alishindwa kuishauri Simba kupata kocha bora akamleta kishingo aliyekuja kuua viwango vya wachezaji, ni kweli anabebwa na jina pia watu aliofanya nao kazi.

Ceo mweledi hawezi kuacua kazi kupitia Twitter tena bila kukabidhi vifaa vya ofisi na pia mchezo wake wa kutaka kuhujumu Simba ni ujinga wa hali ya juu.

Toka Babra aingie Simba ameleta kocha wa hadhi inayoendana na Simba, kocha bora wa makipa, mtaalamu wa kusoma video lakini Senzo ameikuta na kuiacha Simba bila kuongeza chochote
 
Mnataka mbinu mpya wakati hela hamna.tafuteni kwanza pesa ya uhakika tofauti na hapo ni porojo tu maana inawezekana jamaa anaeleza vitu vingi ila utekelezaji wake unakwama kwasababu ya kukosekana ngawira ya uhakika.
 
Utopolo mlijisifu kuwa..... ANAYE SAJILI SIMBA KASAJILIWA NA YANGA
 
Hujui cv ya senzo,hujui tor aliyopewa senzo na yanga,unaropoka nini?
 
Mpira ni pesa bila pesa hata ukawa ni kiongozi gani hakuna kitu.
Bila pesa unaweza kuwa na mipango ila isifanyiwe kazi.
Hakuna mipango bila pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…