Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
- Thread starter
- #41
Ahsante sana mkuu kwa taarifa hii....Kuna Senzo wawili. Mmoja ni Senzo Robert Meyiwa. Huyu alikuwa mcheza mpira na goalkeeper was Orlando Pirates ya Afrika Kusini. Alikuwa pia kipa na kapteni wa timu ya Bafana Bafana. Senzo Meyiwa Aliuawa kwa kupigwa risasi na wezi Oktoba 26, 2014. Alifanyiwa mazishi ya kitaifa.
Mwingine ni Senzo Mthethwa. Huyu ni mwanamuziki wa gospel reggae. Kuna mkanganyiko kama yupo hai au alishafariki. Hata hivyo, nadhani mkanganyiko huu unatokana na kifo cha mchezaji mpira Senzo Robert Meyiwa.
Oktoba mwaka jana Senzo Mthethwa alitarajiwa ku-perform kwenye Sand Music Festival huko Malawi. Ila hasikiki sana na sidhani kama bado anatoa nyimbo mpya kutokana na kupoteza sauti yake baada ya kupata cerebral ya malaria. Labda ndio maana hasikiki. Ila mke wake alishafariki.
Ambacho nilikuwa sifahamu ni kama alishapona kiasi hiki cha kurejea kwenye muziki....
Nimefarijika sana na kufurahi sana kuone amerejea tena...
Welcome back Senzo...